tangazo

Tuesday, December 18, 2012

Bajeti finyu yaathiri somo la Tehama

                                 
BAJETI finyu inayotengwa katika sekta ya elimu nchini, imechangia shule nyingi za msingi mjini Kibaha kushindwa kufundisha somo la teknolojia ya mawasiliano (Tehama).

Hatua hiyo imekuja baada ya Shule ya Msingi Miembesaba Kata ya Kongowe wilayani Kibaha kushindwa kufundisha somo hilo, baada ya Serikali kupigia kelele somo hilo kufundishwa katika shule za msingi.

Akizungumza katika mkutano uliokutanisha wadau mbalimbali, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Miembesaba, Rajabu Chalamila alisema hadi sasa wanashindwa kufundisha somo hilo kutokana na ufinyu wa bajeti.

“Ufinyu wa bajeti hiyo imekuwa ndio chanzo cha shule yetu kushindwa kuanza kufundisha somo la Tehama ukilinganisha na shule nyingine ambazo tunalingana nazo,”alisema Mwalimu Chalamila.

Naye Diwani wa Kata ya Mailimoja, Endrew Lugano alisema katika sekta ya elimu bajeti ya mwaka 2012-2013 serikali imetenga Sh17 bilion hali inayochangia kuonekana haiwezi kukidhi mahitaji ya elimu, hivyo wananchi wametakiwa kuongeza juhudi katika kuchangia wa elimu.

Alisema kutokana na bajeti hiyo kuwa ndogo kulingana na mahitaji makubwa katika sekta ya elimu mjini hapa, aliwataka wananchi kuchangia elimu na sio kutegemea halmashauri pekee.

“Halmashauri ina nafasi yake lakini pia kwa kuangalia hilo wananchi pia mnatakiwa kuunga mkono kwa kuchangia sekta ya afya ili kuweza kuwawawekea malengo mazuri kwa vizazi vijavyo,”alisema Lugano.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa Fikra Huru, Hancy Mahenge alisema bajeti haina mtazamo wa kijinsia na kutolenga mahitaji halisi ya mwananchi wa kawaida pesa nyingi zinaelekezwa kwa viongozi badala ya wananchi.

No comments:

Translate