Zitto Kabwe.
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe ameahidi kuwataja
wanaohusika kuficha mabilioni ya fedha nchini Uswisi katika kikao
kijacho cha Bunge Oktoba, mwaka huu iwapo Serikali itashindwa kufanya
hivyo hadi muda huo.
Wakati Zitto akisema hayo, kashfa hiyo
imechukua sura mpya na sasa fedha hizo zinahusishwa na ufisadi katika
Kampuni ya Meremeta.
Kauli ya Zitto ambaye pia ni Naibu Kiongozi
wa Upinzani Bungeni, imekuja siku chache tangu Waziri wa Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Samuel Sitta kuwataka wanaowafahamu walioficha fedha
hizo kuwataja hadharani ili iwe rahisi kwa Serikali kuwachukulia hatua.
Hata
hivyo, Zitto akizungumza na gazeti hili jana alisema: “Mimi ni mbunge
makini ninayefahamu taratibu za Bunge na kuheshimu haki za watu wengine,
siwezi kukurupuka katika suala hili.
Ninaiachia Serikali na vyombo
vyake iendelee kulifanyia kazi na ikiwa watashindwa kuwataja wahusika,
basi wasubiri kikao kijacho, nitaweka hadharani majina ya wahusika
wote.”
Zitto alisisitiza kuwa Serikali ina uwezo wa kupata taarifa
zozote inazozihitaji kutoka Uswisi na kwamba ndiyo maana ameipa muda wa
kulifanyia kazi suala hilo kabla yeye hajachukua hatua ya kuwataja
wahusika.
“Sikia, lazima tukubaliane jambo moja kwamba mimi siyo
Serikali, wala sina dola, ndiyo maana nasema kwamba tusubiri utekelezaji
wa ahadi ya Serikali, lakini wakishindwa kuwataja, basi mimi nitatumia
nafasi yangu kama mbunge kuwataja na nitafanya hivyo ndani ya Bunge na
wala siyo nje ya hapo,” alisema.
Uchunguzi zaidi wa gazeti hili
umebaini kuwa kiasi cha Dola za Marekani 186 milioni (takriban Sh300
bilioni) kwa viwango vya sasa vya kubadilishia fedha ambavyo ni Sh1,600
kwa Dola ya Marekani, kimefichwa katika benki tatu tofauti za Uswisi.
Uchunguzi
zaidi unabainisha kuwa takwimu hizo ni rasmi kwani zimetolewa na Benki
Kuu ya Uswisi, lakini taarifa zaidi zinadai kuwa kuna fedha nyingi zaidi
zilizofichwa na Watanzania katika benki nyingine nchini humo ambazo
taarifa zake zinaweza kupatikana ikiwa Serikali itasimamia vizuri suala
hilo.
Watanzania 27 wameripotiwa kumiliki fedha nchini humo, na
mmoja wao anadaiwa kwamba anamiliki Dola za Marekani 56 milioni (wastani
wa Sh89.6 bilioni).
Kashfa ya kuwapo kwa vigogo walioficha fedha
zao Uswisi iliibuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini Juni mwaka
huu na baadaye mwangwi wake kulitikisa Bunge katika Mkutano wake wa Nane
uliomalizika hivi karibuni.
Habari hizo zilikuwa zikinukuu
taarifa ya Benki Kuu ya Uswisi iliyoitoa na kuonyesha kuwapo kwa kiasi
cha Sh315.5 bilioni zilizotoroshwa Tanzania na kufichwa nchini humo na
vigogo ambao ni wanasiasa pamoja na wafanyabiashara.
Suala hilo
pia lilijadiliwa katika kikao cha Bunge kilichopita, huku ikidaiwa
kwamba fedha hizo zinatokana na biashara (deals) zilizofanywa na
watendaji wa Serikali na wafanyabiashara kwenye sekta za nishati na
madini na kwamba sehemu kubwa ya fedha zililipwa na kampuni za utafutaji
mafuta na gesi katika Pwani ya Mkoa wa Mtwara zilizopewa mikataba kati
ya mwaka 2004 na 2006.
Uhusiano na Meremeta
Habari zaidi zinadai kuwa fedha zilizofichwa Uswisi hivi sasa zina uhusiano na ufisadi kupitia Meremeta unaohusisha kiasi cha Dola za Marekani 132 milioni wastani wa Sh211.2 bilioni ambazo zilitoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwenda Benki ya Ned Afrika Kusini.
Uhusiano na Meremeta
Habari zaidi zinadai kuwa fedha zilizofichwa Uswisi hivi sasa zina uhusiano na ufisadi kupitia Meremeta unaohusisha kiasi cha Dola za Marekani 132 milioni wastani wa Sh211.2 bilioni ambazo zilitoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwenda Benki ya Ned Afrika Kusini.
Fedha hizo zililipwa
kama marejesho ya mkopo wa Dola 10 milioni (sawa na Sh1.6 bilioni tu,
uliokuwa umechukuliwa na Kampuni ya Meremeta Ltd ambayo ilikuwa mali ya
Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ikishughulikia uchimbaji wa madini.
Utata
katika malipo hayo ni uhalali wa ongezeko la Dola 122 milioni katika
malipo hayo, kwani mkopo wa Dola za Marekani 10 milioni ulirejeshwa na
faida ya zaidi ya asilimia 1,000.
Uchunguzi unaonyesha kuwa fedha hizo za marejesho tata zilifichwa katika benki moja (jina tunalihifadhi) nchini Mauritius, na baadaye kati ya 2005 na 2006 zilihamishiwa nchini Uswisi, ambako sehemu yake zipo kwenye akaunti ya kigogo ambayo inaongoza kwa kuwa na kiasi kikubwa cha fedha, karibu Sh90 bilioni.
Uchunguzi unaonyesha kuwa fedha hizo za marejesho tata zilifichwa katika benki moja (jina tunalihifadhi) nchini Mauritius, na baadaye kati ya 2005 na 2006 zilihamishiwa nchini Uswisi, ambako sehemu yake zipo kwenye akaunti ya kigogo ambayo inaongoza kwa kuwa na kiasi kikubwa cha fedha, karibu Sh90 bilioni.
Kashfa ya Meremeta ni ya muda mrefu na mara nyingi
Serikali imekuwa ikikataa kuizungumzia kwa maelezo kwamba ni suala
ambalo lina masilahi ya usalama kwa taifa.
Awali, Serikali ilisema
kwamba Meremeta Ltd ni kampuni ya Kitanzania iliyokuwa ikimilikiwa na
JWTZ kwa ajili ya mradi wake wa Nyumbu, Mkoa wa Pwani.
Taarifa za
usajili zilizotolewa na Msajili wa Kampuni wa Uingereza na Wales
zinabainisha kuwa kampuni hiyo iliandikishwa nchini humo mwaka 1997 na
baadaye ilifilisiwa hukohuko Uingereza mwaka 2006.
Taarifa ya
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) ya Mei 31, 2005
inabainisha kwamba Meremeta Ltd ni tawi la kampuni ya kigeni
iliyosajiliwa Tanzania, Oktoba 3, 1997 na kwamba hisa 50 za kampuni hiyo
zilikuwa zinamilikiwa na Kampuni ya Triennex (Pty) Ltd. ya Afrika
Kusini, wakati hisa 50 zilizobaki zilikuwa zinamilikiwa na Serikali ya
Tanzania.
Utata kuhusu umiliki wa Meremeta Ltd unatokana na
taarifa ya Brela ambayo pia inazitambua kampuni mbili za Kiingereza
ambazo ni London Law Services Ltd na London Law Secretarial Ltd kuwa
wamiliki wa hisa moja kila moja ndani ya Meremeta.
Licha ya
Serikali kutokuwa mmiliki pekee wa kampuni hiyo, BoT ililipa madeni yote
ya Meremeta badala ya kusaidiana na washirika wake ambao kisheria
wanaonekana kuwa walikuwa wakimiliki hisa katika kampuni hiyo.
Serikali
Tanzania ilikuwa ikimiliki asilimia 50 ya hisa na kwa mujibu wa taarifa
za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), uhalali wa
malipo hayo ulikuwa na walakini kwani kiutaratibu, Nedbank Ltd ilitakiwa
iachwe idai fedha zake kutoka kwa mfilisi wa kampuni hiyo kama ilivyo
kwa wadeni wengine.
Meremeta bungeni
Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini iliwahi kupewa idhini ya kuchunguza suala hilo, lakini Spika wa Bunge, Anne Makinda alilihamishia katika Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.
Meremeta bungeni
Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini iliwahi kupewa idhini ya kuchunguza suala hilo, lakini Spika wa Bunge, Anne Makinda alilihamishia katika Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.
Hata hivyo, uchunguzi huo
haukuwahi kufanyika na Ofisi ya Spika pia haijawahi kutoa taarifa
yoyote. Hivyo suala hilo kubaki kitendawili hadi leo.
Hatua ya
Spika kuridhia uchunguzi ilikuja baada ya mvutano wa muda mrefu,
uliotokana na hoja zilizokuwa zikitolewa na Serikali kwamba suala la
Meremeta lisingeweza kufanyiwa uchunguzi kutokana na “sababu za
kiusalama.”
Kumbukumbu za Bunge zinaonyesha kuwa Zitto aliwahi
kuwasilisha barua kwa Katibu wa Bunge akitoa taarifa ya hoja ya kutaka
kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge kwa ajili ya kuchunguza tuhuma za
ufisadi kupitia kampuni hiyo ya uchimbaji wa dhahabu.
Zitto alitoa
taarifa ya mdomo bungeni Julai 13, mwaka jana kwa mujibu wa Kanuni ya
Bunge Namba 117 (2)-(a) inayomruhusu kutoa taarifa ya kusudio lake la
kuwasilisha hoja ya kutaka Bunge liunde kamati teule.
Aliyekuwa
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi (sasa
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii) aliwahi kusema bungeni kwamba
halifahamu suala hilo kwenye majumuisho ya Bajeti ya wizara hiyo ya
2011/12.
No comments:
Post a Comment