tangazo

Monday, November 26, 2012

Dereva anayeugua saratani kwa kubebeshwa Uranium bila kufahamu

NOVEMBA 6, 2011, siku mbili kabla ya uchaguzi wa Urais nchini Kongo ni siku ambayo Shabani Ally hatoweza kuisahau.
Kama ilivyo ada ya shughuli zake za udereva, Shabani alikwenda nchini Kongo, mjini Lubumbashi kupeleka mzigo. Alipofika huko alitakiwa kupakia mzigo mwingine wa kurudi nao Dar es Salaam.
Walipofika sehemu ya ukaguzi katika eneo la Kisanga, jimbo la Katanga, gari lake lilikamatwa  na baada ya mzigo kuchunguzwa ilibainika kuwa gari limebeba madini yenye mionzi mikali.
Gari hilo, lenye namba za usajili T506BFK, namba ya trela T161ASM na  conteina namba CRXU933671/4 lilikamatwa na kupelekwa katika kituo cha ukaguzi wa madini nje kidogo ya mji wa Lubumbashi.
Shabani  Mkazi wa wilaya ya Temeke, mtaa wa Sandali anasema baada ya wataalamu wa madini kulifanyia uchunguzi gari hilo, walibaini kuwa limebeba madini ya Uranium ambayo yanatajwa kuwa yana mionzi mikali.
Anaitaja kampuni ya Somika ya Kongo kuwa ndiyo iliyoupakia mzigo huo kuuleta Tanzania, ambapo badaye ungesafirishwa na kupelekwa China kwa kutumia meli.
“Nilikuwa nikisaidia kuupanga mzigo ule katika conteina bila kujua ni nini ninachopakia. Kwani karatasi ya maelezo ilionyesha kuwa ninapakia mzigo wa madini ya Ndandash, kumbe hayakuwa madini ya Ndandash pekee bali yalichanganywa na Uranium,” anasema Shabani
 Ilibainika kuwa kampuni ya Somika ilitoa zabuni ya mzigo wa tani 26 na kumbe kati ya tani hizo, 22 zilikuwa ni madini ya uranium na nne tu, ndizo zilikuwa za madini ya Ndandash.
Anasema  magari madogo ya kupakia mizigo ‘focal  lift’ yalikuwa yakiingiza mzigo ndani ya conteina na yeye akisaidia kuipanga hivyo alikuwa akiyashika na kuyakanyaga kabisa madini hayo yenye asili ya mchangamchanga.
Kwa kuwa uchaguzi nchini Kongo ulikuwa katika kilele, Shabani  baada ya kukamatwa alitakiwa kusubiri hadi matokeo yatangazwe ndipo apewe kibali cha kuendelea na safari.
“Ilibidi kampuni ya madini iturudishe hadi katika kampuni ya Somika. Tulipakua mzigo wa madini yote na tukapewa mzigo mwingine ili turudi nao Tanzania,” anasema Shabani
Shabani anasema  akiwa njiani kurudi Tanzania alianza kusikia maumivu makali ya mguu wa kushoto, hata hivyo, aliyapuuzia akijua ni maumivu ya kawaida.
Alipofika Tanzania aliendelea na shughuli zake za udereva na safari hii alipangiwa kwenda Lusaka, Zambia.
“Nikiwa njiani kuelekea Lusaka, kabla hata ya kufika Tunduma nilianza kuumwa. Mguu uliniuma mno na ikabidi niwapigie simu ofisini ili waniletee dereva mwingine,” anasema
 Ilibidi Shabani arudi Dar es Salaam ambapo ofisi yake ilimpa fedha za matibabu na kuanza kufanyiwa uchunguzi.
Anasimulia na kusema  alikutana na Dk Waane katika hospitali ya Burhani, ambaye baada ya kumpima alimshauri ahamie Muhimbili kwa matibabu zaidi kwani tatizo lake linaonekana kuwa kubwa.
“Ilibidi niusikilize ushauri wa Dk Waane,nilikwenda Muhimbili, vipimo vikachukuliwa na majibu yalipotoka yalionyesha kuwa  chembe hai nyeupe za damu zimeongezeka katika kiwango kisicho cha kawaida,” anasema
Cheti cha Shabani kinaonyesha kuwa  chembe hai nyeupe za damu zimeongezeka na kufikia 101 na hata alipokwenda kupima baada ya wiki moja zilionekana kupanda na kufikia 193.
Balaa halikukomea hapo, mapema mwezi Aprili, Shabani alikwenda hospitali baada ya kusikia maumivu makali ya tumbo.
Alipofanyiwa uchunguzi aliambiwa kuwa bandama yake imeongezeka ukubwa kwa kitaalamu  alikuwa amepata maradhi ya ‘splenomegally.’
Mwajiri wake
Mwajiri wa Shabani, aliyefahamika kwa jina la Frank alipopigiwa simu alikataa kuzungumza lolote akidai kuwa amekwishazungumza na shabani na kuyasuluhisha
Shabani, anadai kuwa  Ruvu Transport Limited ilikuwa ikimsaidia kwa fedha za matibabu.
Hata hivyo kwa maelezo ya Shabani, kasi ya huduma hiyo iliendelea kupungua siku hadi siku  na siku moja walimwita na kumtaka asaini barua ya kuacha kazi.
“Waliniita na kuniambia kuwa nitie saini barua ya kuacha kazi na kunipa mshahara wa miezi minne jambo ambalo mimi sikuliafiki. Sikuliafiki kwa sababu  hayo hayakuwa makubaliano yetu,”anasema
Katika mgogoro huo Shabani anasema alikumbana na kauli za kukatisha tamaa kutoka kwa mwajiri wake ambazo zilionyesha kuwa ‘wamemchoka’
“ Wakati mwingine walisema mimi ni mzigo, napenda kubebwa na maneno mengine mengi,’ anasema
Anasema  aliwaeleza kuwa amepata madhara hayo akiwa kazini hivyo anahitaji msaada wao lakini hawakuwa tayari kumsaidia.
Aidha shabani anadai kuwa waajiri wake wamekuwa wakitafuta visingizio kadha wa kadha ili kuipindisha kesi yao.
“Ninachotaka kwao ni huduma za matibabu kwa sababu hata wakinipa mshahara wa miezi minne niliyofanya kazi, sitaweza kufanya kazi sehemu nyingine  kwa sababu tayari ni mgonjwa,” anasema
Shabani  ambaye ana mke na watoto sita anasema amejaribu kutafuta msaada  kutoka kwa mashirika na taasisi  kama Kituo cha Haki za Binadamu(LHRC) na Baraza la Usuluhishi(CMA)
Si hivyo tu, bali pango la nyumba limekwisha na ameshavumiliwa na mwenye nyumba kwa miezi mitatu sasa.
Anasema mwajiri wake alimwambia kuwa  anatakiwa kuchangia shilingi elfu 50  kwa miezi kumi aliyofanya kazi lakini hakukuwa na mchango wowote katika mfuko wake.
“Kilichonishtua ni kuwa nilipokwenda kuangalia mafao yangu NSSF nilikuta hakuna mchango wangu hata mmoja,” anasema
Aidha Shabani analalamika kuwa  hata viongozi wa serikali za mitaa wanaonekana kupewa rushwa ili suala  lake lisitatuliwe.

Madhara ya kiafya yatokanayo na madini ya Uranium
 Madini ya uranium hutumika kutengeneza silaha za nyuklia ambazo zinapingwa vikali kutokana na uhatari wake.
Mabaki (residual)ya  madini hayo yanayotajwa kuwa na madhara makubwa kiafya katika mwili wa binadamu. Madhara hayo yanaweza kuwa ya kikemikali na kimionzi.
Sumu iliyopo katika madini hayo inaweza kuingia mwilini kwa kuvuta hewa yenye vumbi la uranium au kwa kula vitu vyenye chembe za madini hayo.
Vumbi au chembe hizo huingia katika mzunguko wa damu na kuchujwa katika figo jambo ambalo linasababisha figo kuathirika na kushindwa kufanya kazi.
Watu wanaofanya kazi katika maeneo au machimbo ya uranium, kama kubeba na kukanyaga  wapo hatarini kupata saratani pale wanapovuta hewa yenye vumbi lake au kumeza chembechembe zake.
Madhara ya mionzi kwa wachimbaji na wasagaji wa madini ya uranium nchini Marekani hayakugundulika mapema. Miaka ya 1940 na 50 ndipo wengi wao wlaipogundulika na saratani ya mapafu.
Mwaka 1962 takwimu za mahusiano kati ya uchimbaji wa uranium na saratani na mwaka 1990  serikali ya nchi hiyo iliunda sheria (RECA) kuwalinda na kuwalipa mafao walioathirika na madini hayo. Hadi sasa, zaidi ya asilimia 50 ya migodi ya uranium imetelekezwa.

No comments:

Translate