Kiongozi wa kundi la Hezbollah nchini Lebanon,
amesema kuwa marekani ni sharti ikubali lawama kuhusiana na filamu
iliyotayarishwa nchini humo ambayo inaidhalilisha dini ya kiislamu na
kusababisha ghadabu katika mataifa mengi ya kiislamu.
Kiongozi wa Hezbollah, Sheikh Hassan Nasrallah,
alitoa wito kufanyika kwa maandamano ya wiki nzima, sio tu katika balozi
za Marekani bali pia kuzishinikiza serikali za kiislamu kuelezea
ghadhabu dhidi ya Marekani.
Huku maandamano ya kuipinga Marekani yakiendelea
kuhusiana na filamu hiyo katika mataifa kadhaa, mtu mmoja aliuwawa
katika makabiliano na maafisa wa usalama nje ya ubalozi mdogo wa
Marekani katika mji wa Karachi, Pakistan.
Maandamano katika balozi nyingi za Marekani
yamekuwa yakiendelea kuhusu filamu hiyo iliyotengezwa nchini Marekani na
kumdhihaki Mtume Muhammad.
Katika hotuba yake iliyopeperushwa kupitia kituo
cha televisheni cha kundi hilo, Al-Manar, Sheikh Nasrallah alitoa wito
wa kufanyika maandamano zaidi.
Maandamano ya kwanza yatafanyika hii leo Kusini mwa Beirut eneo ambalo ni ngome kubwa ya Hezbollah.
Sheikh Nasrallah aliitaja filamu hiyo kama
hatari sana na kusema ni matusi makubwa kuwahi kutolewa dhidi ya
uisilamu.
Alisema ni matusi makubwa hata kuliko kitabu kilichoandikwa na
Salman Rushdie (Satanic Verses) kikimkejeli Mtume Muhammad na ambacho
kilichapishwa na gazeti moja nchini Denmark mwaka 2005.
No comments:
Post a Comment