Na: Burhani Yakub, Muheza
FAMILIA ya msanii Hussein Ramadhani Mkiety (Sharo Milionea)
aliyekufa katika ajali wilayani Muheza wiki
iliyopita imedai kuwa
haiamini kwamba kifo cha mtoto huyo kilitokana na ajali, hivyo kulitaka
Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina kubaini ukweli.
Mjomba wa marehemu , Mohamed Msenga alisema jana kwamba familia imekuwa
na shaka juu ya mazingira ya kifo hicho baada ya kurejeshewa nguo za
msanii huyo zilizokuwa zimeibwa baada ya ajali lakini hazikuwa na damu.
Msenga alisema muda mfupi baada ya mama mzazi wa Marehemu Zaina Mwaimu
Mkiety (54), kuitwa polisi na kukabidhiwa vitu mbalimbali zikiwamo nguo
ambazo marehemu alikuwa amevaa siku ya ajali hawakuona hata alama ya
damu jambo ambalo liliwashangaza.
Alisema shaka hiyo ilianzia katika eneo ambalo ajali hiyo ilitokea
akisema walipofika na kuonyeshwa mahala alipokuwa ameangukia, hawakuona
damu jambo ambalo liliwatia shaka.
Alisema begi la nguo za msanii huyo lilikuwa na udongo mwingi
likionyesha kwamba walioiba walikuwa wamelifukia kabla ya kusalimisha
lakini hakuna damu zilizoonekana.
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Teule Muheza, Dk Julius Mjema
aliyeufanyia uchunguzi mwili wa Sharo Milionea alisema sababu ya kifo
chake ni kichwa kupondeka.
“Mimi ndiye niliyefanyia ‘postmoterm’ (uchunguzi), mwili wa Sharo
Milionea, ni kwamba kichwa kilikuwa kimepondeka huku mifupa ya kichwa
ikiwa imepondeka pia,” alisema Dk Mjema.
Kuhusu madai ya nguo kutokuwa na damu, alisema marehemu alipata mpasuko
wa ndani kwa ndani na siyo wa nje, ndiyo maana alipofikishwa chumba cha
maiti damu zilionekana zikiwa zimeganda masikioni.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Constantine Massawe
alipoulizwa kuhusu madai hayo ya familia alisema: “Hiyo ni taarifa
ambayo jeshi la polisi litaifanyia kazi kwa kuingia kwa kina katika
kuchunguza ili kuridhisha pande zote.”
Mama yake alia kukosa mjukuu
Katika hatua nyingine, mama mzazi wa msanii huyo amesema kutoachiwa mjukuu na tarehe za mwisho wa mwezi ni alama ambazo zitasababisha awe akimkumbuka mwanaye huyo milele. Akizungumza nyumbani kwake, katika Kitongoji cha Jibandeni Kijiji cha Lusanga wilayani hapa alisema kila ulipokuwa ukifikia mwisho wa mwezi ulikuwa ni muda wake wa neema kwani Sharo Milionea alimtumia fedha za matumizi yake binafsi pamoja na familia nzima nyumbani hapo.
Katika hatua nyingine, mama mzazi wa msanii huyo amesema kutoachiwa mjukuu na tarehe za mwisho wa mwezi ni alama ambazo zitasababisha awe akimkumbuka mwanaye huyo milele. Akizungumza nyumbani kwake, katika Kitongoji cha Jibandeni Kijiji cha Lusanga wilayani hapa alisema kila ulipokuwa ukifikia mwisho wa mwezi ulikuwa ni muda wake wa neema kwani Sharo Milionea alimtumia fedha za matumizi yake binafsi pamoja na familia nzima nyumbani hapo.
“Pamoja na kwamba kila mara alikuwa akinitumia fedha za kutatua
shida zangu mbalimbali nilizokuwa nikimweleza lakini kila mwisho wa
mwezi alikuwa akihakikisha anatuma fungu la matumizi yangu na ndugu zake
hapa nyumbani,” alisema mama huyo.
Alisema mwisho wa mwezi itakuwa ni
alama ya kudumu ya kumbukumbu ya mwanawe kwa sababu ni wakati ambao
alikuwa akimtumia fedha za matumizi yake pamoja na
familia nzima.
Kuhusu mjukuu alisema: “Sharo ni mwanangu wa pekee wa kiume, amekufa
bila kuniachia mjukuu.. hii inaniuma sana lakini namshukuru Mungu kwani
amechukua kiumbe chake na ndiye ajuaye siri iliyofichika mbele yangu,”
alisema.
Alisema hadi alipofariki hakuwahi kumdokeza juu ya kuwa na mtoto wala
kumpa mimba msichana yeyote… “Unajua Sharo Milionea alizaliwa pacha na
mwenzake Hassan lakini mwenzake alifariki dunia siku tano baada ya
kuzaliwa kwa hiyo katika kizazi changu mwanangu pekee wa kiume alikuwa
Sharo Milionea ambaye nilitumaini kwamba angeniletea wajukuu,” alisema
Zaina.
No comments:
Post a Comment