Mwendesha mkuu wa mashtaka nchini Kenya ameauru
kukamatwa kwa mbunge mmoja maarufu nchini humo kwa kuchochea ghasia
dhidi ya watu wa kabila moja.
Ferdinand Waititu, ambaye ni naibu waziri wa
maji alitoa matamshi ya uchochezi dhidi ya watu kutoka jamii ya Maasai
ambao wanaishi katika eneo bunge lake na ambao sana sana hufanya kazi ya
ulinzi.
Vurugu lilianza wakati walinzi hao
waliposhambulia na kumuua kijana mmoja wa kurandaranda mitaani
aliyeshukiwa kwa kitendo cha wizi.
Muda mfupi baada ya bwana Waititu kuwasili
katika eneo hilo na kusema ''
kuanzia leo hatutaki kuwaona watu wa jamii
hiyo ( Wamasaai) katika mtaa huu wa Kayole'' vijana hao wa mitaani
wakajipanga na kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi kufuatia mauaji
ya mmoja wao.
Mmoja wa walinzi hao aliuawa na mwingine kujeruhiwa vibaya.
Hata hivyo mbunge huyo amekana kuwa matamashi
yake yalilenga kuwafukuza wamaasai kutoka eneo bunge lake akisema kuwa
aliwalenga walinzi wa eneo hilo ambao wengi ni watanzania na ambao pia
ni wamasaai.
Aliongeza kuwa matamshi yake ambayo yalirekodiwa hayakukusidiwa. Alisema anakiri kosa lake na hivyo kuomba msamaha.
Wanasiasa wametuhumiwa vikali kwa kuchochea chuki za kikabila huku uchaguzi mkuu ukitarajiwa kufanyika mwezi Machi mwaka ujao.
Zaidi ya watu miamoja wameuwa na maelfu
kujeruhiwa katika makabiliano ya kikabila kati ya Waorma na Wapokomo,
katika eneo la Tana River.
Uhasama wa kikabila ulisababisha vifo vya maelfu
ya watu wakati wa uchaguzi wa mwaka 2007 /2008 kufuatia uchaguzi
uliokumbwa na utata
No comments:
Post a Comment