Stafu Sajenti Yohana Mjema na Afande
Tunu wa kikosi cha Trafiki wakikagua moja ya magari yaliyokaguliwa na
kupatiwa Stika maalum za ukaguzi leo mjini Iringa, wakati wa zoezi la
ukaguzi katika kuadhimisha wiki ya Nenda wa usalama Barabarani, ukaguzi
huo umefanyika katika eneo la Ipogolo katika barabara kuu ya Dar es
salaam- Tunduma.
Koplo Isack Mkaguzi wa magari katika
jeshi la polisi Trafiki akimhoji mmoja wa madereva wa magari makubwa
wakati alipokuwa akikagua gari aina hili lililokuwa likitokea nchini
Congo DRC ambako lilipeleka mafuta, kulia ni Tunu akishiriki katika
zoezi la ukaguzi wa magari, kikosi cha Trafiki kinaendesha zoezi la
ukaguzi wa magari yote na kuyapa stika maalum zinazonyesha kuwa
yamekaguliwa katika kuadhimisha wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani
ambapo mwaka hu kauli mbiu ya mwaka huu ni “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”
Ukaguzi huo umefanyika katika eneo la
Ipogolo mjini Iringa kwenye barabara kuu ya Dar es salaam -Tunduma
ambako maadhimisha hayo yanafanyika kitaifa.
Koplo Isack Mkaguzi wa magari katika
jeshi la polisi Trafiki akumuandikia Stika mmoja wa madereva wa Daladala
mkoani Iringa mara baada ya kukagua gari hilo.
Stafu Sajenti Yohana Mjema akilikagua
Roli lenye namba T 456 ADQ lililokuwa limebeba matofali katika zoezi la
ukaguzi wa magari kuadhimisha wiki ya nenda kwa usalama Barabarani,
kulia ni Afande Tunu akishiriki katika zoezi hilo.
Mabasi yaliyokuwa yakitokea mkoani
Iringa yakipita mbele ya maafisa wa usalama barabarani wakati wa ukaguzi
wa magari katika wiki ya Nenda kwa usalama Mkoani Iringa.
Koplo Isack na Afande Tunu
wakizikagua pikipiki zilizokuwa zikipita katika eneo la Ipogolo mjini
Iringa katika barabara ya Dar es salaam Tunduma wakati wa ukaguzi wa
magari leo.
No comments:
Post a Comment