Mawakili wa mwanamfalme wa Uingereza William na mkewe
Kate Middleton, wanatarajiwa kuwasilisha kesi katika mahakama moja
mjini Paris kubana kuchapishwa tena kwa picha za Kate akiwa nusu uchi.
Wanandoa hao wanataka mahakama kuzuia mauzo ya nakala za jarida la udaku la Closer, ambalo ndilo lilichapisha picha hizo mwanzo.
Picha hizo sasa zimechapishwa na
baadhi ya mitandao ya kigeni huku jarida lengine nchini Ireland la Daily
Star nalo pia likizichapisha.
Mawakili hao pia wanataka viongozi wa mashtaka
nchini Ufaransa kumfungulia mashtaka ya jinai mpiga picha aliyempiga
picha Kate akiwa katika likizo ya faragha na mumewe William.
Mwandishi wa BBC mjini Paris , Christian Fraser,
anasema kuwa mawakili wengi wanasema kuwa kulingana na sheria kali
kuhusu mambo ya faragha nchini Ufaransa, picha hizo zinaonyesha wazi
kuwa maisha ya faragha ya Kate yaliingiliwa.
Ikiwa amri ya kisheria itatolewa na mahakama,
nakala za jarida hilo zitaondolewa madukani mara moja ingawa hukumu ya
mahakama maalum itahusu tu picha hizo nchini Ufaransa.
Hata hivyo hatua hiyo haijazuia kampuni ya
Closer nchini Italia yenye kuchapisha jarida liitwalo Chi, kuzuia
uchapishaji wa nakala zenye picha ya Kate akiwa nusu uchi.
No comments:
Post a Comment