Msanii moja toka Uingereza amekamatwa nchini Uganda kwa madia ya kuandaa na kuonyesha mchezo wa kuigiza kuhusu ushuga.
Polisi wanasema kuwa Muingereza huyo
alionyesha mchezo huo wa kuigiza licha ya kwamba Uganda ilipiga
marufuku kwa muda onyesho hilo.
Mtayarishi David Cecil wa Uingereza alifikishwa
katika mahakama moja mjini Kampala na kushitakiwa kwa madia ya kukaidi
na kupuuza amri ya serikali.
Mahakama hiyo iliambiwa kuwa Bwana Cecil
alionyesha mchezo huo kwa jina "The river and the mountain" katika
ukumbi wa Tilapia Cultural Center taraehe 17 Agosti na pia katika ukumbi
mwengine wa Mish Mash Cultural Center tarehe 26 Agosti mjini Kampala.
Mahakama hiyo ya Kampala ilikataa kuamuachilia
Muingereza huyo kwa dhamana na badala yake kuagiza awekwe katika gereza
la Luzira hadi siku ya jumatatu ,Septemba 17 ambapo kesi yake
inatarajiwa kuendelea.
No comments:
Post a Comment