tangazo

Saturday, February 23, 2013

PEMBE ZA NDOVU ZENYE THAMANI YA MAMILION ZAKAMATWA.

 
Gari la Kampuni ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA likirejea katika Ofisi ya Kanda ya Kusini Magharibi ya Pori la Akiba la SELOU likitokea ndani ya Pori 
Hawa ni wafanyakazi wa Game frontiers of Tanzania wakiwa wamebeba pembe za ndovu


Pembe za ndovu, Risasi na Silaha zilizokamatwa
 ………………………………………………………………………………..
Na Hamza Mashole  wa  Songea- ( www.demashonews.blogspot.com)
Kampuni ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA kwa kushirikiana askari wanyamapori wa Selou na Askari wa vijiji vinavyozunguka pori la Akiba la Selou wamefanikiwa kukamata meno ya tembo 15 yenye thamani ya milion miambili, Risasi 9, Bunduki moja aina ya RIFFLE 458 na Gobole moja ambavyo hutumika kuulia wanyama .
Doria hiyo imechukua takribani siku tatu katika pori la Akiba la Selou ikiwa ni sehemu ya kuwatafuta majangili wanaofanya mauaji ya wanyamapori katika pori hilo,
Akizungumza na mwandishi wetu Bw. Mohamed Mpapa ambaye ni mwakilishi wa kampuni hiyo ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA, Amesema kuwa hiyo ni kujituma kutokana na motisha ya fedha anayoitoa mwezeshaji wa kampuni ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA ndio chachu ya mafanikio ya kukamata meno,bunduki na risasi.
 Akiendelea kuzungumzia tukio hilo Bw. Mohamed Mpapa amesmea baada ya majangili kuwaona Game Frontiers Tanzania wakiwa katika doria ndani ya pori hilo huku wakiwa wamekamilika kimapigano majangili hao waliweza kukimbia na kuacha nyara hizo baada ya kuona nguvu yao ni ndogo katika kupambana na kundi la doria.
Ameongezea kwa kusema Kampuni yake imefurahishwa na mafanikio na ushirikiano uliopo kati yao, Serikali na wanavijiji kukabiliana na ujangili unaoendelea kuwamaliza tembo katika Pori la Akiba la Selou pia ametoa wito kwa jamii kuendelea kutoa ushirikiano katika kuwafichua majangili.
Nae Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kusini Magharibi ya Pori la Akiba la Selou Bw. Bernald Lijaji amesema Pembe zilizokamatwa ni 15 pamoja na Bunduki aina ya RIFLE 458,Gobole moja na Risasi 9 aina ya 458 vimekamatwa katika Doria iliyofadhiriwa na Mwekezaji wa Kampuni ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA

No comments:

Translate