Wanajeshi wa Misri tayari kwa mashambulizi
Helikopta za kijeshi za Misri zimerusha makombora
kwa wapiganaji wanaoshukiwa kuwa wa kundi la kiislamu eno la rasi ya
sinai kaskazini mwa Misri.
Watu ishirini wameripotiwa kuuawa katika kijiji cha Touma wakati eneo la Sheikh Zuwaid nalo lilishambuliwa.
Mashambulizi hayo yamekuja baada ya vituo vya ukaguzi wa usalama kushukiwa kushambuliwa na watu wenye silaha katika mji wa al-Arish na kuwaua watu kadhaa.
Siku ya Jumapili wapiganaji waliwaua askari wa mpakani kumi na sita wa Misri katika eneo hilo.
Baada ya shambulio hilo zito dhidi ya vikosi vya Misri katika eneo la mpaka kuwahi kutokea kwa karne kadhaa, vikosi vya Israeli vilimesema viliwaua baadhi ya wapiganaji walioingia Israeli.
Waandishi wanaripoti kuwa, kumekuwa na ongezeko la majeshi kuzunguka eneo la al-Arish na mpaka wa Misri wa Rafar kuingia Gaza umefungwa moja kwa moja wakati vikosi vya ulinzi vikiwasaka washambuliaji waliosalia.
Hii ni mara ya kwanza kwa Misri kurusha makombora eneo la Sinai toka vita dhidi ya Israel mwaka 1973 ilipojaribu kuichukua rasi ya Sinai, maafisa wa usalama wameviambia vyombo vya habari.
Uwepo wa majeshi ya Misri eneo la Sinai kunahitaji idhini ya Israeli kwa mujibu wa makubaliano
No comments:
Post a Comment