Hivi karibuni ilikuwa almanusura La
Liga isianze Msimu mpya baada ya baadhi ya Klabu kuja juu zikitaka
mfumo wa Mapato yanayotokana na matangazo ya Mechi laivu kwenye TV
urekebishwe ili kila Klabu ifaidike ipasavywo kama vile ilivyo huko
England kwenye Ligi Kuu England, BPL [Barclays Premier League].
Huko England, kwenye Ligi Kuu,
makubaliano ya sasa ya maonyesho ya Mechi laivu kwenye TV ni yale
yaliyoanza tangu Mwaka 2010 na yatamalizika 2013 ambayo yatamwaga Pauni
Bilioni 3.5 kwa kipindi hicho, ikiwa ni Pauni Bilioni 1.17 kwa Mwaka.
Mapato hayo hukatwa Fedha za matumizi
kuendesha Ligi, fungu jingine hugawiwa Vyama tanzu kama vile PFA, Chama
cha Wachezaji wa Kulipwa, LMA, Chama cha Mameneja wa Timu za Ligi,
Vyama vinavyoendesha Ligi za Madaraja ya chini, kama vile Conference na
Football League, Chama cha Marefa na pia kwenye Vyama vinavyotoa
misaada kwa Jamii.
Lakini fungu kubwa la Mapato hayo ya TV
huambuliwa na kugawiwa kwa Klabu 20 zilizomo kwenye Ligi Kuu England na
pia Klabu ambazo zimeporomoka toka Ligi Kuu katika kipindi hicho cha
Mkataba.
Mwishoni mwa Msimu wa 2011/12, Mgao ulikuwa ni jumla ya Pauni Bilioni 1.055.
Kati ya hizo, Pauni Milioni 968.2
ziligawanywa kwa Klabu 20 za Ligi Kuu za Msimu huo na zilizobaki
zilipewa Klabu 7 zilizoporomoka kutoka Ligi Kuu.
MGAWANYO HUWA:
-Mapato yote yanayotoka nje ya England hugawanywa sawa sawa kwa kila Klabu na mgao huo ulikuwa £18,764,644 kwa kila Klabu.
-Mapato yanayozalishwa ndani ya England hugawanywa ifuatavyo:
=Asilimia 50 yake hugawanywa sawa kwa kila Klabu
=Asilimia 25 yake hugawanywa kwa kutegemea Klabu ilirushwa mara ngapi laivu
=Asilimia 25 hutegemea Klabu ilimaliza nafasi ipi kwenye Msimamo wa Ligi mwishoni
Ukiangalia ule Mgao wa Asilimia 25
inayotegemea nafasi ya Klabu utakuta Wolves, waliomaliza Ligi wakiwa
mkiani ambayo ni nafasi ya 20, walipewa £755,062, Blackburn, waliokuwa
nafasi ya 19, walipata mara mbili zaidi ya hizo na Bolton walipata mara
3 zaidi ya hizo kwa kumaliza nafasi ya 18 huku Timu iliyomaliza nafasi
ya Kwanza, Manchester City, wakizoa mara 20 zaidi ya hizo, yaani
£15,101,240.
Ukichukua Mapato ya Klabu ya Kwanza,
Manchester City, utakuta walizoa Jumla ya £60,602,289 na Wolves,
waliomaliza mwisho, walipata £39,084,461.
Kitaalam, utaona Man City walipata Mgao mara 1.55 zaidi ya Wolves.
Huko Spain, kwenye La Liga, Real Madrid
na Barcelona, huwa wanafanya Dili zao wenyewe na hawagawani na Klabu
nyingine na wao hupata mara 14 zaidi ya Klabu nyingine.
Italy, kwenye Serie A, tofaitu ni mara
10 zaidi,.Ufaransa kwenye Ligi 1 ni mara 3 na nusu na Germany, kwenye
Bundesliga, ni mara mbili.
No comments:
Post a Comment