Mkurugenzi wa Mad Mad Entertainment,
Yasmin Razak (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam jana kuhusu kampuni yake kuingia mikataba na wasanii wa filamu
wa Tanzania watakaokwenda Nigeria na Jmahuri ya Kidemokrasia ya Kongo
(DRC) kwa ajili ya kutengeza filamu. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Superior, Issack Kasanga na Rais wa Shirikisho la Filamu
Tanzania, Simon Mwakifamba.
Msanii wa filamu, Steve Nyerere
(kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano hupo.Kushoto ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Superior, Issack Kasanga na Rais wa Shirikisho la
Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba.
DAR ES SALAAM, Tanzania
KAMPUNI ya Mad Mad Entertainment
iliyopo jijini London nchini Uingereza, imeanzisha program maalum ya
kupeleka wasanii wa filamu za bongo nje ya nchi kwa lengo la kukuza
sanaa hiyo hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Yasmin
Razak alisema ameamua kufanya kazi na wasanii hao ili kuleta mabadiliko
na kuwakwamua kiuchumi wasanii wa filamu hapa nchini.
“Kwa muda mrefu niliokaa London sioni
kama sanaa hii ina maendeleo, nikafikiria kitu gani nifanye ili kukuza
tasnia hii, katika mkataba na kampuni msanii atakayetengeneza filamu na
wasanii wa nje atalipwa kiasi cha sh 50 milioni pamoja na malipo
mengine yatakayokuwepo kwenye mkataba, ikiwa ni pamoja na asilimia
fulani kwa kila kazi itakayouzwa hapa nchini.
“Nimekuwa nikifanya kazi hiyo na wasanii wengi kutoka Nigeria wakiwemo kina Omotola, Two Face na wengineo na pia Ghana, Congo na hata Uingereza, hivyo nimeonelea kuwa itakuwa vema Tanzania nao kuingia katika mchakato huo,”alisema Razak.
Razak ambaye amewahi kufanya kazi ya filamu na Fally Ipupa, alitaja vigezo vya msanii atakayechaguliwa ikiwa ni pamoja na umaarufu, kuijua lugha ya kiingereza, uwezo wa kuigiza na kuuvaa uhusika wowote pamoja na mavazi.
Naye rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba aliwataka wasanii hao kujipanga katika kuhakikisha wanaingia kwenye ushindani huo na kuwataka wale watakaochaguliwa kujituma na kuonyesha nidhamu ya uhakika.
“Hapa kuna kuinua vipaji, soko la kimataifa na mengineyo, hivyo ni vema kufanya kazi kikamilifu kwa wale watakaochaguliwa na si kujisahau, wanatakiwa wasanii watatu na tupo katika hatua za awali za mchujo,” alisema
Mwakifamba.
No comments:
Post a Comment