tangazo

Tuesday, July 9, 2013

WANASWA NA JNIA KWA DAWA ZA KULEVYA,YASEMEKANA NI MTU NA MPENZI WAKE.

 

Dar es Salaam . Jeshi la Polisi Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya, linawashikiliwa watu wawili, wanaodaiwa kuwa ni mtu na mpenzi wake kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroin kilo mbili  zinazokadiriwa kuwa  na thamani  ya  zaidi Sh90 milioni.

Mkuu wa kitengo hicho, Godfrey Nzowa aliliambia gazeti hili jana kuwa watuhumiwa hao ambao mmoja ni mwanamke walikamatwa  juzi  saa 8 mchana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Alisema watuhumiwa walikuwa wakisafiri kwenda Mji wa Bangkok Thailand kupitia Addis Ababa, Ethiopia ambapo walikata tiketi ya ndege la shirika hilo.

“Walipoanza kufanya ukaguzi watuhumiwa hawa walijichomeka katikati ya wenzao ndipo tulipowanasa na dawa hizo ambazo walizificha kwenye mabegi yao katikati ya nguo,” alisema Nzowa.

 Alisema  kuwa watuhumiwa hao waligawana dawa hizo kwani walipofanyiwa upekuzi na polisi walikutwa  kila mtu akiwa na  kilo moja.

No comments:

Translate