tangazo

Monday, February 18, 2013

SILAHA ZATEKETEZWA KWA MOTO.

      
Askari wa Polisi akiangalia zoezi la uteketezaji wa  Silaha haramu uliozinduliwa na Makamu wa Rais Dk Mohammed Ghalib Bilal uliofanyika  Ukonga jijini Dar es Salaam jana.Picha na Venance Nestory  

ZAIDI ya silaha haramu 3,100 zimeteketezwa ili kukabiliana na uhalifu unaokumba nchi za Afrika Mashariki.

Akizungumza kwenye mkakati huo kuangamiza silaha hizo Dar es Salaam jana,  Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal  alisema bado  kuna kazi kubwa  kukabiliana  na migogoro eneo hilo kutokana na wimbi la umiliki wa silaha haramu.

Silaha hizo ziliteketezwa kwenye viwanja vya Magereza Ukonga,  huku viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa wakihudhuria.

Dk Bilal alisema migogoro mbalimbali na usugu wa matukio ya uhalifu katika jamii,  yanachangiwa  na uwapo wa silaha ndogo na kubwa ambazo zinazomilikiwa kinyume cha sheria.

Alibainisha kuwa  takwimu zinaonyesha kuna sillaha 500,000  ukanda wa nchi za Afrika  Mashariki zinamilikiwa na watu wa aina mbalimbali kinyume cha sheria, jambo ambalo linasababisha kuongezeka kwa matukio tofauti hasa maeneo ya mipakani.

Translate