Penati ya Dakika ya 94 ya Neymar
imeipa ushindi Brazil wa bao 2-1 leo Alfajiri katika Mechi ya kwanza ya
SUPERCLASICO DE LAS AMERICAS iliyochezwa huko Goias, Brazil.
Brazil na Argentina,
zikichezesha Wachezaji wale tu wanaocheza Soka lao kwenye Vilabu
vilivyopo huko Marekani ya Kusini, zitarudiana hapo Oktoba 3 huko
Resistencia, Argentina.
Katika Mechi hii,
Argentina ndio waliotangulia kupata bao katika Dakika ya 20 kupitia Juan
Manuel Martinez ambae alicheza vizuri pasi za moja mbili na Clemente
Rodriguez.
Brazil walisawazisha Dakika 6 baadae baada ya mchezo safi wa Neymar kumfungulia Paulinho aliefunga.
Huku ngoma ikiwa inamalizika kwa sare ya 1-1, Mchezaji wa Argentina aliunawa mpira ndani ya boksi na Neymar kufunga Penati hiyo.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
VIKOSI:
ARGENTINA:
Oscar Ustari (Boca
Juniors), Marcelo Barovero (River Plate), Esteban Andrada (Lanus), Gino
Peruzzi (Velez Sarsfield), Maximiliano Caire (Colon de Santa Fe),
Lisandro Lepez (Arsenal), Sebastian Dominguez (Velez Sarsfield), Leandro
Desabato (Estudiantes de La Plata), Vergini Santiago (Newell's Old
Boys), German Re (Estudiantes de La Plata), Clemente Rodriguez (Boca
Juniors), Leonel Vangioni (Newell's Old Boys), Rodrigo Brana
(Estudiantes de La Plata), Leandro Somoza (Boca Juniors), Leonardo
Ponzio (River Plate), Mino Sanchez Juan (Boca Juniors), Maximiliano
Rodriguez (Newell's Old Boys), Julio Buffarini (San Lorenzo), Ricardo
Centurion (Racing Club), Cristian Chavez (Boca Juniors), Lucas Viatri
(Boca Juniors), Rogelio Funes Mori (River Plate), Lucas Mugni (Colon de
Santa Fe).
BRAZIL:
Cassio (Corinthians),
Jefferson (Botafogo), Carlinhos (Fluminense), Marcos Rocha (Atletico
Mineiro), Fabio Santos (Corinthians), Lucas Marques (Botafogo), Dede
(Vasco), Rhodolfo (Sao Paulo), Rever (Atletico Mineiro), Arouca
(Santos), Bernard (Atletico Mineiro), Fernando (Gremio), Jadson (Sao
Paulo), Lucas (Sao Paulo), Paulinho (Corinthians), Ralf (Corinthians),
Thiago Neves (Fluminense), Leandro Damiao (Internacional), Luis Fabiano
(Sao Paulo), Neymar (Santos), Wellington Nem (Fluminense).
No comments:
Post a Comment