Maafisa nchini Libya wamewakamata washukiwa
kadhaa wa machafuko yaliyosababisha kifo cha balozi wa Marekani nchini
humo pamoja maafisa wengine wanne wa ubalozi huo mjini Benghazi.
Waziri mkuu mpya wa Libya Mustafa Abu Shaqur
aliambia BBC kuwa uchunguzi unaoendelea kuhusiana na kisa hicho
unaonekana kufanikiwa.
Shambulizi lilifanyika siku ya
Jumanne wakati wa maandamano yaliyopinga filamu iliyotengezwa nchini
Marekani kumkejeli Mtume Mohammed.
Maandamano sawa na hayo yamesambaa katika nchi za kiarabu na mataifa ya Kaskazini mwa Afrika.
Maandamano zaidi yanatarajiwa kufanyika baada ya maombi ya Ijumaa
Makabiliano kati ya polisi wa kupambana na
ghasia pamoja na waandamanaji yameendelea usiku kucha katika mji mkuu wa
Misri, Cairo ambako makundi ya wapiganaji wa kiisilamu pamoja na watu
wengine waliitisha maandamano ya amani ya watu milioni moja baadaye leo
Ijumaa.
Hapo jana kulizuka ghasia zaidi nje ya ubalozi
wa Marekani mjini Cairo kati ya polisi na waandamanaji wanaokashifu
filamu ambayo wanasema kuwa inakejeli imani ya Kiislamu.
Runinga ya Misri ilionyesha gari likiteketezwa moto na watu wengine wakikimbia vitoza machozi.
Waandamanaji walitaka kufukuzwa kwa balozi wa
Marekani nchini humo huku polisi wakiwafyatulia mabomu ya kutoa machozi
waandamanaji waliokuwa wakirusha mawe.
Nchini Yemen waandamanaji walivamia ubalozi wa
Marekani wakichoma moto magari kabla ya vikosi vya ulinzi kuwadhibiti
kwa kuwafukuza kutoka eneo hilo.
Maandamano zaidi pia yamefanyika katika nchi za Tunisia, Morocco, Sudan, Mauritania na Iran.
Wakati huohuo maafisa wa Marekani wanasema
serikali ya nchi hiyo inachunguza ikiwa mashambulio ya jumanne kwenye
ubalozi wa Marekani katika mji wa Libya wa Benghazi yalikuwa ni ya
kupangwa au la .
Balozi wa Marekani nchini Libya , Christopher Stevens, aliuawa .
Maafisa wa Marekani wameelezea mashambulio hayo
kama yenye utata na yenye kupangwa kitaalamu na kuna tetesi kwamba
makundi ya jihad huenda yalihusika .
Awali ilifikiriwa kuwa mashambulio hayo yalikuwa
na uhusiano na maandamano ya kupinga filamu iliyokuwa inamkejeli Mtume
Mohammed.
Takriban waandamanaji mia mbili wamekusanyika
karibu na ubalozi wa Marekani mjini Cairo Misri kwa usiku wa pili
kuelezea hasira yao juu ya filamu hiyo .
Awali waandamanaji walirusha mawe kwenye ubalozi huo na vikosi vya usalama vikafyatua mabomu ya kutoa machozi kuwa tawanya.
Watu wenye silaha waliokuwa na maguruneti
walichomo moto jengo la ubalozi na walioshuhudia wanasema watu hao
walizingira eneo hilo.
Rais Obama amelaani vikali shambulio hilo na ameahidi kushirikiana na serikali ya Libya kuwafikisha mbele ya sheria wahusika
No comments:
Post a Comment