tangazo

Saturday, February 23, 2013

KAHABA AJIFUNGUA NA KUTUPA MTOTO.

Stori:Dustani Shekidele, Morogoro
MTOTO mchanga hivi karibuni ametupwa katika Mto Kikundi mjini hapa akiwa amekufa, jirani kabisa na kambi ya makahaba wanaofanya biashara ya kuuza miili yao 

‘machangudoa’. Baadhi ya watu walioshuhudia mwili wa kichanga hicho walimwambia mwandishi wetu kuwa kichanga hicho kilitupwa na mmoja wa makahaba, hali iliyozua tafrani kwani wasichana wanaoaminika kuwa ni makahaba walikuwa wakiipinga kauli hiyo.

“We mpigapicha usiamini hayo wanayosema hao watu... tuna ujinga kiasi gani tuzae, tuue kisha tutupe mtoto sehemu yetu ya kazi?” alihoji msichana mmoja ambaye alikataa kujitambulisha.

Hata hivyo, wasichana waliojitambulisha kwa majina Pendo Komba, Rose Joseph na Amanda Athuman kwa nyakati tofauti walisema wanaofanya unyama huo ni makahaba japokuwa wenyewe wanakataa.

Walidai kuwa hii ni mara ya sita kwa watoto wachanga kutupwa kwenye eneo hilo.
Afisi mmoja wa polisi aliyekuwepo eneo hilo, (jina tunalihifadhi) wakati wanauchukua mwili wa kichanga hicho alisema wanamtafuta mwanamke aliyefanya ukatili huo ili afikishwe mahakamani.

No comments:

Translate