Gari lililobeba Mwili wa Marehemu
Albert Mangwea likiwa limeshawasili katika viwanja vya leaders tayari
kwa wakazi wa jiji la Dar kutoa Heshima zao Za Mwisho Kabla ya Mwili
Kusafirisha Mkoani Morogoro kwaajili ya Mazishi.
Baadhi ya Ndugu, Jamaa na Marafiki
pamoja na wana kamati wakijiandaa kuteremsha jeneza lililobeba Mwili wa
Marehemu Albert Mangwea katika viwanja vya Leaders muda huu aliyefariki
hivi karibuni Nchini Afrika Kusini.
Baadhi ya Ndugu, Jamaa na marafiki
wa karibu sana na Marehemu Albert Mangwea wakiwa katika sura za majonzi
katika viwanja vya Leaders muda huu.
Huku watu wakiendelea kujitokeza katika viwanja Leaders Club
katika harakati nzima ya kutoa heshima ya mwisho ya ndugu yetu msanii
wetu na kipenzi cha watu wengi muda huu mwili wa Marehemu Albert
Mangwear ndio umeingia katika viwanja vya leaders Club.
Watu wakitoa Salamu za mwisho mbele ya mwili wa marehemu Albert Mangweah.
Mwanamuziki wa Bongo Fleva Naseeb Abdul A.K.A Diamond Platnumz akisubiria kutoa heshima zake za mwisho.
Mwili wa marhemu Albert Mangwea ukiwa kwenye jeneza tayari kwa watu kutoa heshima za mwisho |
Umati wa watu wakiwa wamepanga mstari tayari kwa kwenda kuaga huku kikosi cha msalaba mwekundu na polisi kikiwa stand by just incase anything happens. |
Pichani ni Baadhi ya watu mashuhuri na watanzania wakiwa kwenye foleni kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Albert Mangwear. |
No comments:
Post a Comment