Dar es Salaam . Jeshi la Polisi Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya, linawashikiliwa watu wawili, wanaodaiwa kuwa ni mtu na mpenzi wake kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroin kilo mbili zinazokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi Sh90 milioni.
Mkuu wa kitengo hicho, Godfrey Nzowa aliliambia gazeti hili jana kuwa watuhumiwa hao ambao mmoja ni mwanamke walikamatwa juzi saa 8 mchana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Alisema watuhumiwa walikuwa wakisafiri kwenda Mji wa Bangkok Thailand kupitia Addis Ababa, Ethiopia ambapo walikata tiketi ya ndege la shirika hilo.
“Walipoanza kufanya ukaguzi watuhumiwa hawa walijichomeka katikati ya wenzao ndipo tulipowanasa na dawa hizo ambazo walizificha kwenye mabegi yao katikati ya nguo,” alisema Nzowa.
Alisema kuwa watuhumiwa hao waligawana dawa hizo kwani walipofanyiwa upekuzi na polisi walikutwa kila mtu akiwa na kilo moja.
No comments:
Post a Comment