tangazo

Tuesday, February 5, 2013

STAR TIMES SASA YAANZA KUKODISHA VING'AMUZI


KAMPUNI ya Star Media imeanzisha huduma mpya ya kukodisha ving’amuzi kwa wateja wao, ili kujipatia matangazo ya televisheni kwa mfumo wa dijitali ambao ulianza kutumika rasmi mwanzoni mwa mwaka huu.

Ving’amuzi hivyo vilivyoanza kutolewa jana kwa mkopo, vinawalenga watu wote ambao wako tayari kunufaika na fursa hiyo.

Viitakuwa na chaneli 15 zikiwamo za Tanzania na nyingine zitazoongezwa.
Meneja Masoko wa Star Times, David Kisaka alisema masharti ya kupata huduma hiyo ni mteja kulipia Sh39,000 kama dhamana ya king’amuzi, Sh6,000 ikiwa ni kukodisha.

“Hii ni promosheni ya mwaka mmoja hadi mitano, muda utaanza kuhesabiwa rasmi mteja atakaposaini mkataba wa makubaliano na Star Times. Pia, mteja anaweza kuongeza mkataba wa ukodishaji hata baada ya miaka mitano kumalizika,” alisema Kisaka.

Alisema ili kupata huduma hiyo kwa mara ya kwanza, mteja anatakiwa kusoma, kuelewa na kujaza fomu ya makubaliano ambayo yamefuata sheria na haki zote kulingana na Katiba ya Tanzania.

Kisaka alisema Star Times wakishirikiana na TBC na Star Communication Technology wamejipanga kikamilifu kusambaza huduma za dijitali maeneo mbalimbali nchini kwa gharama nafuu.


No comments:

Translate