tangazo

Thursday, June 13, 2013

MUUAJI WA DADA ALIYECHINJWA KAMA KUKU MIKOCHENI B APATIKANA.


MFANYAKAZI wa Jaji Kileo, Philemon Laiza (27) anadaiwa kumchinja mtumishi wa ndani wa jaji huyo, ambaye ni raia wa Kenya, Perpetua Mainab (30). 


Mtuhumiwa huyo, ambaye alikuwa ni mtunza bustani katika nyumba ya Jaji Kileo, alifanya unyama huo wiki iliyopita.

 Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum, Suleiman Kova, alisema mwili wa mtumishi huyo wa ndani ulikutwa kwenye dampo la kutupia takataka maeneo ya Mikocheni B.

“Tukio hilo lilitokea karibu na dampo la kutupia taka Mikocheni ‘B’, katika eneo linalomilikiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).

“Mfanyakazi huyo wa ndani alikutwa ameshakufa baada ya mwili wake kuchinjwa sehemu ya shingo, jeraha sehemu ya mkono wa kushoto karibu na kiganja, jeraha kwenye paji la uso na mwili wake ukiwa umetapakaa damu sehemu za kichwani,” alisema Kova.

Alieleza kuwa mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa akifanya kazi pamoja na marehemu, alikiri kuwa na marehemu siku hiyo ya Ijumaa ya Juni 8 mwaka huu.

Alisema baada ya polisi kufanya upelelezi mtuhumiwa alikutwa na kiatu kimoja cha marehemu na nguo alizovaa siku ya tukio, ambazo zilikuwa zimetapakaa damu.

“Nguo hizo za marehemu zilikuwa zimetapakaa damu na baada ya mahojiano ya muda mrefu, mtuhumiwa alikiri kuhusika na tukio hilo.

Kamishna Kova alisema kuwa mtuhumiwa alipohojiwa alidai kuwa marehemu alitoweka nyumbani tangu siku ya Ijumaa na baada ya kubanwa na polisi mtuhumiwa alikiri kuhusika na tukio hilo.

Kova alisema mtuhumiwa bado anahojiwa na upepelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.

NEW TRACK: LADY JAY DEE--YAHAYA.

Tuesday, June 11, 2013

BAADHI YA MAGAZETI YA LEO JUMAANNE TZ.



3 ded5d
4 d7f0c
5 5e857

6 5d1b0
7 47585


10 bd70c

12 592b4
13 843a3
14 703f7






15 ec293

MBUNGE ASOTA RUMANDE KWA KUSHINDWA KUTIMIZA MASHARTI YA DHAMANA.

murji 39ae7
Mbunge wa Mtwara Mjini (CCM), Hasnein Murji jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani hapa akituhumiwa na kosa la uchochezi. Baada ya kusomewa shtaka hilo, mbunge huyo alirudishwa rumande kutokana na kushindwa masharti. Sharti hilo lilikuwa ni kuwa na pasi ya kusafiria, ambayo alikuwa ameiacha Dar es Salaam alikokamatwa.

Murji amepandishwa kizimbani ikiwa ni moja ya mkakati wa vyombo vya dola kuwasaka na kuwafungulia mashtaka watu inaowatuhumu kuhusika kuchochea vurugu ambazo chanzo chake ni kupinga ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.

Mwendesha Mashtaka ambaye ni Wakili wa Serikali, Zuberi Mkakatu aliieleza Mahakama kuwa mnamo Januari 19, mwaka huu, maeneo ya Ligula mkoani hapa mtuhumiwa alichochea watu kutenda makosa.

Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Mtwara, Dynes Lyimo alisema dhamana iko wazi kwa mshtakiwa kwa masharti matatu. Kuwasilisha hati ya kusafiria mahakamani na kuwa na mdhamini mmoja mkazi wa Mtwara ambaye atasaini mali isiyohamishika isiyopungua Sh20 milioni. Sharti la tatu lilikuwa mshtakiwa kutoruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara pasipo kibali cha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara.

Mbunge huyo anayewakilishwa na Wakili Chaula Msechu alifikishwa mahakamani hapo jana saa 3.15 asubuhi akiwa katika gari la polisi huku ulinzi ukiwa umeimarishwa. Polisi waliokuwa na silaha na wengine wakiwa na mbwa walikuwa wametanda mahakamani.

Mbali ya mahakamani, polisi walikuwa wakipita katika barabara mbalimbali za Mtwara sambamba na askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Licha ya matangazo mbalimbali ya polisi kwamba hakutakuwa na tishio la uvunjifu wa amani, baadhi ya wananchi waliogopa kufungua biashara zao na wengine wakikimbia mji.
Washtakiwa 91 chanzo mwananchi.

Thursday, June 6, 2013

MAPOKEZI YA MWILI WA MAREHEMU ALBERT MANGWEAR UWANJA WA JAMUHURI.(BAADHI YA PICHA ZA MATUKIO)




















MWILI WA MAREHEMU ALBERT MANGWEAR WAAGWA MOROGORO.

 Mama Mzazi wa Mangweha, Denisia Mangweha akiwa nyumbani kwake kabla ya safari kuelekea Uwanja wa Jamhuri.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akiwasili nyumbani kwa Mama mzazi wa Mangweha.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera asubuhi hii amefika nyumbani kwa Mama Mangwea eneo la Kihonda Mazimbu Road na kumpa pole kwa niaba ya wakazi wote wa mkoa wa Morogoro. Baada ya kutoa pole, Mhe. Bendera aliongoza umati wa watu kutoka Kihonda kuelekea Uwanja wa Jamhuri kwa shughuli za kuaga mwili wa Albert Mangwea aliyefariki dunia Mei 28 mwaka huu nchini Afrika Kusini. Mangwea anatarajiwa kuzikwa katika makaburi ya Kihonda nje ya Kanisa la Mtakatifu Monica jirani kabisa na alipozikwa baba yake mzazi Mzee Keneth Mangwea.

Wakazi wa mjo wa morogoro waanza kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa marehemu albert Mangwea kabla ya kumpeleka katika Nyumba yake ya Milele. Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahala Pema.
 Baadhi ya wasanii na wananchi waliohudhulia uwanjani wakati wa kuaga mwili wa marehemu albert mangwea uwanja wa jamhuri morogoro. 
943280_10152915710755525_916679441_n
Watu wakiaga mwili wa Marehemu albert mangwea uwanja wa Jamhuri morogoro

Wednesday, June 5, 2013

MWILI WA MAREHEMU ALBERT MANGWEAR WAAGWA RASMI JIJINI DAR.(baadhi ya picha za tukio zima la uagaji)

Gari lililobeba Mwili wa Marehemu Albert Mangwea likiwa limeshawasili katika viwanja vya leaders tayari kwa wakazi wa jiji la Dar kutoa Heshima zao Za Mwisho Kabla ya Mwili Kusafirisha Mkoani Morogoro kwaajili ya Mazishi.
 Baadhi ya Ndugu, Jamaa na Marafiki pamoja na wana kamati wakijiandaa kuteremsha jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Albert Mangwea katika viwanja vya Leaders muda huu aliyefariki hivi karibuni Nchini Afrika Kusini.
Baadhi ya Ndugu, Jamaa na marafiki wa karibu sana na Marehemu Albert Mangwea wakiwa katika sura za majonzi katika viwanja vya Leaders muda huu.
Huku watu wakiendelea kujitokeza katika viwanja Leaders Club katika harakati nzima ya kutoa heshima ya mwisho ya ndugu yetu msanii wetu na kipenzi cha watu wengi muda huu mwili wa Marehemu Albert Mangwear ndio umeingia katika viwanja vya leaders Club.
Watu wakitoa Salamu za mwisho mbele ya mwili wa marehemu Albert Mangweah.
Mwanamuziki wa Bongo Fleva Naseeb Abdul A.K.A Diamond Platnumz akisubiria kutoa heshima zake za mwisho.
Mwili wa marhemu Albert Mangwea ukiwa kwenye jeneza tayari kwa watu  kutoa heshima za mwisho
Umati wa watu wakiwa wamepanga mstari tayari kwa kwenda kuaga huku kikosi cha msalaba mwekundu na polisi kikiwa stand by just incase anything happens.
Pichani ni Baadhi ya watu mashuhuri na watanzania wakiwa kwenye foleni kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Albert Mangwear.

Translate