tangazo

Tuesday, May 28, 2013

KIJANA MUUZA BANGI AMCHINJA POLISI KWA KISU SINGONI.






Na Makongoro Oging, Gladness Mallya na Issa Mnally:
 
Kijana mmoja mkazi wa Kurasini jijini Dar, Francis Huruma maarufu kwa jina la Big anayedaiwa kuuza madawa ya kulevya aina ya bangi, amemchinja polisi mwenye namba H.617 Anthony Pasco (22). Tukio hilo la aina yake lilitokea hivi karibuni katika Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Ugimbi uliopo Kurasini, Dar.
Mbali na kumchinja kwa kisu polisi huyo shingoni na kutofanikiwa kumuua kama alivyokusudia, Big pia alimjeruhi vibaya polisi mwingine mwenye namba H.334 Akili Mlawa (23) kwa kisu mguuni na mkononi. Pichani ni Francis Huruma maarufu kwa jina la Big enzi za uhai wake.

Polisi wote waliopatwa na majeraha wamelazwa katika Hospitali ya Jeshi la Polisi, Kilwa Road, jijini Dar. Raia walioshuhudia tukio hilo, walimvamia Big kisha wakamshushia kipigo na baadaye akafariki dunia wakati akitibiwa katika Hospitali ya Temeke, Dar.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, ACP Engelbert Kiondo alisema kuwa Big alifariki dunia katika hospitali hiyo wakati akipatiwa matibabu ya majeraha yaliyosababishwa na kipigo. Awali, wakazi wa eneo hilo walitoa taarifa polisi kutokana na kijana huyo kudaiwa kuendeleza uuzaji wa madawa ya kulevya na pombe aina ya viroba, jambo lililodaiwa kuchochea uhalifu katika kitongoji chao.

Ilidaiwa kuwa Big alikuwa akiwasababisha vijana wengi kutofanya kazi na kutumia muda mwingi kuvuta madawa ya kulevya kisha kufanya uhalifu eneo hilo.

Kamanda Kiondo alisema polisi walifanya msako mkali wa kupambana na uhalifu na kufanikiwa kumtia mbaroni kijana huyo.
“Big alikuwa mbogo na kufanikiwa kumchinja Pasco shingoni lakini hakufanikisha lengo lake la kutaka kumuua,” alisema Kamanda Kiondo.

Baada ya kuona Big amewashambulia polisi, wananchi waliongeza nguvu na kutoa msaada kwa kutumia matofali kumshushia kichapo kijana huyo.

Kamanda Kiondo alisema polisi wengine waliokuwa katika zoezi hilo, walimuokoa Big kutoka kwenye kichapo hicho na kumpakia kwenye gari kisha kumkimbiza kituoni na baadaye katika Hospitali ya Temeke.

Big alipatiwa matibabu katika Hospitali ya Temeke ambako hakuna ndugu yake yeyote aliyejitokeza kwa ajili ya kumuwekea dhamana na baada ya kufanyiwa vipimo alionekana kuwa na malaria pamoja na maumivu makali kutokana na kipigo.

Jitihada za kuokoa maisha ya Big zilishindikana kwani alifariki dunia wakati akiendelea na matibabu.

Hata hivyo, Kamanda Kiondo alisema msako mkali bado unaendelea katika Mkoa wa Kipolisi wa Temeke hasa maeneo ya Mtongani na Mto Mzinga ambako vijana wengi wanafanya uhalifu na kutumia muda mwingi kucheza kamari, kuvuta bangi na kulala na wake za watu kwa kuwatishia wenye wake zao.

“Wazazi wengi wamekuwa wakiwaficha vijana wao pindi wanapotafutwa kwa uhalifu kwani fedha wanazopata kwa njia hizo, nao huzitumia.

“Jeshi la polisi limejipanga kikamilifu kupambana nao,” alisisitiza Kamanda Kiondo.

Polisi waliojeruhiwa wote wanaendelea vizuri na matibabu katika Hospitali ya Kilwa Road.

NASHON KAMINYOGE AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA PIKIPIKI.(baadhi ya picha za sehemu ya tukio)

                       Marehemu Nashon Kaminyoge enzi za uhai wake.

        Pikipiki ambayo marehemu nashon kaminyoge alipatanayo ajali.
        Damu ambayo marehemu alivuja sana na kupelekea kifo chake.
        Mabaki ya helmet ambalo marehemu alikuwa amelivaa kabla ya kupoteza maisha.

Gari ambalo marehemu NASHON KAMINYOGE alijigonga na kusababisha kupoteza maisha


Mungu ailaze roho ya marehemu Nashon Kaminyoge mahala pema peponi
Amin

Saturday, May 25, 2013

NIYONZIMA AONGEZA MKATABA WA MIAKA MIWILI YANGA.

yanga b09a3

Haruna Niyonzima (kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya Yanga SC, Jangwani wakati akitangazwa kusaini mkataba mpya leo. kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Abdallah Bin Kleb. Chanzo: GPL.

HATIMAYE kiungo wa kimataifa wa Rwanda,
Haruna Hakizimana Fadhili Niyonzima amesaini mkataba wa miaka miwili zaidi kuendelea kuichezea Yanga SC na klabu hiyo asubuhi ya leo imetangaza rasmi kuongeza mkataba na mchezaji huyo wa zamani wa APR na Rayon za kwao.

Kulikuwa kuna mvutano mkubwa kati ya Yanga SC na Haruna juu ya mkataba mpya na kiungo huyo ilikuwa aondoke kesho kurejea kwao, bila kusaini mkataba mpya.
Hata hivyo, kutokana na kuwapo kwa taarifa kwamba Simba SC imemtengea dau la Sh. Milioni 70 na Azam FC pia inamtaka kwa dau nono zaidi, Yanga imekubali kila alichoomba Haruna katika mkataba wake mpya. Chanzo: binzubeiry

MAGAZETI YA LEO JUMAAMOSI TZ 25/05/2013

00 a0713
0 e8e9f
1 a84dc
2 2b2ca
3 c9f38

4 33040
5 61155
6 97c91
7 e5600
8 ce8d6
9 21251
11 8414c
12 a72f7
13 932e1

Fainali ya kombe la klabu bingwa Ulaya, Wembley leo

g 7f9c1
Wachezaji wa Bayern Munich wakichuana na Borrusia Dotmund

FAINALI ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya kwa mara ya kwanza, itahusisha timu mbili kutoka Ujerumani siku ya Jumamosi, ishara ya ufanisi wa ligi kuu ya Bundesliga ya kuwekeza katika kukuza vipaji hasa raia wa nchi hiyo.
Maandalizi yote yameshakamilika katika uwanja wa Wembley, na Kombe la Ligi ya mabingwa wa ulaya linameremeta, likisubiri nani atakayelinyakua kati ya vilabu viwili vya Ujerumani vitakavyokutana kwenye fainali. Borussia Dortmund na Bayern Munich ziko tayari pia.

Mahasimu hao wa Ujerumani wamekuwa wakijiandaa kukutana ugenini Uingereza na mashabiki wamekuja kwa wingi.
Badala ya vilabu vya Uhispania na Uingereza ambayo vimekuwa vinahodhi soka ya Ulaya, sasa ni vilabu vya Ujerumani, licha kwamba nchini humo matajiri wakubwa hawaruhusiwi kumiliki vilabu.

Soka imeimarika Ujerumani?

Raia wengi wa Ujerumani wanasubiri fainali hiyo kwa hamu na ghamu na Chancellor Angela Markel atakuwepo katika Uwanja wa Wembley kutizama fainali hiyo.
Ikiwa huu ni mwanzo wa vilabu vya Ujerumani kutawala soka ya ulaya, haijalishi mashabiki wanashabikia klabu gani, tayari watakuwa washindi.
Takriban wachezaji wote wa timu ya taifa ya Ujerumani, watakuwa uwanjani wakati wachezaji wa Klabu ya Bayern Munich watakapotoana jasho na Borussia Dortmund, katika uwanja wa Wembley, wengi wa wachezaji hao wakiwa wametoka katika vyuo viwili vinavyomilikiwa na vilabu hivyo.
Hali hii kwa vilabu vingi vya uingereza ni kama ndoto. Na ila kufahamu jinsi vilabu hivi viliafikia ufanisi huu, tutaanza mwaka wa 2000.
Huo ni mwaka ambao Wajerumani walidhalalishwa katika mashindano ya bara Ulaya, wakati walipomaliza katika nafasi ya mwisho katika kundi lao hata bila kushinda mechi moja.
Wachezaji wengi wa timu ya Ujerumani waalikuwa wakonge na magazeti nchini Uholansi yaliandika kuwa ni fahari yao kuona viwango vya soka vikianguka na kuwa wakati wa Ujerumani kutawala mchezo huo umemalizika.
Wakati huo huo timu za taifa za wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 na 19 vile vile vilikuwa na matokeo mabaya, kwa sababu ya upungufu wa wachezaji wenye vipaji na ukosefu wa vilabu vya kutosha.
Kutokana na mazingira hayo yote, mchezo wa soka nchini Ujerumani ulionekana kuelekea kusambaratika zaidi, hatua iliyolazimisha shirikisho la mchezo wa soka nchini humo, vilabu na mashabiki kuanzisha mazungumzo ya pamoja, ya kutafuta mbinu ya kurekebisha hali hiyo.
Kilichofuata na mabadiliko ya kimsingi ikiwa ni pamoja ya kuwekeza zaidi katika vijana walionekana kuwa na vipaji na pia katika secta ya kuwahimiza vijana wengi kuanza kucheza mechi huo.
Mikakati hiyo ilianza kuzaa matunda na wachezaji wengi wasiozidi umri wa miaka 23, walianza kujumuishwa katika vikosi mbali mbali vya timu vilivyokuwa vikishiriki katika ligi kuu ya Bundesliga.
Mwaka wa 2006, timu ya taifa ya Ujerumani iliyojumuisha vijana wengi chipukizi ilimaliza katika nafasi ya tatu katika fainali za kombe la dunia na mwaka wa 2010 vile vile walimaliza katika nafasi hiyo.
Katika fainali hizo mbili za kombe la dunia, tuzo la mchezaji bora mchanga iliyakuliwa na wachezaji wa Ujerumani Lukas Podolski mwaka wa 2006 na Thomas Mueller mwaka wa 2010.
Tangu wakati huo vilabu vya Ujerumani na vimekuwa vikiandikisha matokeo mema, na mbali ya wachezaji wengi kusajiliwa na vilabu vinavyoshiriki katika ligi ya Bundesliga baadhi yao pia wamesajiliwa na vilabu vingine katika mataifa ya Ulaya.

Chanzo na BBC swahili.

Translate