HABARI ZA KIJAMII.COM
tangazo
Tuesday, July 9, 2013
MWANAFUNZI AJILIPUA KWA MOTO KISA MAPENZI.
MWANAFUNZI wa Chuo cha Ufundi (VETA), mkoani Dodoma, Taliki Juma (22), amedaiwa kujiua kwa kujilipua kwa petroli kisa mapenzi.
Taarifa
zinasema, kufuatia moto mkali uliotokana na petroli hiyo, mbali na
mwanafunzi huyo aliyejitia mhanaga kwa mapenzi, watu wengine wanane
waliokuwa karibu na moto huo nao walijeruhiwa vibaya.
Akithibitisha,
leo Kamanda wa Polisi wa mkoa, David Misime, amesema tukio hilo
lilitokea jana mida ya saa 12.30 jioni katika Kitongoji cha Machaka,
Kata ya Nzughuni.
Kamanda
alifafanua kwamba mapema mwanafunzi huyo alinunua lita tano za mafuta ya
petroli katika kituo cha mafuta cha Nanenane na kisha kujilipua na
kisha kwenda kujilipua akiwa katika saluni ya Irene Mapunda ambaye
inasadikiwa alikuwa mpenzi wake.
Alisema,
mwanzoni watu waliokuwa karibu naye walijaribu kumsihi asijilipue lakini
hawakufanikiwa, kwani aliwasha kibiriti ndani ya saluni hiyo na
kusababisha moto mkubwa kulipuka ambao uliwaunguza wengine waliokuwa
karibu naye pamoja na mali zote zilizokuwa ndani ya Saluni hiyo
kuteketea.
"Uchunguzi
wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi,
hata hivyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linaendelea na uchunguzi wa
kina juu ya tukio hili," ilieleza taarifa ya Kamanda wa Polisi.
Taarifa
iliwataja waliojerihiwa kuwa ni Mugina Hessein (32), Benson Mushi (11)
Japhet Japhet (18), Meshack John (18), Swaibu Kassim (20),Ester Silau
(30), Shaban Pili (20) na Fedrick Gabriel (21) ambao wote wamelazwa
katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na tathimini ya hasara
iliyosababishwa na moto huo bado haijafahamika.
CHADEMA WASUSIA KONGAMANO LA TCD.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema hakitashiriki kongamano la amani lililoandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), chini ya ufadhili wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo wa chama hicho, Benson Kigaila, alisema chama chake kinazo sababu nyingi za kususia kongamano hilo.
Katika taarifa hiyo, Kigaila alimtuhumu Mwenyekiti wa TCD, James Mbatia, kwamba amekiuka maazimio ya kikao cha kuteua mwezeshaji wa mkutano huo na badala yake amefungamana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uteuzi.Alisema Chadema haitashiriki kwa sababu amani ya nchi haijadiliwi na watu 70, bali amani inatengenezwa kwa kuzingatia uwepo wa mazingira ya haki na usawa.
Kigaila alisema Serikali, ambayo inatuhumiwa kwa uvunjifu wa haki za binadamu, haiwezi kujisuluhisha yenyewe na kuongeza kwamba amani si mali ya vyama vya siasa, bali ni tunu inayohusisha wadau mbalimbali.Alisema Pinda, ambaye amekuwa mstari wa mbele kutoa lugha za uchochezi, chuki, uhasama, ubabe, ukiukwaji na za vitisho, hawezi kuwa na fursa ya kuwa mwenyekiti wa kongamano la amani.Kigaila alisema chama chake hakitashiriki kwa sababu Serikali ya CCM imejaa unafiki, kwani imekuwa ikihubiri amani mchana wakati usiku inachochea udini na kuwagawa Watanzania kwa misingi ya imani za kidini na vyama.“Tumepokea barua saa saba leo (jana) kutoka TCD ikitualika kushiriki kongamano la amani, tumekutana kwa dharura kujadili mwaliko huo wa ghafla.“Tunataka umma utuelewe kwamba tuna dhamira ya dhati ya kuona Tanzania inakuwa kisiwa cha amani, lakini hatukubali kushiriki katika vikao ambavyo viongozi hawana dhamira nzuri, hatutaki kutumia gharama ya Sh milioni 400 ambazo ni kodi za Watanzania wanyonge bila mafanikio,” alisema.Mbatia atoa ufafanuzi Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TCD, James Mbatia, aliishangaa Chadema kwa uwamuzi huo na kusema kuwa tuhuma zilizoelekezwa kwake ni za uwongo.Mbatia, ambaye pia ni Mbunge wa Kuteuliwa na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, alisema Pinda hawezi kuendesha kongamano hilo kwa kuwa yupo katika safari ya kikazi mkoani Njombe.“Ni vema wenzetu wasusia wafanye hivyo kwa jambo la msingi, lakini si katika hili. Kwanza nawashangaa wanasusiaje wakati wao walishiriki kikao cha kupanga kongamano hili Februari 7, mwaka huu Dodoma,” alisema.Kwa mujibu wa Mbatia, mada zilizopangwa kujadiliwa ni amani na demokrasia itakayowasilishwa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ole Gabriel na vyombo vya habari na usalama itakayowasilishwa na mwandishi wa habari mkongwe, Ayoub Rioba.
WANASWA NA JNIA KWA DAWA ZA KULEVYA,YASEMEKANA NI MTU NA MPENZI WAKE.
Dar es Salaam . Jeshi la Polisi Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya, linawashikiliwa watu wawili, wanaodaiwa kuwa ni mtu na mpenzi wake kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroin kilo mbili zinazokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi Sh90 milioni.
Mkuu wa kitengo hicho, Godfrey Nzowa aliliambia gazeti hili jana kuwa watuhumiwa hao ambao mmoja ni mwanamke walikamatwa juzi saa 8 mchana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Alisema watuhumiwa walikuwa wakisafiri kwenda Mji wa Bangkok Thailand kupitia Addis Ababa, Ethiopia ambapo walikata tiketi ya ndege la shirika hilo.
“Walipoanza kufanya ukaguzi watuhumiwa hawa walijichomeka katikati ya wenzao ndipo tulipowanasa na dawa hizo ambazo walizificha kwenye mabegi yao katikati ya nguo,” alisema Nzowa.
Alisema kuwa watuhumiwa hao waligawana dawa hizo kwani walipofanyiwa upekuzi na polisi walikutwa kila mtu akiwa na kilo moja.
MJUKUU WA MANDELA AZUA TAFRANI JENGINE...ATAKA KUMSHTAKI WAKILI.
Johannesburg. Wakili wa mjukuu wa Mandela, Gary Jansen anatarajia kumfungulia mashtaka wakili wa familia ya Mandela kwa kuidanganya mahakama kuhusu afya ya Mandela.
Jansen alisema angefungua kesi hiyo jana ingawa
hadi muda wa mahakama unakwisha alikuwa hajafungua shtaka lolote dhidi
ya wanafamilia ya Mandela na wakili wao.
“Mteja wangu amejisikia vibaya, alipenda na
anaheshimu matakwa ya babu yake na wala hakutaka haya mambo yawe
hadharani hadi kwenye vyombo vya habari,” alisema Smith Wakili wa
familia ya Mandela, David Smith ambaye anawasimamia binti mkubwa wa
Mandela, Makaziwe, mke wa sasa Graca Machel na mke wa zamani, Winnie
Madikizela Mandela aliiambia mahakama Juni 26, kupitia haki ya kiapo
kuwa shujaa huyo wa Afrika, yu mahututi kiasi cha madakatri kushauri
mashine ya kupumulia iondolewe.
Tuhuma za kuwa Mandela yupo mahututi na huenda
akafariki wakati wowote, ilimsababisha hakimu kufanya uamuzi wa haraka
ya kusikilizwa kwa kesi hiyo na hatimaye miili ya watoto watatu wa
Mandela kufukuliwa kisha kuzikwa upya huko Qunu.
Hatua hiyo ya mahakama ilifanyika baada ya
kuonekana kuwa Mandela aliwahi kutamka kuwa angependa kuzikwa katika
eneo ambalo watoto wake wengine wamezikwa.
Gerald Bloem, Mwenyekiti wa Baraza la Mahakama ya
Eastern Cape Bar alisema wachunguzi wanaweza kuwaita wanafamilia ya
Mandela kutoa ushahidi kama mashauri ya kinidhamu dhidi ya wakili wa
familia yataendelea.
Hata hivyo, Bloem alieleza kuwa wakili Smith
huenda akakumbana na mkondo wa sheria iwapo itabainika kuwa aliidanganya
mahakama kuhusu afya ya Mandela na atatakiwa kutoa ushahidi ambao
madaktari watakosa pa kuupata.
Wanafamilia hao, walikataa kuzungumza lolote juu
ya hatua za Jansen na mteja wake, Mandla zinazotarajiwa kuchukuliwa
ingawa Denis Goldberg, rafiki wa karibu wa Mandela, alipomtembelea wiki
iliyompita alithibitisha kuwa hakuwa mahututi na aliweza kunyanyua
viungo vyake, sambamba na kutambua sauti.
Goldberg alizungumza na waandishi wa habari na
kuthibitisha kuwa madaktari wamekataa Mandela asiondolewe mashine ya
kupumulia kwani afya si mbaya hadi pale moja ya ogani zake
itakaposhindwa kufanya kazi kabisa.
Wakati huo huo, Mandla amemcheka Mfalme wa Wazulu,
AbaThembu, Buyelekhaya Dalindyebo ambaye alitangaza kumng’oa Uchifu,
kuwa hana sifa za kufanya hivyo.
Dalindyebo alitangaza kumvua Uchifu Mandla kwa
madai kuwa amepoteza heshima yake baada ya kuwa na mgogoro na
wanafamilia wenzake kuhusu mabaki ya miili ya watoto watatu wa Mandela.
Mfalme huyo alisema Mandla hafai kuongoza watu wa
Mvezo kwa kuwa ameipoteza heshima yake ambayo aliipata awali na
kutawazwa kuwa chifu baada ya kulichafua jina la familia inayoheshimika
ya Mandela.
Hata hivyo, Mandla aliikebehi kauli ya mfalme Dalindyebo akisema kuwa mfalme huyo hana msimamo na hekima.
Hata hivyo, Mandla aliikebehi kauli ya mfalme Dalindyebo akisema kuwa mfalme huyo hana msimamo na hekima.
Msemaji wa Mandla, Freddy Pilusa alisema kumfukuza
Chifu kunahitaji mchakato mrefu na ushahidi wa makosa aliyoyafanya na
si kuamka na kuamua kuwa unamfukuza Chifu.
“Huwezi tu kuamka siku moja na kuitisha mkutano na kufanya uamuzi kama huo,” alisema Pilusa.
Hata hivyo, msemaji wa nyumba ya kifalme, ya
kabila la Abathembu, Nkos Daludumo Mtirara alisema: “Sisi tunaona kauli
ya Dalindyebo kama utani tu, kwa sababu alikwishaondolewa kwenye cheo
hicho miezi tisa iliyopita.
“Tunamtambua Mandla kuwa bado ni chifu kwa sababu,
bado Serikali haijamuondoa Mandla katika cheo chake na anaendelea
kupata haki na heshima yake kama kawaida.”
Mtirara alisema kauli ya Zwelibanzi ni ya kuharibu
mila na tamaduni, kuchonganisha na kukuza jambo hili kwa sababu hata
yeye hana mamlaka.
“Tunajua kuwa Zwelibanzi anavuta sana ‘Dagga’ na
tunafahamu kuwa Zwelibanzi yupo katika operesheni ya kuivuruga familia
ya Mandela” alisema Mtirara.
Thursday, June 13, 2013
MUUAJI WA DADA ALIYECHINJWA KAMA KUKU MIKOCHENI B APATIKANA.
MFANYAKAZI wa Jaji Kileo, Philemon Laiza (27) anadaiwa kumchinja mtumishi wa ndani wa jaji huyo, ambaye ni raia wa Kenya, Perpetua Mainab (30).
Mtuhumiwa huyo, ambaye alikuwa ni mtunza bustani katika nyumba ya Jaji Kileo, alifanya unyama huo wiki iliyopita.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum, Suleiman Kova, alisema mwili wa mtumishi huyo wa ndani ulikutwa kwenye dampo la kutupia takataka maeneo ya Mikocheni B.
“Mfanyakazi huyo wa ndani alikutwa ameshakufa baada ya mwili wake kuchinjwa sehemu ya shingo, jeraha sehemu ya mkono wa kushoto karibu na kiganja, jeraha kwenye paji la uso na mwili wake ukiwa umetapakaa damu sehemu za kichwani,” alisema Kova.
Alieleza kuwa mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa akifanya kazi pamoja na marehemu, alikiri kuwa na marehemu siku hiyo ya Ijumaa ya Juni 8 mwaka huu.
Alisema baada ya polisi kufanya upelelezi mtuhumiwa alikutwa na kiatu kimoja cha marehemu na nguo alizovaa siku ya tukio, ambazo zilikuwa zimetapakaa damu.
“Nguo hizo za marehemu zilikuwa zimetapakaa damu na baada ya mahojiano ya muda mrefu, mtuhumiwa alikiri kuhusika na tukio hilo.
Kamishna Kova alisema kuwa mtuhumiwa alipohojiwa alidai kuwa marehemu alitoweka nyumbani tangu siku ya Ijumaa na baada ya kubanwa na polisi mtuhumiwa alikiri kuhusika na tukio hilo.
Kova alisema mtuhumiwa bado anahojiwa na upepelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.
Tuesday, June 11, 2013
MBUNGE ASOTA RUMANDE KWA KUSHINDWA KUTIMIZA MASHARTI YA DHAMANA.
Mbunge
wa Mtwara Mjini (CCM), Hasnein Murji jana alifikishwa katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi mkoani hapa akituhumiwa na kosa la uchochezi. Baada ya
kusomewa shtaka hilo, mbunge huyo alirudishwa rumande kutokana na
kushindwa masharti. Sharti hilo lilikuwa ni kuwa na pasi ya kusafiria,
ambayo alikuwa ameiacha Dar es Salaam alikokamatwa.
Murji
amepandishwa kizimbani ikiwa ni moja ya mkakati wa vyombo vya dola
kuwasaka na kuwafungulia mashtaka watu inaowatuhumu kuhusika kuchochea
vurugu ambazo chanzo chake ni kupinga ujenzi wa bomba la kusafirisha
gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.
Mwendesha
Mashtaka ambaye ni Wakili wa Serikali, Zuberi Mkakatu aliieleza
Mahakama kuwa mnamo Januari 19, mwaka huu, maeneo ya Ligula mkoani hapa
mtuhumiwa alichochea watu kutenda makosa.
Hakimu
Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Mtwara, Dynes Lyimo alisema dhamana iko wazi kwa
mshtakiwa kwa masharti matatu. Kuwasilisha hati ya kusafiria mahakamani
na kuwa na mdhamini mmoja mkazi wa Mtwara ambaye atasaini mali
isiyohamishika isiyopungua Sh20 milioni. Sharti la tatu lilikuwa
mshtakiwa kutoruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara pasipo kibali cha
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara.
Mbunge
huyo anayewakilishwa na Wakili Chaula Msechu alifikishwa mahakamani hapo
jana saa 3.15 asubuhi akiwa katika gari la polisi huku ulinzi ukiwa
umeimarishwa. Polisi waliokuwa na silaha na wengine wakiwa na mbwa
walikuwa wametanda mahakamani.
Mbali ya
mahakamani, polisi walikuwa wakipita katika barabara mbalimbali za
Mtwara sambamba na askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Licha ya
matangazo mbalimbali ya polisi kwamba hakutakuwa na tishio la uvunjifu
wa amani, baadhi ya wananchi waliogopa kufungua biashara zao na wengine
wakikimbia mji.
Washtakiwa 91 chanzo mwananchi.
Subscribe to:
Posts (Atom)