tangazo
Monday, August 20, 2012
ALEX SONG COMPLETE HIS MOVE TO BARCALONA
Alex Song poses for the photographers after arriving at the Nou Camp on Monday
Alex Song has touched down in Barcelona to complete his £15million move after it emerged that Arsenal are happy to let him go.
Arsene Wenger sanctioned the sale of after becoming infuriated by the midfielder’s lack of commitment in pre-season.
And it has emerged that the Cameroon midfielder’s exit has been in the offing for months after a breakdown in the relationship between player and club over an improved contract.
As Sportsmail revealed last Thursday, Song will complete a switch on Monday — sealing the departure of a second key Arsenal player in less than a week.
But unlike the £24million sale of Robin van Persie, who was in the final year of his contract, to Manchester United, the Gunners were under no pressure to offload Song, who had three seasons left on his £55,000-per-week deal.
Club sources claim Song’s levels of professionalism had dropped significantly in recent months and Wenger decided enough was enough earlier this summer.
HII NI MAHUSUSI KWA IRENE UWOYA NA WEMA SEPETU.
ZARINAH Zaitun Hassan ‘Zari’ ni mwanamuziki, mtangazaji na mfanyabiashara mrembo wa Uganda mwenye umri wa miaka 30, akiwa ni mama wa watoto wawili, aliyeolewa na Ivan Semwanga, utambulisho unatosha.
Katika makala hii, Zari ni mfano mzuri wa kuigwa na mastaa wetu wakiwemo waigizaji wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Masawe na Wema Isaac Sepetu kwani ni wa levo yake kiustaa.
Zari anatajwa kuwa ndiye mwanadada mzuri na mwenye mvuto zaidi Afrika Mashariki ambaye pia anashika namba moja kwa wanawake matajiri wa Uganda, akiongoza kwa kuingiza mshiko mrefu, kumiliki majumba na magari ya kifahari kama yale ya mastaa wa Kimarekani.
Zari amepata mafanikio makubwa katika muziki na kipindi chake cha The Boss Lady kwenye Runinga ya UBC nchini humo, kinachomuingizia mkwanja mrefu kutokana na matangazo kikifananishwa na kile cha mwanamitindo wa Marekani, Kim Kardashian cha Keep Up With The Kardashians.
Kwa mujibu wa Jarida la Times la Uganda, huenda Zari akaingia kwenye orodha ya wanawake matajiri zaidi Afrika siku chache zijazo endapo ataendelea kuzichanga.
Zari mwenye maskani yake Kampala na Afrika Kusini, anamiliki ndinga kibao za kisasa na zenye thamani kubwa kama BMW (2006) lenye thamani ya dola 47,000 (Sh. milioni 75.2), Black Chrysler (2008) linalouzwa dola 16,000 (Sh. milioni 25.6) na Audi Q7 (2010) linalogharimu dola 53,000 (Sh. milioni 84.8).
Mengine ni Silver Chrysler (2008) lenye thamani ya dola 13,000 (Sh. milioni 20.8), Jetta Volkswagen (2006) linalogharimu dola 27,000 (Sh. milioni 43.2), Mercedes Benz Convertible (2008) linalouzwa dola 26,000 (Sh. milioni 41.6), Range Rover Sport (2010) lenye thamani ya dola 109,000 (Sh. milioni 174.4),
Lamborghini Gallardo (2010) linalogharimu dola 198,000 (Sh. milioni 316.8), Hummer H2 la dola 150,000 (Sh. milioni 240) na mengine mengi, yote yakiwa na jina lake badala ya namba za usajili.
Pia bidada huyo anamiliki maduka, hoteli na majumba ya kisasa kwenye miji mikubwa ya Pretoria na Cape Town nchini Afrika Kusini na Kampala, Uganda.
Lengo langu ni kutoa changamoto kwa mastaa wetu wanaotembelea magari ya kuazima, kukodisha au kuhongwa. Ipo mifano kibwena ya mastaa wa Kibongo wanaoishi kwa mizinga, kuhongwahongwa, ukuwadi lakini wenye mbwembwe na makeke mjini kumbe hawana lolote. Tujifunze kutoka kwa Zari!
Friday, August 17, 2012
ALIYEKUTWA KACHOMWA MOTO NDANI YA GARI AZIKWA.
Ibada ya kuuombea mwili wa marehemu Rehema
Kaburi la marehemu Rehema Nungu
MWANAMKE aliyeteketezwa ndani ya gari lenye usajili namba T883 BLA aina ya Toyota Corolla katika msitu wa Mabwepande, majivu ya mwili wake yalizikwa Agosti 15 mwaka huu katika makaburi ya Kondo, Tegeta Chanika jijini Dar es Salaam.
Mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la Rehema Nungu aliteketezwa akiwa ndani ya gari na watu wasiofahamika.
Akitoa wasifu wa marehemu Rehema, katika mazishi hayo yaliyofanyika nyumbani kwa mumewe, Simon Sakilu, shemeji wa marehemu Vicent Lissu alisema mwenye taarifa zaidi za kifo hicho azipeleke jeshi la polisi mkoa wa Pwani. Alitoa kauli hiyo kutokana na kifo cha Rehema kugubikwa na utata mzito na mkanganyiko wa hali ya juu na kwamba kwa kufanya hivyo itasaidia kupatikana kwa taarifa sahihi juu ya sakata hilo.
Lissu alisema siku ya mwisho marehemu alipatwa na msongo wa mawazo na alikuwa hazungumzi na mtu yeyote kwani ilifikia hatua ya kuzima simu yake ya mkononi.
Kaburi la marehemu Rehema Nungu
MWANAMKE aliyeteketezwa ndani ya gari lenye usajili namba T883 BLA aina ya Toyota Corolla katika msitu wa Mabwepande, majivu ya mwili wake yalizikwa Agosti 15 mwaka huu katika makaburi ya Kondo, Tegeta Chanika jijini Dar es Salaam.
Mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la Rehema Nungu aliteketezwa akiwa ndani ya gari na watu wasiofahamika.
Akitoa wasifu wa marehemu Rehema, katika mazishi hayo yaliyofanyika nyumbani kwa mumewe, Simon Sakilu, shemeji wa marehemu Vicent Lissu alisema mwenye taarifa zaidi za kifo hicho azipeleke jeshi la polisi mkoa wa Pwani. Alitoa kauli hiyo kutokana na kifo cha Rehema kugubikwa na utata mzito na mkanganyiko wa hali ya juu na kwamba kwa kufanya hivyo itasaidia kupatikana kwa taarifa sahihi juu ya sakata hilo.
Lissu alisema siku ya mwisho marehemu alipatwa na msongo wa mawazo na alikuwa hazungumzi na mtu yeyote kwani ilifikia hatua ya kuzima simu yake ya mkononi.
JOHN BOCCO AONGEZEWA SIKU 6 ZA MAJARIBIO
John Bocco.
Baada ya majaribio ya siku 7 Super Sport United imewapunguza wachezaji sita kati ya 9 waliokuwa wakifanya majaribio, waliopunguzwa wanatoka Congo, Senegal, Nigeria na Mali. Wachezaji waliobaki ni JB19 toka Tanzania, Mnigeria ambaye alikuwa Petro Athletico ya Angola na Raia wa Chad. Nafasi ni moja tuu. Bocco ameongezewa siku sita nyingine za majaribio hadi Alhamisi Ijayo....All The Best JB19.
Baada ya majaribio ya siku 7 Super Sport United imewapunguza wachezaji sita kati ya 9 waliokuwa wakifanya majaribio, waliopunguzwa wanatoka Congo, Senegal, Nigeria na Mali. Wachezaji waliobaki ni JB19 toka Tanzania, Mnigeria ambaye alikuwa Petro Athletico ya Angola na Raia wa Chad. Nafasi ni moja tuu. Bocco ameongezewa siku sita nyingine za majaribio hadi Alhamisi Ijayo....All The Best JB19.
Yondan, Chombo wasubiri rungu la kamati
KAMATI ya Sheria, Maadili na Hadhi ya Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imesema itasimama kwenye mstari ulionyoka kutoa uamuzi kwa wachezaji wataonekana katika orodha ya usajili zaidi ya timu moja.
Akizungumza na Mwananchi jana, mwenyekiti wa kamati hiyo, Alex Mgongolwa alisema hakutakuwa na upendeleo katika kutoa uamuzi wa utata wa wachezaji.
Mgongolwa alisema, kamati yake inatambua hali halisi ya zoezi zima la usajili kwa klabu za Ligi Kuu na Daraja la Kwanza, hivyo watakuwa makini.
"Nia yetu siyo kuendeleza matatizo, tunachotaka kwa sasa ni kumaliza utata wa usajili kwa haki, na tutafanya hivyo bila upendeleo," alisema uliopo Mgongolwa.
Kuhusu madai kutoka kwa baadhi ya watu kuituhumu kamati yake kutoa umauzi wa upendeleo hasa kwa klabu ya Yanga, alisema: "Hapa tunafuata kanuni, suala la upendeleo hakuna. Hapa hakuna Simba wala Yanga."
"Tutaangalia kanuni zinasemaje kama mchezaji amesaini zaidi ya timu moja, tutangalia pia mazingira yaliyotumika, hatutaibeba klabu yoyote katika hili, wengi wamekuwa wakisema Yanga imekuwa ikipendelewa siyo," alisema.
Kauli ya Mgongolwa imekuja siku chache kupita tangu Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Aden Rage, ambaye pia alikuwa mjumbe kwenye kamati Mgongolwa, kutangaza kujiuzulu.
Katika madai yake, Rage aliseme amefikia uamuzi huo baada ya kubaini kuwa, kamati hiyo imekosa uaminifu kwa vile imekuwa ikitoa uamuzi kwa upendeleo na kwamba siku zote imekuwa ikiikandamiza klabu yake.
Tayari suala mgongano wa usajili wa klabu tatu kubwa, Simba, Yanga na Azam limeshaonekana kufuatia majina ya wachezaji watatu kuonekana kwenye orodha ya timu hizo.
Beki Kelvin Yondan aliyesajiliwa na Yanga kutoka Simba, jina lake liko kwenye orodha ya timu zote mbili zilizowasilishwa Jumatano wiki hii.
Vilevile, jina la mchezaji Ramadhan Chombo, ambaye Simba wanadai kumsajili kutoka Azam FC, limo kwenye orodha ya Wekundu hao wa Msimbazi kama ilivyo kwa Azam.
Wakati huohuo, timu zote zitakazoshiriki Ligi Kuu msimu wa 2012\2013, zimewakilisha usajili wao mpaka kufikia jana asubuhi.
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema timu tano tu za Daraja la Kwanza ndizo zilizowasilisha usajili kufikia jana kati ya 24 zilizopaswa kufanya hivyo.
Osiah, alikiri kuwapo na utata wa usajili wa baadhi ya wachezaji na kusema suala hilo litatolewa uamuzi mapema na Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi ya Wachezaji.
"Kuna utata umejitokeza kwa baadhi ya fomu za usajili kwa wachezaji wa timu za Simba ,Yanga na Azam, kamati husika katika hilo itatoa ufafanuzi," alisema Osiah.
Kuhusu timu za Daraja la Kwanza zilizowasilisha majina ni pamoja na Tesema, Polisi na Transit Camp (Dar es Salaam), Mkamba, Moro United (Morogoro).
Rooney ashangilia, asema sasa ni Rom + Roo
LONDON, England
KOCHA wa Arsenal, aliyekuwa akisuasua kumuuza Robin van Persie kwenda Manchester United amekubali kwa dau la Pauni 24 milioni.
Arsenal ilithibitisha kukamilika kwa 'dili' hilo na mchezaji huyo amekwenda Manchester kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.
Klabu hiyo ilikubalia kuanzishwa upya kwa mazungumzo, na lengo ni kumchukua mchezaji huyo na sas Van Persie ni mchezaji halali wa United.
Alex Ferguson alisema, kumsajili mchezaji huyo, sasa itakuwa kazi kwa Manchester City kutetea taji lake.
Wenger alifanya kazi ya ziada kumshawishi Van Persie kubakia lakini ilishindikana na Van Persie alikuwa anataka kuondoka tu.
Kocha huyo wa Arsenal aliulizwa na Televisheni ya Ufaransa kama alikuwa na mpango wa kununua mchezaji mwingine: "Tayari tumeshanunua mchezaji, yuko [Lukas] Podolski na [Olivier] Giroud. Tunasikitika kumpoteza mchezaji mwenye ubora, lakini mkataba wake umebakia mwaka mmoja na hatuna jinsi."
Van Persie aliweka wazi katika taarifa yake ya Julai 4 kwamba anataka kutwaa mataji. Kwa njia nyingine, hafurahishwi na jinsi Arsenal FC inavyokwenda". Alikataa moja kwa moja kumwaga wino na alikuwa amebakiwa na miezi 12. Arsenal ilikuwa ikimtaka kwa udi na uvumba mchezaji huyo.
Taarifa ya Arsenal ilisema: "[Sisi] kama Arsenal tunathibitisha Robin van Persie amekwenda Manchester United. Van Persie anakwenda Manchester kwa ajili ya kufanyiwa vipimo kabla ya kuanza mazoezi."
Arsenal ilitangaza Paundi 20 milioni kama bei ya kumuuza mchezaji huyo. Kabla ya kwenda nchi za Asia Julai 21, ambako Van Persie hakwenda na klabu ilipokea ofa kutoka klabu za United, City na Juventus, ambazo zote zilimtaka kwa Paundi 15 milioni.
Juzi United iliandika kwenye mtandao wake kuwa "Taarifa Mtu aliyekuwa na furaha alikuwa Wayne Rooney, ambaye alisema sasa safu yao ya ushambuliaji imekamilika.
"Van Persie ni mkali," Rooney alisema. "Amefanya makubwa akiwa na Arsenal kwa miaka mingi. Kuja kwake kutaongeza thamani ya timu na sasa itakuwa Rom + Roo."
Kikwete azitaka Barca, Madrid kuja nchini
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa bado Serikali ina dhamira ya kuileta moja ya timu za Ligi Kuu ya Soka ya Hispania, 'La Liga' kuja Tanzania na amemtaka Balozi mpya wa Hispania nchini kusaidia kufanikisha mpango huo.
Aidha, Kikwete ameipongeza Hispania kwa kufanikiwa kutetea ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Ulaya katika mashindano yaliyomalizika mwezi uliopita nchini Poland na Ukraine.
Rais Kiwete alisema hayo jana Ikulu, jijini Dar es Salaam katika hafla ya utambulisho wa balozi mpya wa Hispania nchini, Luis Manuel Cuesta Civis.
Kikwete alisema: “Wananchi wa Tanzania, ambako timu za Hispania, zina washabiki na wafuasi wengi, bado wanasubiri kwa hamu ziara ya moja ya timu kubwa za Ligi Kuu ya Soka ya Hispania. Tunataka ije hapa, icheze mechi moja ama mbili na itembelee mbunga zetu maarufu za wanyama.”
Aliongeza:“Kama utakavyokuja kuthibitisha mwenyewe, Watanzania ni watu wanaopenda michezo na hasa soka na ni wafuatiliaji wakubwa wa Ligi Kuu ya Hispania ambako timu zenye mvuto zaidi ni Real Madrid na Barcelona.”
“Tunawapongeza sana kwa kuweka historia. Kwanza mlishinda Kombe la Mataifa ya Ulaya, kisha mkashinda Kombe la Dunia. Sasa mmeweza kutetea Kombe la Ulaya. Hili halijapata kutokea kwa nchi moja kushikilia
vikombe vyote viwili vikubwa vya soka duniani kwa wakati mmoja ama nchi kutetea Kombe la Ulaya.”
Wakati huohuo, serikali imesema imeridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wanamichezo walioshiriki michezo ya Olimpiki iliyomalizika Jumapili iliyopita, London, England.
Pamoja na wanamichezo hao kurudi bila medali, lakini serikali imesema wanastahili pongezi kwa vile walijitahidi kushindana kadri walivyoweza.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Leonard Thadeo wakati wa hafla ya chakula
cha usiku kwa wanamichezo iliyofanyika muda mfupi baada ya kuwasili.
"Mmetujengea heshima kubwa Olimpiki, miaka ya nyuma wanamichezo wetu waliokuwa wakituwakilisha baada ya mashindano wanazamia uko, lakini nyinyi hakufanya hivyo" alisema Thadeo.Mbali na
kuwapongeza wanamichezo hao, pia Thadeo aliwakabidhi vyeti na medali za ushiriki kwenye michezo ya Olimpiki.
Katika michezo hiyo, Tanzania iliwakilishwa na wanamichezo wa masumbwi, riadha na kuogelea, ambapo waliishia hatua ya makundi.
Thursday, August 16, 2012
Rais wa Nigeria ataka mabadiliko
Rais Goodluck Jonathan
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan, ameamuru mabadiliko yafanyike katika sekta ya michezo baada ya taifa hilo kukosa kushinda hata medali moja katika michezo ya Olimpiki.
Waziri wa Habari Labaran Maku amesema rais anataka mageuzi makubwa katika sekta hiyo ili kurejesha hadhi ya taifa hilo katika michezo.
Wachanganuzi wanasema, matokeo ya Nigeria katika mashindano ya olimpiki ya London mwaka huu yalikuwa mabaya zaidi katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.
Rais Jonathan, aliwasilisha suala hilo wakati wa kikao cha baraza la mawaziri kilichofanyika katika mji mkuu Abuja.
''Naamini kile taifa hili linahitaji kwa sasa ni kutathmini kile kilichotendeka na kufanya mabadiliko, ili kurejesha heshima na hadhi ya taifa hilo'' alisema Bwana Maku.
Nigeria ndilo taifa lenye idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika, na linajihisi kama taifa lenye ushawishi mkubwa zaidi.
Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Bi. Hillary Clinton, amesema hatma ya Nigeria siku zijazo ni nzuri ikiwa taifa hilo litaendeleza mikakati yake ya kupambana na ufisadi.
Bi. Clinton aliyasaema hayo wakati alipofanya kikao na rais Goodluck Jonathan, katika mji mkuu wa nchi hiyo Abuja.
Nigeria ni miongoni mwa mataifa yanayoongoza kwa uzalishaji wa mafuta duniani, lakini viwango vya ufisadi viko juu zaidi, hali ambayo imehujumu ufanisi wa taifa hilo.
STARS YATOKA SARE KWENYE FRIEND MATCH
Mabeki wa Taifa Stars wakimwangilia mshambuliaji wa timu ya taifa ya Botswana akifunga bao la tatu wakati wa mechi ya kirafiki iliyochezwa jana kwenye uwanja wa Molepolole mjini Gaborone.
Taifa Stars imetoka sare ya mabao 3-3 na wenyeji Botswana (Zebras) katika moja kati ya mechi kadhaa za kirafiki za kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) zilizochezwa jana (Agosti 15 mwaka huu) usiku.
Hadi mapumziko kwenye mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Molepolole ulioko Kilometa 40 nje ya Jiji la Gaborone, timu hizo zilikuwa zimefungana mabao 2-2. Stars ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 17 lililofungwa kwa penalti na beki Erasto Nyoni.
Mwamuzi Lekgotia Johannes Stars alitoa adhabu hiyo baada ya beki Oscar Obuile Ncenga wa Zebras kumuangusha ndani ya eneo la hatari mshambuliaji Mrisho Ngasa aliyekuwa akimkabili kipa Mompoloki Sephekolo.
Bao hilo halikudumu muda mrefu, kwani Zebras walisawazisha dakika ya 26 baada ya shuti kali lililopigwa na Lemponye Tshireletso nje ya eneo la hatari kumshinda nahodha wa Taifa Stars, Juma Kaseja. Dakika tano baadaye kiungo mshambuliaji Mwinyi Kazimoto aliifungia Stars bao la pili kwa shuti la mbali.
Tshireletso aliisawazishia tena Zebras dakika ya 37. Mfungaji alifunga bao hilo kwa kichwa akiunganisha mpira wa krosi kutoka wingi ya kushoto uliopigwa na Tebogo Sembowa ambaye kabla alimtoka beki Aggrey Morris.
Kipindi cha pili kilianza kwa Kocha Kim Poulsen wa Stars kuwatoa Frank Domayo na Salum Abubakar na nafasi zao kuchukuliwa na Shabani Nditi na Athuman Idd. Safari hii Zebras ndiyo walioanza kufunga dakika ya 69 ambapo kiungo Michael Mogaladi aliifungia bao la tatu kwa kichwa akiunganisha krosi fupi iliyotokana na mpira wa kurusha.
Dakika 13 za mwisho Stars walicheza pungufu baada ya beki Erasto Nyoni kutolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na kumchezea rafu mshambuliaji Lovemore Murirwa.
Mrisho Ngasa ambaye alikuwa nyota kwenye mchezo huo aliisawazishia Stars dakika ya 84 baada ya kugongeana one-two na mshambuliaji Simon Msuva aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Haruna Moshi.
"Licha ya timu kucheza vizuri, tatizo kubwa lilikuwa kwenye safu ya ulinzi ambapo mabeki waliruhusu mipira mingi ya krosi na kuwaacha washambuliaji wa Botswana wakifunga bila bughudha. Mabeki hawatakiwi kuruhusu mipira ya krosi, wakiruhusu ni lazima wahakikishe wanawadhibiti washambuliaji wa timu pinzani.
"Kwa upande wa washambuliaji, Said Bahanuzi alikuwa akicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa akiwa na Stars tangu nilipomjumuisha kwenye timu kwa mara ya kwanza. Kuna makosa madogo madogo ambayo niliyatarajia, hivyo nitamrekebisha polepole," alisema Kocha Poulsen mara baada ya mechi hiyo.
Stars; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Amir Maftah, Aggrey Morris, Kelvin Yondani, Frank Domayo/Shabani Nditi, Mrisho Ngasa, Salum Abubakar/Athuman Idd, Said Bahanuzi/Simon Msuva, Haruna Moshi/Ramadhan Singano na Mwinyi Kazimoto.
Zebras; Mompoloki Sephekolo, Tshepo Motlhabankwe/Tshepo Maikano, Edwin Olerile, Oscar Obuile Ncenganye, Mompati Thuma, Patrick Motsepe/Jackie Mothatego, Lemponye Tshireletso, Michael
Mogaladi, Tebogo Sembowa, Ntesang Simanyana na Galabgwe Moyana/Lovemore Murirwa.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inarejea nyumbani leo (Agosti 16 mwaka huu) ambapo itawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 1.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways.
ROBIN VAN PERSIE AKUBALI KUJIUNGA NA TIMU YA MANCHESTER UNITED.
Robin Van Persie
MCHEZAJI Wayne Rooney wa Manchester United hivi sasa amepata pacha wake ambaye ni RVP, yaani Robin Van Persie ambaye usiku wa kuamkia leo amenunuliwa na klabu hiyo kwa mpunga wa Pauni milioni 22 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 54.3
RVP anatarajiwa leo kwenda Old Trafford kwa ajili ya vipimo vya afya yake na kusaini mkataba ambapo atakuwa akilipwa zaidi ya Pauni 200,000 kwa wiki ambazo ni sawa na Sh. Milioni 493.7
Kwa mujibu wa mtandao wa SunSport, kocha Fergie wa United anategemea kukamilisha uhamisho huo kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya England.
Van Persie atakuwa mshambuliaji wa mbele ambapo Rooney atakuwa akimsaidia kwa nyuma.
Mchezaji huyo amejiunga na klabu hiyo baada ya kugombewa pia na Manchester City na Juventus ya Italia.
Mzee Wenger wa Arsenal alisema kwamba: “Inasikitisha sana kumpoteza mchezaji muhimu kama huyo. Alikuwa bado ana mwaka katika mkataba wake hivyo hatukuwa na jinsi bali kumwacha aondoke.”
MCHEZAJI Wayne Rooney wa Manchester United hivi sasa amepata pacha wake ambaye ni RVP, yaani Robin Van Persie ambaye usiku wa kuamkia leo amenunuliwa na klabu hiyo kwa mpunga wa Pauni milioni 22 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 54.3
RVP anatarajiwa leo kwenda Old Trafford kwa ajili ya vipimo vya afya yake na kusaini mkataba ambapo atakuwa akilipwa zaidi ya Pauni 200,000 kwa wiki ambazo ni sawa na Sh. Milioni 493.7
Kwa mujibu wa mtandao wa SunSport, kocha Fergie wa United anategemea kukamilisha uhamisho huo kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya England.
Van Persie atakuwa mshambuliaji wa mbele ambapo Rooney atakuwa akimsaidia kwa nyuma.
Mchezaji huyo amejiunga na klabu hiyo baada ya kugombewa pia na Manchester City na Juventus ya Italia.
Mzee Wenger wa Arsenal alisema kwamba: “Inasikitisha sana kumpoteza mchezaji muhimu kama huyo. Alikuwa bado ana mwaka katika mkataba wake hivyo hatukuwa na jinsi bali kumwacha aondoke.”
RASHID MATUMLA AANZA KUJIFUA RASMI ILI KUMKABILI MANENO OSWAD.
Kocha Mkongwe wa mchezo wa Masumbwi nchini Habibu Kinyogoli 'kushoto' akimfua bondia Rashid Matumla wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala. Matumla anajiandaa kupambana na Maneno Osward siku ya Iddi Mosi kwenye pambano litakalofanyika katika ukumbi wa Dar Live .
Subscribe to:
Posts (Atom)











































