Wachezaji wa Bayern Munich wakichuana na Borrusia Dotmund
FAINALI ya kombe la klabu bingwa
barani Ulaya kwa mara ya kwanza, itahusisha timu mbili kutoka Ujerumani
siku ya Jumamosi, ishara ya ufanisi wa ligi kuu ya Bundesliga ya
kuwekeza katika kukuza vipaji hasa raia wa nchi hiyo.
Maandalizi yote yameshakamilika katika
uwanja wa Wembley, na Kombe la Ligi ya mabingwa wa ulaya linameremeta,
likisubiri nani atakayelinyakua kati ya vilabu viwili vya Ujerumani
vitakavyokutana kwenye fainali. Borussia Dortmund na Bayern Munich ziko
tayari pia.
Mahasimu hao wa Ujerumani wamekuwa wakijiandaa kukutana ugenini Uingereza na mashabiki wamekuja kwa wingi.
Badala ya vilabu vya Uhispania na
Uingereza ambayo vimekuwa vinahodhi soka ya Ulaya, sasa ni vilabu vya
Ujerumani, licha kwamba nchini humo matajiri wakubwa hawaruhusiwi
kumiliki vilabu.
Soka imeimarika Ujerumani?
Raia wengi wa Ujerumani wanasubiri
fainali hiyo kwa hamu na ghamu na Chancellor Angela Markel atakuwepo
katika Uwanja wa Wembley kutizama fainali hiyo.
Ikiwa huu ni mwanzo wa vilabu vya
Ujerumani kutawala soka ya ulaya, haijalishi mashabiki wanashabikia
klabu gani, tayari watakuwa washindi.
Takriban wachezaji wote wa timu ya
taifa ya Ujerumani, watakuwa uwanjani wakati wachezaji wa Klabu ya
Bayern Munich watakapotoana jasho na Borussia Dortmund, katika uwanja wa
Wembley, wengi wa wachezaji hao wakiwa wametoka katika vyuo viwili
vinavyomilikiwa na vilabu hivyo.
Hali hii kwa vilabu vingi vya
uingereza ni kama ndoto. Na ila kufahamu jinsi vilabu hivi viliafikia
ufanisi huu, tutaanza mwaka wa 2000.
Huo ni mwaka ambao Wajerumani
walidhalalishwa katika mashindano ya bara Ulaya, wakati walipomaliza
katika nafasi ya mwisho katika kundi lao hata bila kushinda mechi moja.
Wachezaji wengi wa timu ya Ujerumani
waalikuwa wakonge na magazeti nchini Uholansi yaliandika kuwa ni fahari
yao kuona viwango vya soka vikianguka na kuwa wakati wa Ujerumani
kutawala mchezo huo umemalizika.
Wakati huo huo timu za taifa za
wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 na 19 vile vile vilikuwa na matokeo
mabaya, kwa sababu ya upungufu wa wachezaji wenye vipaji na ukosefu wa
vilabu vya kutosha.
Kutokana na mazingira hayo yote,
mchezo wa soka nchini Ujerumani ulionekana kuelekea kusambaratika zaidi,
hatua iliyolazimisha shirikisho la mchezo wa soka nchini humo, vilabu
na mashabiki kuanzisha mazungumzo ya pamoja, ya kutafuta mbinu ya
kurekebisha hali hiyo.
Kilichofuata na mabadiliko ya kimsingi
ikiwa ni pamoja ya kuwekeza zaidi katika vijana walionekana kuwa na
vipaji na pia katika secta ya kuwahimiza vijana wengi kuanza kucheza
mechi huo.
Mikakati hiyo ilianza kuzaa matunda na
wachezaji wengi wasiozidi umri wa miaka 23, walianza kujumuishwa katika
vikosi mbali mbali vya timu vilivyokuwa vikishiriki katika ligi kuu ya
Bundesliga.
Mwaka wa 2006, timu ya taifa ya
Ujerumani iliyojumuisha vijana wengi chipukizi ilimaliza katika nafasi
ya tatu katika fainali za kombe la dunia na mwaka wa 2010 vile vile
walimaliza katika nafasi hiyo.
Katika fainali hizo mbili za kombe la
dunia, tuzo la mchezaji bora mchanga iliyakuliwa na wachezaji wa
Ujerumani Lukas Podolski mwaka wa 2006 na Thomas Mueller mwaka wa 2010.
Tangu wakati huo vilabu vya Ujerumani
na vimekuwa vikiandikisha matokeo mema, na mbali ya wachezaji wengi
kusajiliwa na vilabu vinavyoshiriki katika ligi ya Bundesliga baadhi yao
pia wamesajiliwa na vilabu vingine katika mataifa ya Ulaya.Chanzo na BBC swahili.
No comments:
Post a Comment