Jeshi la polisi Zanzibar limefanikiwa kumkamata mtu anaedaiwa
kuhusika na mauwaji ya Padri wa kanisa Katoliki Evarest Mushi yaliotokea
mapema mwaka huu.
Akizungumza na wandishi wa habari kamishna wa jeshi la polisi
Zanzibar Mussa Ali Mussa amesema mtuhumiwa huyo Omar Mussa Makame mkaazi
wa Mwanakwerekwe ametambuliwa na watu walioshudia tukio hilo lilitokea
katika maeneo ya Bububu.
Amesema baada ya kuchora michoro ya sura ya mtu aliehusika na tukio
hilo kwa kutumia watu walioshuhudia na kuitoa kwenye vyombo vya ulinzi,
wananchi na mitandao ya kijamii mhalifu huyo ametambuliwa.
Kamishna Mussa amesema mwananchi aliesaidia kutambuliwa kwa mtu huyo
atazawadiwa shilingi milioni 10 kufuatia jeshi la polisi kuahidi kutowa
zawadi ya kiwango hicho cha fedha.
Hata hivyo amesema kwa usalama wa mtu aliesaidia kukamatwa kwa
mhalifu huyo na sababu za kiupelelezi tukio la kuimkabidhi fedha hizo
litafanyika kwa njia za siri
Aidha Kamishna Mussa amewataka wananchi kuendelea
kutoa ushirikiano wa hali ya juu ili kufanikisha upelelezi wa matukio
mengine yaliopita ikiwemo kujeruhiwa kwa viongozi wa kidini.
Amesema jeshi la polisi litaendelea kutunza siri zap watu watakaotoa taarifa hizo.
No comments:
Post a Comment