Akizungumza kwenye mkakati huo kuangamiza silaha hizo Dar es Salaam jana, Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal alisema bado kuna kazi kubwa kukabiliana na migogoro eneo hilo kutokana na wimbi la umiliki wa silaha haramu.
Silaha hizo ziliteketezwa kwenye viwanja vya Magereza Ukonga, huku viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa wakihudhuria.
Dk Bilal alisema migogoro mbalimbali na usugu wa matukio ya uhalifu katika jamii, yanachangiwa na uwapo wa silaha ndogo na kubwa ambazo zinazomilikiwa kinyume cha sheria.
Alibainisha kuwa takwimu zinaonyesha kuna sillaha 500,000 ukanda wa nchi za Afrika Mashariki zinamilikiwa na watu wa aina mbalimbali kinyume cha sheria, jambo ambalo linasababisha kuongezeka kwa matukio tofauti hasa maeneo ya mipakani.
1 comment:
safi sana yani.
Post a Comment