Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa, Ban Ki
Moon ameandaa mkutano maalum mjini New York kujadili mzozo unaokumba
Mali ambako wapiganaji wa kiisilamu wameteka eneo la Kaskazini mwa nchi
hiyo.
Nchi kadhaa za Afrika Magharibi pamoja na
Ufaransa zinataka azimio la Baraza la usalama la umoja wa mataifa,
litakalo wawezesha kuunga mkono hatua za kijeshi dhidi ya kile
wanachokiita magaidi wa Kaskazini mwa Mali.
Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, aliambia
mkutano wa baraza kuu la umoja wa mataifa, Jumanne, kuwa Ufaransa iko
tayari kuunga mkono juhudi za kuirejeshea Mali hadhi yake kama nchi
huru.
Jeshi la pamoja la nchi za Magharibi mwa Afrika
lijulikanalo kama ECOMOG, na ambalo limewahi kuingilia kati mizozo
katika baadhi ya nchi za Afrika,
linasema kuwa takriban wanajeshi elfu
tatu, wana kibarua cha kutwaa eneo la Kaskazini kutoka kwa wapiganaji
hao.
Lakini mwandishi wa BBC anasema kuwa viongozi wa
Afrika wanatafuta uungwaji mkono kutoka kwa Baraza la usalama la umoja
wa mataifa kabla ya kupeleka wanajeshi huko.
No comments:
Post a Comment