UNAWEZA
usiamini lakini ukweli ni kuwa Juma Ali (48), mkazi wa Mtoni jijini Dar
es Salaam amedai kwamba mkewe, Hadija Chande (40) (pichani) amemchezea
kishirikina, hivyo kujikuta hana nyeti ya kiume.
Taarifa kutoka
katika vyanzo vyetu vya habari zimedai kwamba Ali kwa sasa hana uwezo wa
kufanya tendo la ndoa kwa kuwa nyeti yake imetoweka kimiujiza na
shutuma zote anambebesha mkewe kwamba ndiye aliyefanya ‘mchezo’ huo.
Habari zinadai kuwa kutokana na hilo, kumezuka mgogoro mkubwa kati ya
wanandoa hao kwani mume amekuwa akimdai mkewe arejeshe nyeti yake,
jambo ambalo halijawezekana.
Imedaiwa kuwa Hadija, mara baada ya
kufunga ndoa na Ali mwaka 1996 alikuwa na wivu wa kupindukia, hivyo
kuamua kutafuta dawa na kumfanyia mumewe ili ndoa yao izidi kuimarika
lakini mara baada ya kutenda alichoambiwa afanye kama dawa, nyeti
ilitoweka na kubaki na ‘kipande’ kidogo cha kusaidia kutoa haja ndogo.
“Kutokana na madai ya Ali, mkewe aliamua kufungasha virago na kutoweka
nyumbani na kwenda kusikojulikana wakati mumewe yupo kazini,” kilisema
chanzo.
Gazeti hili baada ya kusikia habari hizo za kushangaza,
lilimtafuta Ali ambaye baada ya kuulizwa kuhusu mkasa huo alititirisha
maneno kama ifuatavyo:
“Ni kweli hayo uliyoambiwa. Kwa sasa
ninachomdai mke wangu aliyetoweka ni nyeti yangu, naomba anirudishie
kwani ufumbuzi wa mgogoro wetu hauwezi kupatikana kamwe kama
hatazirudisha.
“Hapa unaponiona ndugu mwandishi mimi siyo mwanaume
tena. Sina ‘kitu’, hapa kimebaki ‘ kipande’ kama kalamu ambayo haifanyi
kazi yoyote. Mke wangu nilipomuoa alinikuta nina watoto sita niliozaa na
mke niliyemuacha mwaka 1994, sasa hivi siwezi kufanya tendo la ndoa.
“Mgogoro wa kutoweka na nyeti yangu ulianzia mke wangu alipoanza
kunilalamikia kuwa natembea nje ya ndoa na akaniahidi kuwa ni lazima
atanidhibiti. Madai yake niliyapinga lakini nguo zangu za ndani zikaanza
kupotea. Nilipomuuliza alisema angeninunulia nyingine, nilikuwa na
mashaka naye, nikamuomba anirudishie lakini hakufanya hivyo.
“Mara
tu chupi zangu zilipoanza kupotea, nikawa sisikii hamu ya tendo la ndoa.
Mwezi uliopita, nyeti yangu ikawa imetoweka, nilipomuuliza akawa mbogo.
Ilipofika Julai 28, mwaka huu, saa sita mchana, nilitoka kazini na
kurudi nyumbani lakini sikumkuta mke wangu na nguo zangu za ndani na
soksi hazikuwepo pia.
“Licha ya nguo, picha zangu nazo alizichukua
na nilipomuuliza mtoto wangu Karim akasema mama yao amesema kabeba vitu
vyake vyote ndani ya nyumba na hakumuambia anakokwenda.
“Nilikaa
siku tatu, nikaamua kwenda serikali ya mtaa wetu ya Mtoni na
wakanishauri nikaripoti polisi ambako nilipokwenda walifungua jalada
namba namba MTG/RB/2054/2012. Polisi waliniambia nitakapomuona popote
niwaarifu ili wamkamate.
“Nilisafiri kwenda mikoani na niliporudi
nilikuta barua kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) wilayani
Temeke ikinitaka niende katika ofisi zao kwa kuwa mke wangu kafungua
shauri la kutaka talaka, jambo nililogundua kuwa alishauriwa na rafiki
zake ili nimpe nyumba.
“Najua kilichomtoa mke wangu nyumbani ni
kushindwa kunirejeshea nyeti yangu, hapa ameshaniua hivyo siyo rahisi
kwake kurudi kwani hatafurahia tendo la ndoa. Ili kesi hii iishe sharti
ni moja tu kwamba anirudishie nyeti yangu,” alisema Ali.
Mke wa Ali, Hadija alipohojiwa kuhusu sakata hilo alikuwa na haya ya kusema:
“Mbona na mimi sizai na sina hata mtoto wa dawa? Kuhusu kwamba
nimetoweka na nyeti yake ni kwamba mimi sijui mambo hayo,
asinifuatefuate.”
Mjomba wa Hadija, Abdalah Chande alipoulizwa
kuhusu sakata hilo, alikiri kuelezwa na Ali kuhusu mgogoro huo na kudai
kuwa alimzushia kuwa yeye ndiye anayemharibu mpwae (Hadija) na akampiga
marufuku kukanyaga nyumbani kwake, akaahidi kushirikiana na baba yake
mdogo kutatua tatizo hilo.
Baba mdogo wa Hadija aliyejitambulisha
kwa jina moja la Juma alipoulizwa kuhusu mgogoro huo alisema hautambui
lakini alimlaumu mwanaye huyo kwa kupeleka shauri hilo Bakwata kabla ya
kulifikisha kwake.
No comments:
Post a Comment