Kajala
Masanja (pichani kushoto) na kulia akitoka
mahakamani
SHAHIDI
wa nne Monika Timber (41), amedai mahakamani katika kesi ya kula njama,
kuhamisha umiliki wa nyumba na utakatishaji wa fedha inayomkabili msanii wa
filamu nchini Kajala Masanja na mume wake Faraja Chambo kuwa nyumba hiyo ya
washtakiwa iliuzwa wakati zuio lililotolewa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (Takukuru) bado muda wake haujamalizika.
Kadhalika,
shahidi huyo ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kunduchi Salasala,
amedai kuwa Takukuru walitoa zuio la nyumba hiyo kufanyiwa chochote ikiwamo
kuuzwa hadi uchunguzi wa kesi ya utakatishaji fedha haramu inayomkabili
mshtakiwa Chambo utakapomalizika.
Timber
alitoa ushahidi wake leo mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo anayesikiliza kesi
hiyo.
Akiongozwa
na Mwendesha Mashtaka Takukuru, Leonard Swai shahidi huyo alidai kuwa taasisi
hiyo ilitoa zuio la kwanza Julai 15, mwaka 2009 ikimtaka mmiliki kutofanya kitu
chochote ndani ya miezi 6 kwa kuwa inafanyiwa uchunguzi.
Alidai
kuwa baada ya muda wa zuio lile kumalizika, Takukuru waliwasilisha zuio la pili
Februari 18, mwaka 2010 lakini kabla muda wake kumalizika nyumba
iliuzwa.
"Nyumba
ile ilipouzwa ofisi yangu haikuhusishwa na muuzaji wala mnunuaji ...nilihojiwa
na Takukuru baada ya ile nyumba kuuzwa nikawaeleza sikuwa na taarifa kwa sababu
zuio bado lilikuwa halijamalizika muda wake," alidai Timber.
Katika
kesi hiyo, Kajala na Chambo, wanakabiliwa na shtaka la kula njama ya kuhamisha
umiliki wa nyumba iliyoko Kunduchi Salasala jijini Dar es Salaam kinyume na
kifungu cha 34 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007 wakijua
ni kosa kwani tayari Mwanasheria Mkuu wa serikali alishazuia kuuzwa kwa nyumba
hiyo.
Shtaka la
pili, ilidaiwa kuwa Aprili 14, mwaka 2010 washtakiwa hao walihamisha isivyo
halali umiliki wa nyumba hiyo kwenda kwa Emiliana Rwegarura huku wakijua
imepatikana kwa njia ya rushwa kinyume na kifungu cha 34(2)A(3) cha Sheria ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007.
Katika
shtaka la tatu ilidaiwa kuwa siku na mahali hapo washitakiwa hao walitakatisha
fedha huku wakijiua ni kinyume na sheria hiyo.
Washtakiwa
walikana mashtaka yote kwa nyakati tofauti kutokana na mashtaka yanayowakabili
kutokuwa na dhamana kisheria. Washtakiwa wako mahabusu mpaka kesi itakapotolewa
uamuzi.
No comments:
Post a Comment