Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, na Naibu Waziri wa
Kilimo Chakula na Ushirika, Adam Malima, wakizungumza nje ya ukumbi wa
Karimjee, baada ya kushiriki shughuli ya kuaga mwili wa marehemu,Salim
Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba
kupitia Chama cha CUF, aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri Mstaafu,
Edward Lowasa, na viongozi wengine wakishiriki shughuli ya kuaga mwili
wa marehemu Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani
Visiwani Pemba kupitia CUF, aliyefariki jana mchana katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili. Shughuli za kuaga mwili wa marehemu zimefanyika kwenye
Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Machi 29, 2013.
Rais Jakaya Kikwete, akiweka saini
katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la
Chambani CUF, Salim Hemed Khamis, aliyefariki dunia jana katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa baada ya kuuguaa ghafla
wakati akiwa katika Kikao cha Kamati ya Bunge cha Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa katika Ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es
Salaam juzi. Marehemu mefariki kwa ugonjwa wa shinikizo la damu.
No comments:
Post a Comment