Takriban watu watatu wamethibitishwa kufariki baada ya jengo lenye ghorofa zaidi ya kumi kuporomoka mjini Dar es Salaam, Tanzania.Waokozi wanaendelea na shughuli ya kuwatafuta na kuwaokoa manusura na wanasema kuwa hadi sasa watu kumi na watatu waliokuwa wamenaswa wameokolewa.
Zaidi ya wengine arobaini wangali wamenaswa chini ya vifusi.Shughuli ya ujenzi ilikuwa inaendelea kwenye jengo hilo wakati lilipoporomoka katikati mwa mji wa Dar es Salaam.Miongoni mwa watu ambao wangali kupatikana ni wafanyakazi wa mjengo na watoto kutoka shule jirani ya mafunzo ya dini ya kiisilamu.Kulingana na walioshuhudia ajali hiyo, watu walisikika wakipiga mayowe kutaka msaada."nilidhani lilikuwa tetemeko la ardhi, na kisha nikasikia mayowe,'' alisema shahidi mmoja.Jengo hilo liko katikati mwa Dar es Salaam na liliporomoka saa tatu kasorobo asubuhi kwa saa za Afrika mashariki.Mamia ya watu wanaaminika kuwa ndani ya jengo hilo huku wengine wakiwa nje wakati wa ajali hiyo . Hata hivyo idadi kamili ya watu hao bado haujulikani.
No comments:
Post a Comment