Na John Banda, Dodoma
Mwanafunzi wa kidato cha pili katika
shule ya Sekondari Nzuguni iliyopo manispaa ya Dodoma amekufa kwa
kujichoma moto baada ya Mjomba wake kumchapa viboko kutokana na kosa la
kutomsaidia Bibi yake kuosha vyombo.
Tukio la kifo cha mwanafunzi huyo lilitokea jana jumapili ambapo saa 11 jioni katika hospital Rufaa ya General Dodoma baada ya kulazwa kwa masaa kadhaa

.
Akisimulia kifo marehemu nyumbani kwa mwenyekiti wa mtaa wa maweni B. mjomba wa marehemu Paul Samwel 21 alisema kuwa siku hiyo ya tukio alitoka kazini kwake mapema akarudi nyumbani na kumkuta mama yake akiingia jikoni baada ya kutoka kuosha vyombo ndipo alipotaka kujua alipo Catherine kwani siku hiyo ya ijumaa wanawahi kutoka shule.
Samwel alisema mama huyo alimjibu kuwa Katherine alipofika alitoka na hajui alipoelekea ndipo alipomsubili mpaka aliporudi akamuuliza kwamba kwanini alimuacha Bibi yake afanye kazi wakati anajua haoni vizuri ndipo akamua kukata fimbo na kuanza kumchapa alipotosheka akamuacha baada ya muda akiwa nyumba jirani alisikia kelele nyumbani.
''ndugu yangu nilikuta mjomba anaungua mwili mzima kuanzia kichwani tuliposaidia na kumpeleka hospital mwili wote haukuwa na kazi bali moyo tu ndiyo ulikuwa ukidunda pekee na jana jumapili saa 11 jioni alikata roho kwa weli ameniuma sana maana ni kama mdogo wangu maana mama yake alimuacha akiwa mdogo sana'', alisema Samwel
Kwa upande wa Wanafunzi wenzake waliofika kuomboleza nyumbani hapo walisema Marehemu alikuwa akilalamika mara kwa mara kuwa alikuwa akiteseka sana nyumbani kiasi cha kila siku kupewa adhabu za vipigo na mjomba wake huku akitaka fedha kwa Babu yake za kunulia vifaa vya shule na mahitaji mengine kama mtoto wa kike alikuwa anachapwa pia.
Wanafunzi hao Desleria Lupembe, Elika Zabron, Maria Paul na Anastadhia Boniface Wote wa kidato cha pili Nzuguni walisema kwa siku zilivyokuwa zinazidi kusogea karibu na kifo chake walikuwa wakimshangaa mwenzao huyo.
''Mara kwa mara alikuwa akituambia wakati wowote atakufa hivyo tumpe picha zetu ili awe anatuangalia na sisi hapa unayetuona tulishampa zetu, lakini alhamis akawa serios sana akasema mambo yamezidi hata jumatatu hatakuja shule na hatutaonana kwasababu siku hiyo alinyimwa hela na Babu yake mzee Samwel pamoja na kuchapwa sana huku akiambiwa amfuate mama yake'', alisema Maria paul [15]
Nae Bibi wa marehemu Juliana Samwel akizungumzia tukio hilo alisema baada ya kuchapwa na mjomba wake Kathe alichukua mafuta ya taa na kujimwagia mwili mzima na mengine akayanywa kisha akijiwasha na njiti ya kiberiti akawaka mwili mzima kiasi cha yeye kushindwa kumsaidia.
mwanangu mtoto aliungua karibu mwili mzima maana alikuwa amejiviringisha kanga toka chini mpaka juu nilipiga kelele majirani wakaja kuzima ule moto na kumbe alishaungua sana hata ngozi ilikuwa ikijichubua yenyewe, mzee Samwel angekueleza mengi lakini kaenda hospital kuuhifadhi mwili maana mama ya mrehema ndiyo leo anatoka Dar hivyo mazishi ni kesho mapema, kuhusu kifo sina cha kufanya imetokea imetokea nitafanyeje'', alisema. mama huyo wa umri kati ya 50/55
Kwa upande wa majirani walisema tukio hilo lilikuwa la kutisha na si la kawaida kuwahi kutokea imeonyesha watoto wa sasa siyo wa kunyanyaswa hovyo, wakatoa ushauri kuwa kila mwenye mtoto akae na mwanae asimuamini mtu ndiyo sababu ya watoto wengi hasa wa kike kuharibikawa kutokana na kukosa uangalizi.

No comments:
Post a Comment