DAKTARI
wa kitengo cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa Mbeya,Paul Kisabi (32),
amefikishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Mbeya, akikabiliwa na mashitaka mawili
ya kushawishi na kupokea rushwa ya shilingi 100,000 kutoka kwa mgonjwa
aliyefikishwa Hospitalini hapo baada ya kupata ajali.
Hatua hiyo imekuja baada ya Taasisi ya kuzui na
Kuipambana na rushwa nchini takukuru, kumtia mbaroni daktari huyo juzi kwa
tuhuma za kupokea rushwa ya kiasi hicho cha fedha baada ya kumuwekea mtego.
Daktari huyo Kisabi amepandishwa kizimbani majira ya saa 3:45
na kusomewa mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Mbeya,
Fransis Kishenyi, aliyepangiwa kusikiliza kesi hiyo ambayo imeibua hisia kali
kwa wananchi.
Katika kesi hiyo namba 237 ya mwaka 2012, upande wa mashitaka
uliongozwa na waendesha mashita wawili wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na
rushwa nchini (TAKUKURU), Joseph Mulebya na Nimrod Mafwele.
Waendesha mashitaka
hao walidai kuwa Disemba 19 majira
ya asubuhi akiwa katika sehemu yake ya kazi katika kitengo cha upasuaji,
mshitakiwa alitenda kosa la kwanza la kushawishi rushwa ya shilingi 200,000
kutoka kwa mgonjwa Meshack Brown, aliyefika hapo kwa lengo la kupatiwa
matibabu.
Walisema katika
kosa la pili, siku hiyo majira ya saa nane mchana akiwa katika baa moja iliyojulikana kwa jina la
Victoria iliyopo Jijini hapa, mshitakiwa alitenda kosa lingine la kupokea hongo
ya shilingi 100,000, huku akijua kuwa vitendo vyote hivyo ni kinyume na sheria.
Walisema kuwa kwa
mujibu wa sheria za taasisi hiyo,
makosa yote yaliyotendwa na mshitakiwa yanaangukia kwenye kifungu cha 15 ibara
ya 1 (a) cha sheria ya kuzuia rushwa namba 11 ya mwaka 2007.
Kabla kupangwa tarehe ya kutajwa tena kesi hiyo,
Wakili wa mshtakiwa huyo,
Ladislaus Rwekaza,aliiomba mahakama impe dhamana mteja wake akidai kuwa makosa
yanayomkabili yanadhaminika.
Hakimu Kishenyi alikubaliana na maombi ya Wakili Rwekaza kuwa mashtaka yote
yanayomkabili mshtakiwa yanadhaminika na kusema dhamana yake iko wazi.
Alimtaka mshtakiwa
huyo kutimiza masharti ya kuwa na
mdhamini mmoja ambaye atasaini mali yenye thamani ya Sh,500,000, na kwamba awe
na utambulisho wa barua kutoka kwa kiongozi wa serikali ya mtaa .
Hata hivyo mahakama ililazimika kuahirishwa kwa
muda wa dakika 20 ili kutoa nafasi kwa
mdhamini wa mshitakiwa kuleta barua hiyo baada ya kudai kuwa alikuwa ameisahau
kwenye gari lililokuwa nje ya jingo la mahakama.
Baada ya kupokea
ombi hilo hakimu Kishenyi
aliwahoji waendesha mashitaka kama wameridhika na hoja, ambao kwa pamoja
walikubali kwa maelezo kuwa dhamana ni haki ya kisheria kwa mshitakiwa hivyo
hawakuwa na pingamizi.
Mshitakiwa aliweza kutimiza masharti ya dhamana hiyo na
hivyo kuachiwa huru hadi januari 7 mwaka 20013 ambapo kesi hiyo itaendelea
kusikilizwa katika mahakama hiyo.
Kwa mujibu
wa kumbukumbu za mahama hiyo, mshitakiwa huyo Daktari Kisabi ni mmoja wa
mashahidi wa kesi nyingine inayoendelea mahakamani hapo ya mtoto Anethi
anayedaiwa kuchomwa moto katika mkono wake, kufungiwa ndani na kulazimishwa
kula kinyesi chake na Shangazi yake.
Habari na moses
picha Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment