tangazo

Tuesday, November 6, 2012

SHERIA YA USHOGA YASITISHWA NCHINI MALAWI

Rais wa Malawi Joyce Banda

Serikali ya Malawi imesitisha rasmi mswaada wa sheria ya kupinga mapenzi ya jinsia moja.

Polisi wameagizwa kutowakamata watu wanaojihusisha nayo, mpaka hapo uamuzi utakapotolewa wa kuendelea na sheria hiyo au la.

Mapenzi ya jinsia moja nchini Malawi yamepigwa marufuku na kutolewa kifungo cha miaka hadi kumi na minne jela kwa wanaokamatwa kushiriki.

Baadhi ya viongozi wa kimagharibi wametishia kusitisha kuzipa msaada nchi za Afrika ambazo zinakataa kutambua haki za mashoga

Ushoga ni haramu katika nchi nyingi za Afrika na linasalia kuwa swala tete katika jamii nyingi za Afrika zenye kukumbatia maadili ya kiafrika.

Mmoja wa viongozi wa kijamii wenye ushawishi mkubwa, bwana Kaomba, amiomba serikali kutoruhusu bunge kubadili sheria zake kuhusu ushoga. ''Hii ni kinyume na maadili'' alisema kiongozi huyo.

Mwandishi wa BBC mjini Blantyre Raphael Tenthani, anasema kuwa kusitisha kwa muda sheria hiyo, itawaudhi sana watu wengi hasa viongozi wa kidini pamoja na watu kwa ujumla.

Mnamo mwaka 2010, wanaume wawili walikamatwa na kushtakiwa kwa utovu wa nidhamu hadharani baada ya kusema kuwa wataoana.

Kesi hiyo ilivutia sana kero kutoka kwa jamii ya kimataifa na hata kusababisha baadhi ya wahisani kusitisha msaada kwa nchi hiyo, na ikawa pigo kubwa kwa nchi hiyo ambayo ni moja ya nchi maskini zaidi duniani.

Rais wakati huo akiwa , Bingu wa Mutharika - aliwasamehe wanaume hao kwa misingi ya kibininadamu ingawa alisisitiza kuwa ni kinyume na maadili ,na tamaduni za kiafrika na hata sheria za nchi.

Hata hivyo rais Joyce Banda, aliyemrithi Bingu aliwaambia wabunge kuwa anataka kubatilisha sheria hiyo na kuhalalisha mapenzi ya jinsia moja.

No comments:

Translate