Gari
ambayo imepata ajali na kuua wachezaji watatu wa klabu ya DC Motema Pembe ya
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo jana Ijumaa, likiwa nyang'anyang'a baada ya
kugongana na lori.
KINSHASA, DR Congo
Mlinda mlango Guelor Dibulana na
washambuliaji Hugues Muyenge na Mozart Mwanza walikuwa wakirejea nyumbani baada
ya ibada ya Ijumaa Kuu kwenye Kanisa la Saint-Dominique jijini hapa, kisha gari
walilokuwamo kugongana na lori
WACHEZAJI watatu wa klabu ya soka ya
DC Motema Pembe (DCMP) ya hapa wamefariki dunia kwa ajali ya gari iliyotokea
jana Ijumaa jijini hapa, mamlaka za kipolisi zimeeleza.
Mlinda mlango wa kimataifa Guelor
Dibulana, washambuliaji Hugues Muyenge na Mozart Mwanza walikuwa wakirejea
nyumbani baada ya ibada ya Ijumaa Kuu kwenye kanisa la Saint-Dominique jijini
hapa, kisha gari walilokuwamo kugongana na lori.
Mchezaji mwenzao aliyetambulika kwa
jina moja la Mbindi, ambaye alikuwa dereva wa gari hiyo yu mahututi, pamoja na
abiria mwingine mmoja ambaye hakutambulika, lakini wote wana majeraha makubwa
na hali zao ni mbaya.
DCMP ilikuwa inajiandaa na pambano
la leo Jumapili ya Pasaka dhidi ya AS Vita Club katika mechi ya tatu ya
Linafoot – ligi ya daraja la juu zaidi DR Congo na ilitarajiwa jana Jumamosi
mamlaka husika zingebadili ratiba hiyo.
Uongozi wa juu wa klabu hiyo
ulikataa kujibu maswali kutoka SuperSports.com, ukidai ilikuwa ni mapema mno
kwa wao kutoa maelezo kuhusiana na ajali hiyo pamoja na vifo vya wanandinga
wake. Mungu aziweke roho za marehemu mahala pema peponi. Ameen.
SuperSport.com
No comments:
Post a Comment