tangazo

Thursday, November 22, 2012

WAHITIMU WA CHUO CHA UDOM WASOTEA MAJOHO


 Baadhi ya wahitimu wa chuo kikuu cha Dodoma wakiwa kwenye foleni tayari kwa kuchukua majoho yao ambayo watayavaa katika sherehe za kumalizia safari yao ya miaka mitatu ya masomo yao ya Chuo Kikuu Cha Dodoma hapo Jana na leo
Foleni ikiwa haisogei kabisa huku wengine wakiendelea kusubiri na wengine kupiga stori mara baada ya kutokuonana takribani miezi minne tokea walipomaliza masomo yao chuoni hapo
Wahitimu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma UDOM kitivo cha Sayansi ya Jamii, Sanaa na Lugha wakiwa kwenye foleni ya kuchukua majoho tayari kwa kuhudhuria sherehe za mahafali ya tatu ya chuo kikuu cha Dodoma yanayotarajia kufanyika tarehe 21 na 22 Novemba 2012 katika viwanja vya Chimwaga 
Hapo mwenye nguvu ndie alikuwa wa kwanza kuingia na mnyonge alisubiri yote hiyo wakigombania kuingia wa kwanza kwaajili ya kuchukua majoho tu
 Huku wengine wakiwa wamejikalia zao chini wakisubiri vurugu za kuingia kwaajili ya kuchukua majoho ziishe nao waingie kuchukua majoho yao
Baadhi ya wahitimu mara baada ya kuchukua majoho yao tayari kwaajili ya sherehe za mahafali ya tatu ya Chuo Kikuu cha Dodoma yanayotarajiwa kufanyika tarehe 21 na 22 novemba 2012 katika viwanja vya Chimwaga Chuoni hapo
 Mara Baada ya Kuchukua Majoho yao Wahitimu hawa waliyajaribu kwanza kuona yanawatosha huku wengine wakisema kuwa "safari hii Majoho Yanatolewa Kwa GPA likikuenea GPA yako ni kubwa lisipokuenea GPA Yako ni Ndogo"

No comments:

Translate