Rais wa Marekani Barack Obama, amewaomba wamarekani kumpa fursa nyingine kuiongoza nchi hiyo.
Ombi lake amelitoa katika kilele cha kongamano la chama cha Democratic mjini North Carolina.
Akijiwasilisha kama mgombea wa urais
mwenye kuleta matumaini kwa wamarekani, Rais Obama alisema kuwa
uchaguzi utakaofanyika mwezi Novemba, utatoa fursa kwa wapiga kura
kuchagua kati ya maono mawili tofauti kuhusu hatma ya Marekani.
Aliwataka Wamarekani kuwa wavumilivu akisema
kuwa matatizo yanayokabili Marekani yamekuwa yakiongezeka kwa miaka
mingi na kuwa itachukua muda kuweza kuyatatua.
Lakini aliongeza kuwa ikiwa watamchagua tena,
ataweza kubuni nafasi mpya za kazi, kupunguza madeni na kuimarisha
uchumi wa Marekani.
Rais Obama alisema anajiona kama kiongozi
aliyekuwa amewekwa kwa mizani kujaribiwa uongozi wake na kuwa amefaulu.
Alisema mpinzani wake wa Republican, Mitt Romney, hayuko tayari kwa
mashauriano ya kidiplomasia.
Alitofautisha malengo yake na yale ya chama
pinzani na kurejelea kauli mbiu yake ya mwaka 2008 , kuwataka watu kuwa
na matumaini.
"sikuwahi kusema kuwa safari hii itakuwa rahisi na sitatoa ahadi hiyo hii leo'' Obama aliambia kongamano la wajumbe wa Democrat.
Mitt Romney wa chama cha Republican atapambana
na Rais Obama kuwania urais huku kura za maoni zikionyesha wawili hao
wakikaribiana.
No comments:
Post a Comment