tangazo

Saturday, March 30, 2013

AKAMU WA RAIS DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL AFIKA KUJIONEA JENGO LA GHOROFA 16 LILILOPOROMOKA JIJINI DAR JANA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia Jengo la Ghorofa 16, lililoporomoka lenyewe leo asubuhi katika Mtaa wa Indra Ghand na Zanaki. Makamu amefika kushuhudia Shughuli za uokoaji ambazo zinaendelea, ambapo hadi sasa idadi ya watu waliofariki imeelezwa kuwa imefikia watatu na waliookolewa wakiwa hai ni 17, kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum, Suleiman Kova.
 Uokoaji ukiendelea.....
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiondoka eneo la tukio baada ya kuangalia Jengo la Ghorofa 16, lililoporomoka lenyewe leo asubuhi katika Mtaa wa Indra Ghand na Zanaki. Makamu amefika kushuhudia Shughuli za uokoaji ambazo zinaendelea, ambapo hadi sasa idadi ya watu waliofariki imeelezwa kuwa imefikia watatu na waliookolewa wakiwa hai ni 17, kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum, Suleiman Kova.
Askari Jeshi wakikokota Jenereta kubwa kusogeza eneo la tukio ili kuhakikisha mwanga unapatikana kurahisisha shughuli za uokoaji hadi usiku, baada ya giza kuingia.

No comments:

Translate