PENGINE haya tunaweza kuyaweka kwenye kundi la madhara yatokanayo na utandawazi. Mitandao ya kijamii ipo inayowasaidia wanafunzi katika masomo yao na kazi, lakini wengine wanatumia mitandao hiyo visivyo.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa matumizi
mabaya ya teknolojia hasa mitandao ya kijamii yamechochea ongezeko la
uhalifu, ubakaji, matumizi ya dawa za kulevya na zaidi biashara ya
ukahaba vyuoni.
Mitandao ya ‘Facebook’, ‘Twitter’, ‘BBM’,
‘Instagram’ inafahamika kwa namna inavyoweza kuwaunganisha watu kutokana
na urahisi wake katika kuitumia.
Mwananchi Jumapili limebaini kuwa katika mitandao hiyo makundi mbalimbali yameanzishwa yakiwa na malengo tofauti.
Baadhi wameanzisha makundi kwa lengo la kujenga
mitandao ya kibishara, kidini, michezo, burudani, vichekesho na mengine
ambayo mara nyingi huwa wazi na yeyote anaweza kujiunga na kuona
kinachoendelea ndani.
Mbali na hayo ndani ya mtandao wa ‘Facebook na
‘BBM’ yapo makundi yanayoendesha biashara ya ukahaba, yakiwahusisha
wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali nchini.
Uchunguzi umebaini kuwa wanafunzi hao wanaofanya
biashara ya ukahaba kwa kutumia mitandao wameweka picha na namba kwa
ajili ya mawasiliano kwa mteja atakayekubaliana na bei waliyoweka.
Baadhi ya wanafunzi hao wanatumia mtandao wa
‘University Tanzania Jokes’, ‘Jicho la Mvulana Liko Fasta Kuliko
Google’, ‘Benki ya Utamu Tanzania’ na nyingine katika kufanikisha
biashara hiyo ya ngono.
Ukiingia katika mitandao ya Facebook, Twitter,
BBM, Instagram, utabaini kuwapo kwa makundi yaliyoundwa kutengeneza
mitandao ya ngono, ambayo huweka pia namba za simu za wahusika,
zikiambatana na picha, ambao ikiwa utaangalia picha na kuvutiwa, unaweza
ukapiga simu husika kuzungumza naye kwa kufanya mapatano kabla ya
kukubaliana.
Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwa
mwanamume anaweza kumpata msichana kutoka chuo kikuu chochote nchini
anayefanya biashara ya ukahaba kupitia mitandao hiyo.
Baadhi ya vyuo wanavyotoka wasichana wanaofanya
biashara hiyo na kujitangaza kwenye mitandao ni pamoja na Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo Kikuu cha
Mtakatifu Augustine (SAUT), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na Chuo cha
Usimamizi wa Fedha (IFM).
Kwa nyakati tofauti, waandishi wa gazeti hili
walitembelea makundi yanayojinadi kufanya biashara hiyo pamoja na
kufanya mawasiliano na wasichana watatu ambao waliweka picha na namba
zao kwenye mtandao.
Wasichana hao walijitambulisha kwa majina, vyuo na vitivo
wanavyosoma na baada ya kuwafuatilia kwa kuweka ahadi za kimapenzi
ilithibitika kuwa wanafanya biashara ya ukahaba huku wakiwa wanafunzi wa
vyuo vikuu.
Mmoja wa wasichana hao alijitambulisha kwa jina la
Bianca (sio jina lake halisi), ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa pili
Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Baada ya mwandishi kufanya naye mawasiliano
walikubaliana kukutana eneo la Udasa na muda wa ahadi ulipofika,
mwandishi alifika eneo hilo na kukutana na binti huyo ambaye aliiona
picha yake na namba ya simu kwenye mtandao, tofauti na alivyodhani awali
kuwa huenda wasichana hao wanatumia picha za watu wengine kujinadi.
Kutokana na lengo la msichana kuwa ni biashara ya
ngono, mwandishi wa gazeti hili alilazimika kumpeleka binti huyo katika
hoteli moja maarufu jijini, akimweleza kuwa inabidi wanywe pombe kwanza
kabla ya kwenda chumbani kwa makubaliano ya kumlipa Sh50,000.
Binti huyo alikabidhiwa fedha hizo ili
kumwaminisha uhalisia wa kuwapo hitaji na muda wa kwenda naye chumbani
ulipofika waliongozana lakini mwandishi akatoroka njiani akiwa
amethibitisha kuwapo kwa tabia hiyo.
Gazeti hili lilimfuatilia mwanafunzi mwingine
ambaye alijitambulisha kuwa anasoma katika Chuo cha Ustawi wa Jamii,
ambaye kama ilivyokuwa kwa wa kwanza, hakupata taabu kujieleza.
Baada ya mwandishi kueleza alipoipata namba yake mazungumzo yao yalikuwa hivi:
Binti aliuliza: “...Kwa hiyo, uko wapi?”
Mwandishi alijibu: “Nipo Ubungo.”
Binti akauliza tena: “Unaweza kuja Ustawi?”
Binti aliuliza: “...Kwa hiyo, uko wapi?”
Mwandishi alijibu: “Nipo Ubungo.”
Binti akauliza tena: “Unaweza kuja Ustawi?”
Baada ya mawasiliano hayo mwandishi aliambiwa binti huyo kuwa anaweza kumfuata chuoni hapo.
Mwandishi wa gazeti hili alifika maeneo ya
Kijitonyama jirani na kilipo chuo hicho, na kumpigia simu binti huyo,
ambaye aliipokea na safari hii alimwambia mwandishi kuwa ikiwezekana aje
na rafiki yake.
Ilichukua nusu saa kwa wasichana hao kufika katika
baa, ambayo mwandishi alikaa kuwasubiri, mara walitokea wasichana hao
wakiwa wachangamfu, warembo waliovalia mavazi ya kisasa, yaliyoacha
sehemu kubwa ya miili yao wazi.
Muda wa dakika saba walizokaa zilitosha kuwafanya
wazoeane na mwandishi kama vile waliwahi kukutana miaka mingi ya nyuma,
stori, vinywaji na mambo yalifanyika kama ilivyokuwa Udasa.
Mwananchi Jumapili liliendelea na uchunguzi wake
kwa wasichana wengine ambao wameweka picha zao katika mitandao hiyo
wakijiuza, ambapo walipopigiwa simu walijibu na kufika katika maeneo
waliyokubaliana.
Gazeti hili liliwasiliana na wasichana zaidi ya 10 kutoka katika
vyuo tofauti jijini na wote walikiri kuwa wapo katika biashara
wakieleza kuwa mteja akipatikana wanaweza kukubaliana malipo.
Wasichana hao ni tone kati ya mamia ya wanafunzi
wa vyuo, ambao hivi sasa wamebuni njia hiyo baada ya kuona ule mtindo wa
kujiuza nyakati za usiku katika maeneo mbalimbali kuwa umeanza kupitwa
na wakati.
Baadhi ya wasichana wanaofanya biashara hiyo hasa
mkoani Dodoma, wamekuwa wakiwatumia mawakala ambao huwapa namba za simu
na pindi anapotokea mteja, huunganishwa na kiongozi wa kikundi hicho
kabla ya kupata aina ya msichana anayetaka.
Hata hivyo mteja asiporidhika na msichana
aliyeletewa, hutafutiwa mwingine, huku pia wasichana husika
wakitofautiana mahitaji kabla ya kufanya nao ngono.
Wapo wanaoweka masharti ya kunyweshwa pombe
kwanza, kupelekwa disko au kwenye muziki pamoja na wanaokwenda kwa
matakwa ya mteja moja kwa moja.
Wanafunzi wazungumza
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Mwananchi Jumapili baadhi ya wanafunzi walikiri kuwa katika vyuo kuna wasichana wanaojiuza, ingawa walisema kuwa, hawajui kama wamefikia hatua ya kuweka picha katika mitandao na namba za simu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Mwananchi Jumapili baadhi ya wanafunzi walikiri kuwa katika vyuo kuna wasichana wanaojiuza, ingawa walisema kuwa, hawajui kama wamefikia hatua ya kuweka picha katika mitandao na namba za simu.
Mwanafunzi Aisha Idd wa Chuo cha Usimamizi wa
Fedha (IFM), alisema kuwa biashara ya ukahaba inafanyika, lakini
hafahamu kama wanatumia mitandao kujitangaza.
“Sijawahi kufikiria kama wanaweza kufika mbali
kiasi hiki, sijui kama wanajiuza kwenye mitandao, lakini hii inaonyesha
kuwa tunakoelekea ni kubaya zaidi kwani hawa ndio watu wanaotegemewa
katika ujenzi wa taifa,” anasema Aisha na kuongeza:
“Ninafikiri Serikali inapaswa kuliangalia hili,
yaani wasomi ndiyo wanaoongoza kwa kufanya mambo machafu, hii ni aibu
na inaweza kuitia doa sekta nzima ya elimu ionekane haina maana kama
msomi wa chuo kikuu anaweza kufanya upuuzi huu.”
Naye John Mkongo alisema kuwa hashangai kusikia
kuwa wanafunzi hao wametafuta njia nyingine ya kutafutia wateja kwa kuwa
wanaweza kufanya chochote ili wapate pesa za kufanyia starehe.
“Hii inawezekana kabisa kwani hawa dada zetu
wamefikia kufanya mambo ya ajabu kama vile wamepata wazimu, ili kupata
pesa wanaweza kukubali kufanya chochote, najua siku za usoni tutaendelea
kusikia mambo ya ajabu zaidi kwani hawa wenzetu wamejitoa mhanga,”
anasema Mkongo.
Anaongeza kuwa kinachowafanya wasichana hao
kujiingiza katika biashara ya ukahaba ni tamaa, akitoa mfano baadhi ya
wasichana ambao hawajihusishi kabisa na mambo hayo.
“Mimi ninaona kinachowagharimu hawa dada zetu ni tamaa tu, huku
wengine wakiponzwa na ulimbukeni wa kuvamia mambo, ambayo wameanza
kuyaona baada ya kuingia chuoni hasa kupenda vitu vya gharama kama vile
simu, nguo, manukato na magari,”anasema Mkongo.
Wakuu wa vyuo wanena
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Profesa Tolly Mbwete anasema hali hiyo inatokana na kukua kwa utandawazi.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Profesa Tolly Mbwete anasema hali hiyo inatokana na kukua kwa utandawazi.
“Ni wakati sasa kwa wizara inayohusika (Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ) kuhakikisha inafuatilia jambo
hili na kuchukua hatua stahiki,” anasema Profesa Mbwete na kuongeza:
“Elimu nayo inatakiwa kutolewa kwa watumiaji ili kutokuathiri dhamira ya kukua kwa utandawazi, jamii nzima ielimishwe kuhusu matumizi sahihi ya mitandao hiyo.”
“Elimu nayo inatakiwa kutolewa kwa watumiaji ili kutokuathiri dhamira ya kukua kwa utandawazi, jamii nzima ielimishwe kuhusu matumizi sahihi ya mitandao hiyo.”
Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Profesa
Idris Kikula, anasema kuwa hana taarifa za kuwapo kwa makundi hayo
lakini akabainisha kuwa unatakiwa kuwapo kwa utafiti ili kujiridhisha
kama ni kweli hao wanaofanya hivyo ni wanafunzi wa vyuo.
Anasema kama yapo ni wakati sasa wa kuhakikisha
wanakemewa kwani kuna baadhi ya wasichana wanatumia mitandao
kujitambulisha kuwa ni wanafunzi wa vyuo, wakati siyo wanafunzi.
“Hapa Dodoma katika kipindi cha Bunge wanawake
wanaojiuza huwa wengi kila unayemuuliza atakwambia anasoma chuo, lakini
ukimuuliza kozi gani atakwambia bado sijapangiwa hivyo hii ni hatari,”
anasema Profesa Kikula.
Wazazi wasikitika
Mkazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam, Florence Baltazar anasema vitendo hivyo vinatokea kwa sababu ya kuiga mambo ya nchi za nje.
Mkazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam, Florence Baltazar anasema vitendo hivyo vinatokea kwa sababu ya kuiga mambo ya nchi za nje.
Baltazari anasema Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA), inatakiwa kuhakikisha inafuatilia mitandao hiyo ikibidi
kuifunga kabisa.
Zubeda Hamza anasema vijana wa siku hizi hawajitambui hususan wasichana ambao wamekuwa hawapo makini na utu wao.
Zubeda Hamza anasema vijana wa siku hizi hawajitambui hususan wasichana ambao wamekuwa hawapo makini na utu wao.
“Kweli kama msichana anajitambua hawezi kutongozwa
katika mtandao na kukubali haraka au kujinadi hivyo wasichana
wanatakiwa kutambua utu wao,”anasema na kuongeza:
“TCRA inatakiwa kuwa inafanya mapitio ya mitandao yote ili ile inayokiuka taratibu waweze kuifungia.”
Kwa upande wake Charles Mashiri anasema kuwa
wasichana wa siku hizi wamekuwa hawashikiki, hasa wanapofika vyuoni na
kwamba hawataki kukaripiwa au kuonywa.
“Akiwa nyumbani anakuwa mtaratibu lakini akitega
mgongo kutoka kutoka nyumbani anaanza tena ujinga wake, hivyo kama
vitendo hivyo vipo basi Serikali inatakiwa kufuatilia na kuchukua hatua
zaidi,”anasema.
No comments:
Post a Comment