tangazo

Friday, September 7, 2012

Falcao's father reaffirms transfer comments



 Radamel Garcia, father of Radamel Falcao, has once again risked upsetting Atletico Madrid fans by reaffirming that his son dreams of playing for rival Real Madrid.

Radamel Senior told Colombian radio station Todelar on Wednesday that his son had his heart set on a move to the Santiago Bernabeu, and would look to pursue a move at the end of the current season.

The striker, who scored a hat trick in Atletico's 4-1 Super Cup victory over Chelsea last Friday, was then moved to pledge his commitment to the Vicente Calderon outfit on Twitter.

However, speaking to Colombian radio station Antena 2, his father again confirmed his son's desire to wear the Blancos jersey.

"Saying my son wants to play for Real Madrid is not a sin. He always wants to play in the best teams in the world. The next club is for him to decide," he said.

Earlier on Wednesday, Goal.com exclusively revealed that Manchester City lead the race to sign the 60 million euro-rated former Porto hit man, something that was alluded to in Radamel Senior's original comments.

"His dream has always been to play for Real Madrid, even though clubs like Manchester City and Chelsea have shown an interest," he had said.

KAMPUNI YA BIA YA TBL YAKABIDHI FIFAA VYA MICHEZO KWA SIMBA NA YANGA



Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe (wa pili kushoto), akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa Msemaji wa Klabu ya Yanga, Louis Sendeu (kushoto) na akamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ , ikiwa ni sehemu ya udhamini wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji hicho kwa Klabu za Simba na Yanga, katika hafla iliyofanyika kwenye Ofisi ya TFF, jijini Dar es Salaam jana. Wa (pili kulia) ni Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba. PICHA ZOTE/DAILY MITIKASI BLOG
Msemajimaji wa Klabu ya Yanga, Louis Sendeu (kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ (kulia) wakionyesha kwa waandishi wa habari baadhi ya vifaa vya michezo baada ya kukabidhiwa na Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe (wa pili kushoto), ikiwa ni sehemu ya udhamini wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji hicho kwa Klabu za Simba na Yanga, katika hafla iliyofanyika kwenye Ofisi ya TFF, jijini Dar es Salaam jana. Wa (pili kulia) ni na Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba.

MWANDISHI ALIEJISALIMISHA POLISI MWENYEWE KATI YA WALE WATATU WALIOTANGAZWA KUSAKWA BAADA YA KIFO CHA MWANGOSI.

Kwa sababu za kiusalama ilikua picha yake isiwekwe hapa lakini yeye mwenyewe ameidhinisha iwekwe kwa sababu haogopi, Francis Godwin ni huyo mwenye nguo nyeusi.
 
Siku mbili baada ya kifo cha mwandishi mwenzao wa habari (Daudi Mwangosi) aliefariki kutokana na kulipukiwa na bomu akiwa mikononi mwa polisi waliokuwa wanatawanya wafuasi wa Chadema huko Iringa, mwandishi wa habari Francis Godwin ambae alikua rafiki wa marehemu amejisalimisha polisi kufata masharti ya taarifa iliyotolewa kwa yeye na wenzake wawili kusakwa na polisi.
 
Exclusive na millardayo.com namkariri Godwin akisema “kutokana na hali halisi ya kushuhudia tukio la mauaji ya Mwangosi, nilifukuziwa kwa nyuma na gari lisilokua na namba pia nilipofika nyumbani niliambiwa kuna watu walikuja kuniulizia lakini hawafahamiki, na taarifa zikatoka kwamba tunasakwa”
Kuhusu kujisalimisha, Godwin amesema aliamua kufanya huo uamuzi baada ya kusikia taarifa za kusakwa kwake pamoja na waandishi wengine wawili, jana (september 5) aliamua kujisalimisha mwenyewe Polisi akiwa amesindikizwa na waandishi wa habari kama hamsini ambapo baada ya kufika pale walikutana na kamishna wa makosa ya jinai Tanzania Robert Manumba ambae ilibidi ahoji polisi Iringa kama ni kweli wanamtafuta Godwin na wenzake.
.
Namkariri Godwin akisema “baada ya kumuuliza mmoja kati ya maofisa wake kama ni kweli wanamtafuta Godwin ofisa huyo alijiumauma na baadae akasema hatumtafuti, baada ya hapo waandishi wa habari tulisimama tukaondoka kwa sababu ya kutokubaliana na kilichotaka kuendelea kuhusu taarifa ya uchunguzi ya Manumba”
Kingine kilichoendelea baada ya hapo ni Club ya waandishi wa habari Iringa kuziomba redio mbalimbali za iringa ambazo zimekua zikirusha matangazo ya polisi jamii kusimamisha matangazo hayo ambapo wamiliki wa vyombo hivyo wamekubali ombi.
Francis Godwin ambae alikua karibu na marehemu Daudi Mwangosi muda mfupi kabla ya kuuwawa kwa bomu amesema “Nilijua kwamba mimi ni miongoni mwa waandishi watatu wanaotafutwa kwa sababu marehemu kabla ya kifo akiwa amekamatwa nilitaka kwenda kumuokoa pale lakini nilipokua namsogelea Daudi akaniambia Godwin mdogo wangu kimbia… wakati nakimbia kama hatua 20 mbele nyuma nageuka nasikia mlipuko mkubwa, kuangalia ni Wangosi amekufa na nilibahatika kupiga baadhi ya picha ambapo askari waliokuwepo walipoona narudi kwenye eneo hilo walinionyeshea bunduki ikabidi ninyooshe mikono juu kwamba jamani mimi nakuja kwa heri wakaniambia potea”
Muda mfupi baada ya Marehemu Daudi kulipukiwa na bomu.
 
Godwin amesema baada ya kugeuka na kuanza kukimbia walianza kumfukuzia ila bahati nzuri gari yake ilikua mbali, baada ya kutishwa na polisi walipokwenda hospitali ulipopelekwa mwili wa marehemu ilibidi waanze kutoa mabango ya wanahabari yaliyobandikwa kwenye gari yao pamoja na kutoa namba za gari, alianza safari ya kuondoka lakini kuna gari zilikua zinamfukuzia kwa nyuma mpaka alipofika nje kidogo ya mji wa Iringa na kuingia mitaani ndio akafanikiwa kukimbia.
Kwenye sentensi ya mwisho Godwin anasema ameibiwa siri na askari mmoja ambae alimwambia kuhusu kutafutwa kwake yeye na waandishi wa habari awengine mbapo alimuonya kwamba msimamo na kauli aliokua ameutoa pamoja na ushahidi wa tukio la mauaji ndio vimefanya atafutwe

Kuuawa kwa Mwandishi Iringa: CCM yatoa Tamko Nakutaka Uchunguzi Usichukue Muda Mrefu




CCM imevitaka vyombo na tume zilizoundwa kuhusiana na kifo cha mwandishi wa habari Daudi Mwangosi, vichunguze kwa umakini na weledi mkubwa ili kubaini kila kitu ikiwemo chanzo cha vurugu zilizotokea na mazingira yaliyosabaisha kipigo hadi kufa mwandishi huyo.

Aidha imetaka uchunguzi usichukue muda mrefu ili ukweli kuhusiana na kadhia hiyo ujulikane mapema na hatua zichukuliwe kwa kila atakayebainika kuwa sababu au chanzo cha vurugu na kifo cha mwandishi huyo.


Aidha imesema imepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kifo hicho na kujeruhiwa kwa askari watatu wa Polisi wakati wa vurugu hizo na kimetoa pole kwa wafiwa, wanahabari wote nchini na wote walioguswa na msiba huo kwa namna moja au nyingine.


Hayo yamesemwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye katika taarifa ya CCM kwa vyombo vya habari, leo jijini hapa, kuhusiana na sakata la vurugu hadi kifo cha mwandishi huyo, juzi mkoani Iringa.


"Itakumbukwa tarehe Septemba 2, 2012 katika operesheni za CHADEMA mkoani Iringa kulitokea vurugu zilizosababisha kuuawa kwa mwandishi wa habari mzoefu, Daudi Mwangosi na kujeruhiwa vibaya kwa polisi watatu wa kikosi cha kutuliza ghasia.








JINSI KESI YA KAJALA ILIVYOONDELE HAPO JANA.


Kajala Masanja (pichani kushoto) na kulia akitoka mahakamani



SHAHIDI wa nne Monika Timber (41), amedai mahakamani katika kesi ya kula njama, kuhamisha umiliki wa nyumba na utakatishaji wa fedha inayomkabili msanii wa filamu nchini Kajala Masanja na mume wake Faraja Chambo kuwa nyumba hiyo ya washtakiwa iliuzwa wakati zuio lililotolewa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) bado muda wake haujamalizika.
Kadhalika, shahidi huyo ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kunduchi Salasala, amedai kuwa Takukuru walitoa zuio la nyumba hiyo kufanyiwa chochote ikiwamo kuuzwa hadi uchunguzi wa kesi ya utakatishaji fedha haramu inayomkabili mshtakiwa Chambo utakapomalizika.
Timber alitoa ushahidi wake leo mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo anayesikiliza kesi hiyo.
Akiongozwa na Mwendesha Mashtaka Takukuru, Leonard Swai shahidi huyo alidai kuwa taasisi hiyo ilitoa zuio la kwanza Julai 15, mwaka 2009 ikimtaka mmiliki kutofanya kitu chochote ndani ya miezi 6 kwa kuwa inafanyiwa uchunguzi.
Alidai kuwa baada ya muda wa zuio lile kumalizika, Takukuru waliwasilisha zuio la pili Februari 18, mwaka 2010 lakini kabla muda wake kumalizika nyumba iliuzwa.
"Nyumba ile ilipouzwa ofisi yangu haikuhusishwa na muuzaji wala mnunuaji ...nilihojiwa na Takukuru baada ya ile nyumba kuuzwa nikawaeleza sikuwa na taarifa kwa sababu zuio bado lilikuwa halijamalizika muda wake," alidai Timber.
Katika kesi hiyo, Kajala na Chambo, wanakabiliwa na shtaka la kula njama ya kuhamisha umiliki wa nyumba iliyoko Kunduchi Salasala jijini Dar es Salaam kinyume na kifungu cha 34 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007 wakijua ni kosa kwani tayari Mwanasheria Mkuu wa serikali alishazuia kuuzwa kwa nyumba hiyo.
Shtaka la pili, ilidaiwa kuwa Aprili 14, mwaka 2010 washtakiwa hao walihamisha isivyo halali umiliki wa nyumba hiyo kwenda kwa Emiliana Rwegarura huku wakijua imepatikana kwa njia ya rushwa kinyume na kifungu cha 34(2)A(3) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007.
Katika shtaka la tatu ilidaiwa kuwa siku na mahali hapo washitakiwa hao walitakatisha fedha huku wakijiua ni kinyume na sheria hiyo.
Washtakiwa walikana mashtaka yote kwa nyakati tofauti kutokana na mashtaka yanayowakabili kutokuwa na dhamana kisheria. Washtakiwa wako mahabusu mpaka kesi itakapotolewa uamuzi.

AY BALOZI MPYA WA AIRTEL



Meneja Mahusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa kumtambulisha AY (kushoto), makao makuu ya Airtel, Morocco, Dar es Salaam leo. Kulia ni Hawa Bayumi, Meneja Huduma za Jamii wa Airtel.


Meneja Mahusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (katikati) akimkabidhi simu AY (kushoto), makao makuu ya Airtel, Morocco, Dar es Salaam leo. Kulia ni Hawa Bayumi, Meneja Huduma za Jamii wa Airtel.
MWANAMUZIKI nyota Tanzania, Ambwene Yessayah ‘AY’ ameteuliwa kuwa Balozi wa Airtel, akimpokea Ally Kiba aliyekuwa balozi wa kampuni hiyo msimu uliopita.
 
Meneja Mahusiano wa Airtel, Jackson Mmbando amesema leo kwamba wameamua kumpa dili hiyo AY baada ya kuvutiwa na kazi zake kwa ujumla, akiwa msanii ambaye ametwaa tuzo kibao za kitaifa na kimataifa na kushirikiana na wanamuziki wengi wa kimataifa sambamba na kutumbuiza katika maonyesho makubwa hadi Ulaya na Amerika.
 
Kwa upande wake AY, alishukuru kwa dili hilo na kusema Airtel hawatajuta kwa kufanya naye kazi. Kwa kuanzia, AY alisema atafanyia kazi mradi wa kuchangia elimu ambao Airtel inashirikiana na BAMVITA.
 
Amewataka Watanzania kuchangia mradi huo kwa kutuma neno “Vitabu” kwenda namba 15626 na wataweza kuchangia Sh. 200 katika mradi huo au wengine kuchangia kwa Airtel Money kupitia namba 0788 041361.
 
AY pia alikabidhiwa simu aina ya Samsung Galaxy Tab7.0 Plus yenye thamani ya Sh. 1.200,000 na Mmbando, sambamba huduma zote ambazo zinalipiwa na Airtel.
 
Naye Meneja Huduma za Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi alisema wanampokea kwa furaha AY na wanaamini watashirikiana naye vema kufanya kazi za kijamii za kampuni hiyo.

PICHA ZA WATANZANIA WALIOFARIKI MGODINI LINDI

 

 


 

 WATU saba wamepoteza maisha baada ya kufukiwa na kifusi katika machimbo ya madini yaliyopo katika kata ya Nandagala wilayani ya Ruangwa mkoani Lindi.
 
Akizungumza na mwandishi wa habari hii Diwani wa kata hiyo, Andrew Chikongwe alisema kuwa kazi ya kufukua kifusi na kutoa miili ya marehemu hayo ilianza majira ya saa 9 alasiri hadi mapema asubuhi huku wakifanikiwa kupata miili yote.
 
Chikongwe alisema kuwa kazi hiyo ilikuwa ngumu kutokana na kuwepo kwa zana duni za uokoaji wakati wa kufukua mchanga na hatimaye kupata miili hiyo.
 
Diwani huyo aliwataja marehemu hao kuwa ni Nyang'ana Mkelecha mkazi wa Musoma, Mohamed Omari Fondogoro Mkazi wa Morogoro, Bakari Liganga mkazi wa Chunyu Ruangwa.
 
Wengine ni Rajab maarufu ROGER mkazi wa Musoma, Uwesu Bakari Abeid mkazi wa Rondo ,Chakoda mkazi wa Dar na Rashid Ally maarufu BADE mkazi wa Masasi mkoani Mtwara.

Minara ya mawasiliano ya simu yashambuliwa


                                                                 Ramani ya Nigeria


 Takriban Minara 24 ya kurushia mawasiliano ya simu za mkononi imevamiwa kote nchini Nigeria.

Msemaji wa jeshi ameripotiwa akilaumu kundi la wapiganaji la Boko Haram kwa uvamizi huo wa kwanza wa aina yake dhidi ya kampuni tisa za huduma za simu.
Kundi la Boko Haram limekuwa likilaumu kampuni hizo kwa kushirikiana na mashirika ya usalama kuwasaka wanachama wa kundi hilo.

Wataalamu wanasema kuwa uharibifu huo utagharimu kampuni hizo mamilioni ya dola.

Milio ya risasi na milipuko ilisikika huku moto mkubwa ukiteketeza minara hiyo Mjini Kano sawa na miji ya Maiduguri, Gombe na Bauchi.

Uvamizi mwingine ulitokea mjini Potiskum.
Msemaji wa jeshi mjini Maiduguri Luteni Kanali Sagir Musa, aliambia BBC kuwa maafisa wa usalama walishuku kundi la Boko Haram kwa uvamizi huo.

Kwa mujibu wa Luteni Kanali Musa, hii ni mbinu mpya ya mashambulizi ambayo imeanza kutumiwa na kundi hilo.

Siku ya Jumatano, kampuni tisa ziliripoti uharibifu uliofanyiwa minara yao 24. Duru zinaarifu kuwa baadhi ya kampuni zilizolengwa ni MTN ya Afrika Kusini pamoja na ile ya himaya ya nchi za kiarabu, Etisalat.

Boko Haram lilianza kufanya mashambulizi mwaka 2009 wakitaka sheria za kiisilamu kutumika, wakishambulia majengo ya serikali , makanisa na kuwaua wahubiri wa kiisilamu wenye msimamo wa kadri.

WACHIMBA MADINI WAACHIWA HURU RASMI.


                       Wachimba migodi waachiliwa


 Karibu wafanyakazi wote wa migodi ya madini nchini Afrika Kusini waliokamatwa katika vurugu za mwezi uliopita wameachiliwa.

Watu arobaini na wanne waliuawa katika vurugu hizo zilizowahusisha polisi na wafanyakazi wa migodi ya madini ya dhahabu ya Marikana.

Hatua hiyo imekuja wakati vyama vingi vya wafanyakazi wa migodi vimetiliana saini na kampuni ya migodi kumaliza mgomo ambao umeathiri kwa kiasi kikubwa sekta ya machimbo ya platinum.

Lakini makubaliano hayo hayakutiwa saini na chama muhimu kisichotambuliwa, ambacho ni kitovu cha mgogoro huo.

 Kutoka katika vilima kuzunguka mji wa Rustenberg unaweza kuona machimbo yaliyosambaa, yakiwa yamezungukwa na kambi za maskwota, ambamo wanaishi wafanyakazi wa migodi hiyo na familia zao.

Hapa ndipo inapotoka asilimia sabini na tano ya madini ya dhahabu nyeupe ijulikanayo kama platinum inayozalishwa duniani.

Chama chao cha Taifa cha Wafanyakazi wa Migodi, kinachotambuliwa kisheria, kinaonekana kuwa karibu karibu sana na kampuni iliyosajiliwa Uingereza ya Lonmin.

Pia kinaonekana kuwa karibu zaidi na Rais Jacob Zuma. Kwa hiyo wafanyakazi wameelekeza macho yao

kwa chama cha AMCU - chama ambacho hakitambuliwi na kampuni hiyo.

AMCU ilikuwa katika mazungumzo ya siku nzima hapo jana, yaliyosuluhishwa na makanisa na serikali.

Lakini makubaliano yalipofikiwa wajumbe wa chama hicho cha AMCU walitoka nje. Kitu walichotaka ni kuboresha malipo yao na hakuna la kujadili zaidi.

Malalamiko yao yamechukuliwa na Julius Malema, ambaye alifukuzwa kutoka chama cha ANC wakitafuta mahali pa kusimamia malalamiko yao.

Na vikundi vingine vya mrengo wa kushoto vinawaunga mkono wachimba migodi hao.Lakini bei ya madini ya platinum ambayo imekuwa ikianguka kwa asilimia ishirini kwa mwaka mmoja uliopita, kampuni hiyo inasema haina uwezo wa kuwalipa zaidi wafanyakazi wa migodi hiyo.

Thursday, September 6, 2012

MAN United yatangaza 33 kwa UEFA CHAMPIONZ LIGI!

Manchested United imetangaza Kikosi cha awali cha Wachezaji 33 kwa ajili ya Mashindano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
+++++++++++++++++++++++++

RATIBA za MAN UNITED KUNDI H:
Jumatano Septemba 19
Manchester United FC - Galatasaray A.S.

Jumanne Oktoba 2
CFR 1907 Cluj - Manchester United FC

Jumanne Oktoba 23
Manchester United FC - SC Braga

Jumatano Novemba 7
SC Braga - Manchester United FC

Jumanne Novemba 20
Galatasaray A.S. - Manchester United FC

Jumatano Desemba 5
Manchester United FC - CFR 1907 Cluj
+++++++++++++++++++++++++
Kikosi hicho kina Majina 25 kwa ajili ya Listi A na 8 kwa Listi B.

Kwa mujibu wa Kanuni za UEFA, Mchezaji anaweza kusajiliwa kwenye Listi B ikiwa amezaliwa Tarehe 1 Januari 1991 au baada ya hapo na amekuwa akiruhusiwa kuichezea Klabu husika kwa muda usio chini ya Miaka miwili mfululizo tangu atimize Miaka 15 wakati ambapo amesajiliwa na UEFA.

Pia Kanuni hiyo inasema kuwa Wachezaji ambao wametimiza Miaka 16 wanaweza kusajiliwa kwenye Listi B ikiwa katika Miaka miwili iliyopita wamechezea Klabu hiyo kwa Miaka miwili iliyopita mfululizo.

Wachezaji wa Listi B wanaweza kusajiliwa wakati wowote kabla ya Mechi husika.
Kwa Listi A, jumla ya Wachezaji wanaoruhusiwa kusajiliwa ni 25 na wawili kati yao wanatakiwa kuwa Makipa na si chini ya Wachezaji wanane wawe ‘wamekulia’ kwenye Klabu hiyo.

MAKIPA: David De Gea, Anders Lindegaard, Sam Johnstone*

MABEKI: Rafael, Patrice Evra, Phil Jones, Rio Ferdinand, Jonny Evans, Chris Smalling, Nemanja Vidic, Alexander Büttner, Marnick Vermijl*, Michael Keane*

VIUNGO: Antonio Valencia, Anderson, Ryan Giggs, Michael Carrick, Nani, Ashley Young, Paul Scholes, Tom Cleverley, Darren Fletcher, Nick Powell, Larnell Cole*, Jesse Lingard*, Ryan Tunnicliffe*

 MAFOWADI: Wayne Rooney, Javier Hernandez, Danny Welbeck, Robin van Persie, Shinji Kagawa, Federico Macheda*, Joshua King*

LISTI ya FIFA UBORA DUNIANI: Spain palepale, Bongo yashuka nafasi 4 ipo 132!


 >>>KUMI BORA, Ni Portugal pekee imepanda nafasi 1!!

>>>BRAZIL Wapanda 1, Wapo wa 12!!

Spain, ambao ndio Mabingwa wa Ulaya na Dunia, wameendelea kushika Nambari Wani kwenye Listi ya FIFA/Coca Cola ya Ubora Duniani iliyotolewa leo huku Tanzania ikiporomoka nafasi 4 na kushikilia Nambari 132 lakini kwenye Kumi Bora hamna mabadiliko yeyote isopokuwa Portugal kupanda nafasi moja na kushika nafasi ya 4 huku Uruguay ikishuka nafasi moja na kukamata ya 5.

Brazil, Mabingwa wa Dunia mara 5, wamepanda nafasi moja na sasa wapo nafasi ya 12.
Kwa Afrika, Timu ambayo iko juu kabisa ni Ivory Coast iliyobaki nafasi yake ile ile ya 16.
Listi nyingine mpya itatolewa Oktoba 3.

KUMI BORA:
[Kwenye Mabano nafasi za Mwezi uliopita]
1. (1) Spain
2. (2) Germany
3. (3) England
4. (5) Portugal
5. (4) Uruguay
6. (6) Italy
7. (7) Argentina
8. (8) Netherlands
9. (9) Croatia
10. (10) Denmark

ENGLAND: Mgao wa mapato toka TV UNARIDHISHA Klabu zote!!

Hivi karibuni ilikuwa almanusura La Liga isianze Msimu mpya baada ya baadhi ya Klabu kuja juu zikitaka mfumo wa Mapato yanayotokana na matangazo ya Mechi laivu kwenye TV urekebishwe ili kila Klabu ifaidike ipasavywo kama vile ilivyo huko England kwenye Ligi Kuu England, BPL [Barclays Premier League].
Huko England, kwenye Ligi Kuu, makubaliano ya sasa ya maonyesho ya Mechi laivu kwenye TV ni yale yaliyoanza tangu Mwaka 2010 na yatamalizika 2013 ambayo yatamwaga Pauni Bilioni 3.5 kwa kipindi hicho, ikiwa ni Pauni Bilioni 1.17 kwa Mwaka.
Mapato hayo hukatwa Fedha za matumizi kuendesha Ligi, fungu jingine hugawiwa Vyama tanzu kama vile PFA, Chama cha Wachezaji wa Kulipwa, LMA, Chama cha Mameneja wa Timu za Ligi, Vyama vinavyoendesha Ligi za Madaraja ya chini, kama vile Conference na Football League, Chama cha Marefa na pia kwenye Vyama vinavyotoa misaada kwa Jamii.
Lakini fungu kubwa la Mapato hayo ya TV huambuliwa na kugawiwa kwa Klabu 20 zilizomo kwenye Ligi Kuu England na pia Klabu ambazo zimeporomoka toka Ligi Kuu katika kipindi hicho cha Mkataba.
Mwishoni mwa Msimu wa 2011/12, Mgao ulikuwa ni jumla ya Pauni Bilioni 1.055.
Kati ya hizo, Pauni Milioni 968.2 ziligawanywa kwa Klabu 20 za Ligi Kuu za Msimu huo na zilizobaki zilipewa Klabu 7 zilizoporomoka kutoka Ligi Kuu.
MGAWANYO HUWA:
-Mapato yote yanayotoka nje ya England hugawanywa sawa sawa kwa kila Klabu na mgao huo ulikuwa £18,764,644 kwa kila Klabu.
-Mapato yanayozalishwa ndani ya England hugawanywa ifuatavyo:
=Asilimia 50 yake hugawanywa sawa kwa kila Klabu
=Asilimia 25 yake hugawanywa kwa kutegemea Klabu ilirushwa mara ngapi laivu
=Asilimia 25 hutegemea Klabu ilimaliza nafasi ipi kwenye Msimamo wa Ligi mwishoni
Ukiangalia ule Mgao wa Asilimia 25 inayotegemea nafasi ya Klabu utakuta Wolves, waliomaliza Ligi wakiwa mkiani ambayo ni nafasi ya 20, walipewa £755,062, Blackburn, waliokuwa nafasi ya 19, walipata mara mbili zaidi ya hizo na Bolton walipata mara 3 zaidi ya hizo kwa kumaliza nafasi ya 18 huku Timu iliyomaliza nafasi ya Kwanza, Manchester City, wakizoa mara 20 zaidi ya hizo, yaani £15,101,240.
Ukichukua Mapato ya Klabu ya Kwanza, Manchester City, utakuta walizoa Jumla ya £60,602,289 na Wolves, waliomaliza mwisho, walipata £39,084,461.
MGAO_WA_TV
Kitaalam, utaona Man City walipata Mgao mara 1.55 zaidi ya Wolves.
Huko Spain, kwenye La Liga, Real Madrid na Barcelona, huwa wanafanya Dili zao wenyewe na hawagawani na Klabu nyingine na wao hupata mara 14 zaidi ya Klabu nyingine.
Italy, kwenye Serie A, tofaitu ni mara 10 zaidi,.Ufaransa kwenye Ligi 1 ni mara 3 na nusu na Germany, kwenye Bundesliga, ni mara mbili.

MWILI WA MEREHEMU DAVID MWANGOTA WAZIKWA.

 Waandishi wa Habari wakiwa wamebeba Mwili wa Marehemu kuelekea Makabirini
Wakiwa wanafanya ibada ya Mwisho kabla ya kuanza maziko
Hapa wakiwa wanashusha mwili wa marehemu katika Nyumba yake ya milele
Mwili wa Marehemu Daudi Mwangosi ukiwa Tayari katika Kaburi
Shughuri za kuzika zimeanza
 Mazishi yanaendelea 
 Mke wa Marehemu Daudi Mwangosi akiweka Shada la Mauwa kwa machungu
 Mke wa Daudi Mwangosi akiwa analia kwa uchungu katika Kaburi la Marehemu Mumewe 
Watoto wa Marehemu wakiwawanaweka mashada ya maua sasa 
Ni ngumu sana Kuamini kwa mke wa Marehemu lakini hali ndivyo ilivyo kuwa akiwa na huzuni kubwa
 Dr Slaa akiweka Shada la Mauwa 
Dr Slaa Baada ya kumaliza kutoa heshima za mwisho
Mh. Mark Mwandosya akiweka Taji la maua pamoja na mke wake 
 Rais wa UTPC akiweka shada la Maua
 Ndugu wa Marehemu akiweka shada la Maua
Mwenyekiti wa Mbeya Press Club akiweka shada la maua 
Mwandishi Mkuu wa Mbeya  yetu, Ndugu Joseph Mwaisango akiwa anatoa heshima zake za Mwisho katiaka Kaburi
Wananchi wakiwa wanarejea baada ya mazishi

Waandishi wa Habari wakichukua Tukio Live `
Na huu Ndio Mwisho wa tukio zima la Mazishi ya Ndugu yetu, Mwanaharakati, Mpiganaji Daudi Mwangosi aliyekuwa Mwandishi wa Chanel 10.

BASI LAPINDUKA NA KUUA MMOJA MKOANI TABORA.


Na:Robert Kakwesi,Tabora


 Mtu mmoja amefariki dunia na wengine zaidi ya kumi kujeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupinduka wilayani uyui.
 

Akizungumza kwa niaba ya kamanda wa polisi mkoani Tabora,Anthony Ruta,Mrakibu mwandamizi wa polisi,John Kauga,amesema
 ajali hiyo imetokea eneo la kizengi wilayani uyui baada ya basi la kampuni ya Muro kupinduka.

Kauga amesema mwanamke mmoja amefariki duniua katika ajali hiyo ambaye bado    hajatambulika na mwili wake umehifadhiwa 
 chumba cha maiti cha hospitali ya mkoa,kitete.

majeruhi zaidi ya kumi wamelazwa katika Hospitali hiyo huku Daktari wa Mkoa,Leslie Mhina,akisema majeruhi wanazidfi kuongezeka.

akizungumzia chanzo cha ajali hiyo,mrakibu mwandamizi Kauga amesema ni baada ya dereva wa basi hilo lenye namba za usajili T 904 BWA
,Sihaba Mohamed kumuachia utingo wake ambaye jina lake halijapatikana kuendesha basi hilo na kusababisha ajali.

Amesema dereva na utingo wake wote wamekimbia baada ya ajali iliyotokea jana usiku jumanne majira ya saa tatu kasorobo na wanatafutwa.

Perez: Ronaldo does not want to leave Real Madrid



The Portuguese star refused to celebrate either of his two goals in Los Blancos' 3-0 victory over Granada on Sunday, saying he was 'sad' with a 'professional issue' at the club.

"If he wanted to leave he'd have said so when the transfer window was still open," the 65 year-old told Marca

"There are other reasons behind it."

Ronaldo himself took to Twitter to dispel rumors that his dismay was due to a desire for a new contract.

"That I am feeling sad and have expressed this sadness has created a huge stir," he wrote on the social networking site.

"I am accused of wanting more money, but one day it will be shown that this is not the case," he added.

Translate