Ulinzi umedhbitia katika nchi nyingi za
kiisilamu huku zikijiandaa kwa maandamano makubwa hii leo baada ya
maombi ya Ijumaa.
Maandamano hayo yanapinga filamu iliyotengezwa nchini Marekani kumkejeli Mtume Muhammad na dini ya kiisilamu.
Nchini Pakistan, serikali imetenga siku maalum kwa jina "special day of love" kwa miniajili ya kumsifu Mtume Muhammad.
Marekani imelipia matangazo ya kibiashara nchini Pakistan, rais Obama akionekana kukashifu vikali filamu hiyo
Maandamano makubwa kupinga filamu hiyo tayari yamesababisha vifo sehemu mbali mbali duniani.
Ingawa Marekani ndiyo imeathirika zaidi kutokana
na mandamano hayo, uchochezi umeoneka kuongezeka kutoka barani Ulaya
baada ya jarida moja nchini Ufaransa kuchapisha picha za kumfanyia mzaha
Mtume na waisilamu waliopinga vikali filamu hiyo.
Pakistan imetoa wito kwa watu nchini humo kuandamana kwa amani.
Vyama vyote rasmi vya kisiasa pamoja na
mashirika ya kidini wametangaza maandmano kwa ushirikiano na makundi ya
kibiashara huku maandamano hayo yakitarajiwa kuwa makubwa sana.
Waziri wa mambo ya nje nchini humo, Hina Rabbani
Khar, ameambia shirika la habari la AP kwamba siku hiyo maalum inanuiwa
kushinikiza maandamano ya amani na kuzuia watu wenye msimamo mkali
kusababisha ghasia kutokana na hasira yao dhidi ya Marekani.
Duru zinasema kuwa vituo vya mafuta, maduka na masoko yatafungwa leo na huenda usafiri ukasitishwa .
No comments:
Post a Comment