Mbuyu Twite.
KLABU
ya Simba kupitia kwa mwenyekiti wake, Ismail Aden Rage imeweka wazi
kuwa haijalipwa fedha za usajili ambazo ilimpatia beki Mbuyu Twite,
ambapo imesisitiza kuwa iwe isiwe lazima walipwe fedha zao walizompa
mchezaji huyo ikishindikana watafuata sheria zote ikiwemo kumfikisha
mahakamani.
Rage amesema kuwa watafuata sheria zote za soka ambapo
kuonyesha wamepania kufanya hivyo tayari wameshawakilisha pingamizi la
mchezaji huyo kuichezea Yanga kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
kisha ikishindikana wataenda katika mahakama za kiraia licha ya kuwa
Shirikisho la Soka la Fifa haliruhusu masula ya soka kupelekwa huko.
“Tujafahamu
kuwa Fifa hairuhusu masuala ya soka kupelekwa katika mahakama za
kawaida, lakini alichokifanya Mbuyu ni criminal case, kwani alichukua
fedha zetu kwa ajili ya kufanya kazi na sisi lakini hakufanya hivyo.
“Wao
wanasema eti alikuwa na mkataba wa Lupopo, ulishaona wapi mkataba wa
miaka sita! Nimefurahi Championi mmeeleza ukweli juu ya kila kitu
kilivyokuwa kuwa, ni kweli tulimpa dola 30,000, lakini atatakiwa
kutulipa jumla ya dola 39,500, zikiwemo za usumbufu na nauli
tuliyompatia wakati anasaini mkataba wetu.
“Yanga hawajafanya haki
katika hili, hatutakubali, wasipoturudishia fedha zetu akifika nchini
tunamfikisha kwenye vyombo vya sheria, hatutakubali. Wawaulize TP
Mazembe, nilisema nimewashika pabaya na kweli ilikuwa hivyo.
“Hivyo katika hili, Yanga nimewashika pabaya na wasilete ujanjaujanja,” alisema Rage.
No comments:
Post a Comment