Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,akifuatana na Makamo wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China
Hui Liangyu baada mazungumzo yao alipofika Ikulu Mjini Zanzibar
jana,akiwa katika ziara ya siku mbili. [Picha na Ramadhan Othman,
Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,akisalimiana na Makamo wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China
Hui Liangyu alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa katika ziara ya siku
mbili ,Makamo Waziri Mkuu Liangyu akiwa na ujumbe wake walifanya
mazungumzo na Rais [Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.]
Othman,Ikulu.]
NA Rajab Mkasaba , Ikulu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein leo amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Hui Liangyu huku China ikiahidi kuendelea
kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta za maendeleo.
Katika mazungumzo hayo viongozi hao walieleza ni kwa namna gani nchi
mbili hizo zimeweza kukuza na kuimarisha uhusiano huo wa muda mrefu
ambao umeweza kuleta manufaa zaidi.
Aidha, Dk. Shein alimueleza Naibu Waziri Mkuu huyo kuwa Zanzibar
inajivunia uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya Zanzibar
na China ambao ulianzishwa na viongozi waasisi akiwemo Hayati Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume na
Mwenyekiti Mao Tse Dung.
No comments:
Post a Comment