tangazo

Friday, September 14, 2012

NJAMA YA MASHAMBULIZI YASHTUKIWA KENYA


     Magwanda ya mabomu ya kujilipua

Polisi nchini Kenya wamenasa magwanda yenye mabomu ya kujilipua pamoja na zana zengine ambazo zilikuwa zitumike kwa mashambulizi ya kigaidi mjini Nairobi.

Washukiwa wawili wamekamatwa katika msako huo uliofanywa asubihi ya leo katika mtaa wa Eastleigh mjini Nairobi.

Msemaji wa polisi nchini Kenya Eric Kiraithe anasema kuwa maguruneti kumi na mbili pamoja na bunduki aina ya AK 47 pia zilinaswa wakati wa msako uliofanywa na polisi mtaani humo.

"tunaamini kuwa silaha hizi zilinuiwa kutumika kufanya mashambulizi ya kigaidi mjini Nairobi'' alisema bwana Kiraithe.

Silaha hizo zinasemekana kufanana na zile zilizotumika katika mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika nchini Uganda dhidi ya watu waliokuwa wanatazama fainali ya kombe la dunia mwaka 2010, ambapo watu 76 waliuawa.

Kundi la Al-Shabab lilikiri kufanya mashambulizi nchini Uganda, wakisema kuwa wanapinga kuhusika kwake na mapambano dhidi ya kundi hilo nchini Somalia.

Kenya imeshambuliwa karibuni na kundi la al-Shabab baada ya kupeleka vikosi vyake Somalia.

No comments:

Translate