Baraza la umoja wa mataifa limefungua rasmi mkutano wake mjini New York.
Rais Barack Obama amefungua mkutano huo kwa
hotuba ya kumsifu balozi wa zamani wa Libya ambaye aliuawa katika
shambulizi dhidi ya ubalozi wa Marekani mjini Benghazi mapema mwezi huu.
Alisema kuwa Marekani haitachoka katika juhudi zake kuwasaka wauaji wa balozi huyo na kuwawajibisha kisheria.
Alilaani ghasia hizo zilizotokea kufuatia
ghadhabu katika nchi za kiisilamu baada ya kutolewa kwa filamu
iliyokejeli Mtume Muhammad na dini ya kiisilamu.
Obama amelaani filamu hiyo na kusema Marekani
haina uhusiano wowote na filamu hiyo na vile vile amelaani waliotengeza
filamu hiyo.
Rais Obama ameitaka serikali ya rais wa Syria
Bashar Assad kuondoka mamlakani na kuwa Marekani itafanya kila iwezalo
kuzuia Iran kuwa na zana za nuklia.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, naye katibu mkuu
wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon, alikitaja kipindi hiki kama kipindi
cha msukosuko ,mpito na mageuzi.
Alionya kuwa fursa inaweza kuwa inatoweka ya kupata suluhu baina ya Israil na Wapalestina, ya kuwa na mataifa mawili.
No comments:
Post a Comment