KLABU ya Mtibwa Sugar leo Jumatano itaingia mzigoni kupambana na Jamhuri ya Zanzibar katika mchezo mkali wa nusu fainali ya michuano ya Super 8, huku Simba ikiivana Azam.
Michezo yote hiyo itapigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam huku ule wa Mtibwa ukitacheza saa nane mchana.
Mashabiki wanasubiri mchezo huu kwa hamu kubwa na wanaamini kuwa utakuwa maalum kwa ajili ya kulipa kisasi cha mabao 3-1 ambacho Simba ilipata kwenye robo fainali ya Kombe la Kagame.
Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja wa Mtibwa, David Gboya, alisema mechi hiyo itakuwa ngumu kutokana na kila timu kujiandaa vyema, ikiwa na lengo la kutwaa ubingwa.
Alisema timu yake itacheza kwa kujituma kama ilivyokuwa kwa mechi nyingine zilizopita, kwa kuwa wana kikosi bora na imara kutokana na usajili mzuri walioufanya.
“Sisi kama kawaida yetu tumejiandaa vizuri, kama unavyojua tunashindana ili tushinde, japokuwa kila timu iliyoingia kwenye michuano hii ina malengo ya kuhakikisha inatwaa ubingwa.
“Tunajivunia wachezaji wetu wapya na wa zamani kwa kuwa wamekuwa wakionyesha uwezo mkubwa kadiri siku zinavyosonga, nafikiri tutafanya vizuri na kuhakikisha tunazichukua sisi hizo milioni 40 anazopata bingwa,” alisema Gboya.

No comments:
Post a Comment