Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Bw. Zelothe Sephen.
MWANAFUNZI wa darasa la saba Shule ya Msingi Hogolo, wa umri wa miaka 14
(jina limehifadhiwa) ambaye ni Mkazi wa Mtaa wa Ikulu Kijiji cha Hogolo
wilayani Kongwa, mkoani Dodoma ameuawa kwa kunyongwa na kuzikwa kwenye
shimo nyuma ya nyumba yao karibu na choo baada ya kubakwa.
Uchunguzi
wa awali unaonesha kuwa chanzo cha mauaji hayo yaliyofanyika Jumamosi
iliyopita ni wivu wa kimapenzi kwani marehemu enzi za uhai wake,
anadaiwa alikuwa amevunja uhusiano na mpenzi wake wa muda mrefu, Heri
Aboubakar na kuanzisha uhusiano mpya na Wilfredy Muhaha maarufu Kabo.
Hata
hivyo bado haijafahamika muuaji halisi wa marehemu huyo licha ya polisi
kuwashikilia watu kadhaa kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo akiwemo
mpenzi wake wa sasa, Muhaha.
Mbali na Muhaha wengine wanaoshikiliwa
Polisi ni Ashad Jafari ambaye ni mkulima na mkazi wa Mtaa wa Nyerere
Hogolo ambaye ni rafiki wa marehemu na Rino Mazoea, mkulima na mkazi wa
Ikulu Hogolo wilayani Kongwa ambaye ni kaka wa marehemu.
Kamanda
Zelothe Steven alisema wanamtafuta Aboubakar ambaye amekimbia kijijini
hapo na hajulikani alipo mpaka sasa. Katika tukio hilo, kaka wa marehemu
ambaye pia anashikiliwa Polisi, katika maelezo yake ya awali alidai
kusikia purukushani zikitokea usiku wa tukio hilo la mauaji lakini
hakutoka usiku huo kushuhudia nini kinaendelea.
Marehemu alikuwa
akiishi na babu na bibi yake hapo kijijini na siku ya tukio , walezi
hao, walikuwa wameondoka kwenda katika vijiji vya jirani, ambapo bibi
yake alikuwa amekwenda Kongwa kwa ajili ya kujengea makaburi na babu
yake alikwenda Kijiji cha Banyi Banyi kutembelea wagonjwa.
mshuwa.blogspot.com
No comments:
Post a Comment