Polisi nchini Afrika Kusini wametumia risasi za
mipira na gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji waliokuwa
wanagoma karibu na mgodi mmoja unaomilikiwa na kampuni ya Anglo
American.
Makabiliano hayo yametokea siku moja baada ya
mkataba kuafikiwa kati ya wachimba migodi wa Marikana na wamiliki wa
kampuni ya Lonmin.
"hatutaruhusu mikutano yoyote haramu kufanyika'' alisema msemaji mmoja wa polisi.
Wafanyakazi wa kampuni ya Lonmin walisitisha
mgomo wao wa wiki sita siku ya Jumanne baada ya kukubali nyongeza ya
asilimia 22 ya mishahara.
Migomo hiyo ilisambaa hadi katika migodi mingine
nchini humo. Afrika Kusini ni mojawapo ya nchi zinazozalisha madini
mengi duniani.
Mnamo siku ya Jumatatu rais Jacob Zuma alisema
kuwa migomo katika sekta ya madini ililetea nchi hiyo hasara ya zaidi ya
dola nusu milioni.
Migomo ilianza nchini humo baada ya kampuni ya
madini ya Anglo American Platinum (amplats),kampuni kubwa zaidi ya
madini ya Platinum duniani kufungua kiwanda chake baada ya kufungwa wiki
jana kufuatia migomo hiyo.
Msemaji wa kampuni ya Amplats, Mpumi Sithole
alisema kuwa migodi ya Rustenburg,ambacho ni kitovu cha uchimbaji migodi
nchini humo, Kaskazini Mashariki mwa Johannesburg uliendelea na kazi
kama kawaida.
No comments:
Post a Comment